Arusha Press Club tumeaibisha - Kifo cha Mwangosi

chachana

Member
Aug 4, 2011
57
92
Viongozi wa Arusha Press club tumeshindwa kuwaelewa. Tumekaa tukisubiria wote kufanya maandamani ya AMANI kupinga mauaji ya kikatili aliyofanyiwa daudi mwangosi. Tumeshangaa wamekuja na taarifa kutoka POLISI kuwa maandamano yamezuiliwa kwa sababu darasa la saba wanajiandaa na mitihani. Jamani upuuzi gani huu.......!!
Tatizo ni viongozi wa Arusha Press club waoga na wengi ni waganga njaa wa mfumo wa kifisadi. Leo ni kwa mwangosi kesho.......??
 
waandishi wengi kimsingi ni waganga njaa na wapenda rushwa wakubwa hata hili la Mwangosi wanalishikia bango kwa kuwa ni mwandishi mwenzao ila yapo mengi machafu wanafumbia macho kutokana na njaa na rushwa! wapo wachache wanaozingatia weleni na nidhamu ya uandishi ila wengi wao ni njaa kali!!
 
Waandishi woga wekeni pembeni jikomboeni, hii serikali bila bango haitendi haki,tafadhalini jikomboeni tutawaunga mkono, bila nyie tutauwawa wengi na kuchimbiwa kimyakimya nani atatuhabarisha.
 
Jamaa tulizuiliwa kwasababu ya ugeni mkubwa ulioko hapa jijini Arusha...
 
Kweli john mhala, gwandu na wanafiki na waoga wengine. Ajabu hata baadhi ya waandishi wa gazeti la mwananchi arusha hawaeleweki baadhi wapo kwenye payroll za vigogo waliopo kwenye system wanatunzwa.
 
Kwa hili la kutofanya maandamano ya amani kwa kweli limenisikitisha, mbona mtihani wa darasa la saba bado?
 
Viongozi wa Arusha Press club tumeshindwa kuwaelewa. Tumekaa tukisubiria wote kufanya maandamani ya AMANI kupinga mauaji ya kikatili aliyofanyiwa daudi mwangosi. Tumeshangaa wamekuja na taarifa kutoka POLISI kuwa maandamano yamezuiliwa kwa sababu darasa la saba wanajiandaa na mitihani. Jamani upuuzi gani huu.......!!
Tatizo ni viongozi wa Arusha Press club waoga na wengi ni waganga njaa wa mfumo wa kifisadi. Leo ni kwa mwangosi kesho.......??

Kitu usichokijua wewe piga kimya tu!

Eti darasa la saba wanajiandaa kwa mtihani ndio izuie maandamano!
 
ama kweli polisi vichwa vyao ni nazi..yaani mtu mzima unaweza ukatoa sababu ya kipuuzi kama hiyo?...eti darasa la saba wanajianda na mitihani, kwani hao wandishi wa habari ndio walimu wao? au hayo maandamano yanafanyikia madarasani? ...na nyie waandishi hamkuweza kuhoji uhusiano wa maandamano yenu na maandalizi ya mtihani kwa darasa la saba?
 
Hao viongozi wa Arusha Press Club hawafai, hawana ushirikiano, waoga na inawezekana ni double agents. Baadhi ya waandishi wa habari hutumika serikalini kwa kuitwa wadau. Wanaotumika hawafai kuwa wanachama. Hao wa Arusha wafutwe uongozi mara moja.

Mwangosi kafa kishujaa kutokana na kuwa kiongozi pekee aliyeingia katikati ya kundi la mbwa mwitu (polisi) ili aweze kumwokoa kondoo wake (Godfrey ambaye ni mwandishi mwenzake) aliyekuwa akiraruliwa na mbwa hao. Huyo ndiye mfano wa kiongozi anayetakiwa na kufuata nyayo zake katika kazi,jamii na Taifa kwa ujumla. Siyo bora viongozi uchwara.
 
Viongozi wa Arusha Press club tumeshindwa kuwaelewa. Tumekaa tukisubiria wote kufanya maandamani ya AMANI kupinga mauaji ya kikatili aliyofanyiwa daudi mwangosi. Tumeshangaa wamekuja na taarifa kutoka POLISI kuwa maandamano yamezuiliwa kwa sababu darasa la saba wanajiandaa na mitihani. Jamani upuuzi gani huu.......!!
Tatizo ni viongozi wa Arusha Press club waoga na wengi ni waganga njaa wa mfumo wa kifisadi. Leo ni kwa mwangosi kesho.......??

Ahaaaa kumbe wachumia tumbo hawa? Sasa huko AR si ndiko vurugu za SSM kubwa? Itakapowafika nyie itakuwaje? Ile kuna tetesi kiongozi wao anaandikia gazeti la Uhuru, la Chama cha Mapinduzi!!!! Yaani kweli mmekubali kutumika kama tambara? Juzi mlijitetea kuna mkutano wa mazingira, leo mtihani. Kwani maandamano ya amani yana shinda gani na watu wako mkutano na wengine madarasani? Ok Fisadis at worl. Bravo men!
 
John Mhala ni mwakilishi wa gazeti la uhuru unategemea nini ?.

Huyu John Mhala by profesional ninavyomjua alikua ni Porter pale Hoteli ya New Safari Hotel enzi hizo! Namaanisha alikua ni mbeba mizigo ya wageni wanaofikia Hotelini hapo! gafla nikamuona anaandikia gazeti moja la hapa Arusha linaloitwa Arusha Raha nalo gazeti hilo limekufa kifo cha Mende kwakua lilikua liaandika habari za kuwapamba matajiri wa Mirerani! Gafla akaibukia kwenye kampuni ya kuegesha magari kama bosi fulani! Akaingia mitini baada ya kampuni hiyo kufa kifo cha Mende baada ya mmiliki wa kampuni hiyo kuishia Magereza kwa tuhuma ya kuuwa na kupora madini ya wahindi fulani lakini akatoka baada ya miaka mitano! Huyu ndiye John Mhala ninayemjua kumbe anaandikia gazeti la UHURU?? Sizani kama angeweza kuandamana kwa njaa aliyonayo!
 
Nilimuona yule mwenyekiti wao anataja maandalizi mtihani wa darasa la saba kuwa ni moja ya sababu ya kutofanyika maandamano ya amani nikacheka sana
 
Back
Top Bottom