Arusha ni chanzo cha utajiri wa ma RPC na RCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha ni chanzo cha utajiri wa ma RPC na RCO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Sep 26, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa najiuliza sana mwenendo wa ma polisi na mapesa yao .Kuporomosha majumba makubwa kila koma kama Mahita na Tibaigana.Mtoa habari mmoja anasema kwamba kila aliye wahi kuwa RPC ama RCO Arusha lazima ni tajiri.Je Arusha kuna nini hadi wakubwa hawa wabakie kuwa matajiri wakati wameingia wakiwa watumishi wa kawaida na mshahara wao wajulikana ?

  Je ndiyo chanzo cha mauaji na ujambazi mkubwa Mkoa huu ?Mwenye nalo neno anipe msaada tafadhali .
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  umeshakimbia huko Tarime?
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Kibunango, unahitaji kweli degree 3 kuelewa kwamba mtu wa Arusha anaweza kuwa Tarime muda huu na tukaongea nami nikaja hewani kuuliza ? Niko Tarime na tunakomaa na Mtikila na wajinga wenzake kama Msekwa na Makamba .
   
 4. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nimeishi Arusha miaka mingi na kuna ukweli fulani kuhusu hili jambo, ingawa sina uhakika kama ma-RPC au RCO wa mikoa mingine hawana utajiri mkubwa. Pia wapo wengine ambao hawana utajiri unaoweza kuitwa utajiri, kwa mfano SACP Magoha alikuwa RCO Arusha, baadae akawa RPC pia hapo Arusha kabla hajahamishiwa Pemba kipindi kile cha "mauaji ya Pemba" ya Januari 2001. Licha ya kufanyishwa ile kazi chafu sana ya Pemba, sasa hivi ni babu tu mstaafu, analishwa na mkewe ambaye ni mwalimu wa primary school. Anaishi kwenye nyumba yake mwenyewe, lakini zaidi ya hapo "hana kitu". Alikuwepo pia SACP Peter Lucas kama RPC Arusha, lakini sasa hivi hasikiki kokote. DCP Alfred Tibaigana kweli anayo hela, pamoja na James Kombe na wote wamepitia Arusha, na labda ni kweli hizo hela zina uhusiano na Arusha. Sasa hivi Tibaigana amenuia kuingia kwenye siasa, na kuna tetesi zaidi ya tetesi kuwa anakusudia kumng'oa Masilingi kule Muleba.

  Wapo makamanda ambao walikuwa wanafahamika kuwa walikuwa wanasapoti ule mtandao wa wezi wa magari, cha ajabu mmojawapo alicheza karata zake vizuri na Mkapa akaukwaa u-IGP, huyu ni Omar Mahita. Wala hakuna siri juu ya uhusiano kati ya Omar Mahita na majambazi maarufu kama kina Babu Sambeke na Alex Massawe, kuanzia kipindi alipokuwa RPC wa Kilimanjaro. Huo uhusiano uliendelezwa pia na RPC aliefuata wa Kilimanjaro, Dr Mohamed Chicco (sijui aliko siku hizi). Mtandao huo wa majambazi Nairobi-Arusha-Moshi umedumu miaka mingi, na bila shaka usingeweza kufanikiwa bila sapoti pia ya ma-RCO na RPC wa Arusha, ambao wako katikati ya chain hiyo.

  Wakuu wengi wanapopelekwa Arusha (si polisi tu) huwa wanatajirika, hasa wanapojihusisha na mambo yanayotajirisha wengine kama madini na biashara ya utalii. Labda hata rushwa za pale ni "nene" zaidi kuliko sehemu nyingine! Mtakumbuka hata utajiri wa Lowassa "ulifumka" hasa alipokuwa pale AICC. Daniel ole Njoolay alikuwa mkurugenzi wa magazeti ya chama "Uhuru" na "Mzalendo", lakini Mkapa alipomzawadia ukuu wa Mkoa wa Arusha, aliibuka na kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa kwa kujigawia vitalu vya kuchimba Tanzanite kule Mererani. Hata alipohamishiwa Mwanza aliendelea kuonekana zaidi Arusha kwenye biashara zake. Sasa hivi yuko Rukwa, lakini "himaya" zake Arusha zinaendelea kustawi.

  Naweza kusema utajiri wa wakuu wa Arusha ni mchanganyiko wa mambo mengi, ikiwamo fursa nzuri zaidi za biashara, na wengine (nachelea kusema wengi) ufisadi.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Kithuku asante kwa shule hii .Naendelea kungoja maoni zaidi wakatu nazidi kushangaa uliyo yasema ni mazito na makubwa
   
Loading...