bushland
JF-Expert Member
- Mar 6, 2015
- 7,015
- 4,982
Kizaazaa jana kilitokea hapa jijini Arusha kwa wasajili wa laini wote katikati ya jiji la Arusha baada ya mzungu kusajiliwa laini ya simu kwa dollar elfu moja.
Mzungu huyo aliletwa na flycatcher kwa msajili huyo kusajili laini na makubaliano yalikuwa kati ya mzungu na flycatcher huyo aliemdaka barabarani wakati akiuliza wapi anaweza sajili laini, ndipo alipochajiwa dollar elfu moja na alitoa bila hiyana.
Baadae kabisa huko alikokuwa akakutana na mswahili na katika maongezi yao ndipo alimwambia amefurahi amepata simcard. Mswahili akamuliza sh. ngapi kauziwa na yeye kumjibu kuwa kachajiwa dollar 1000, ndipo mswahili huyo akawaka na kupeleka inshu polisi.
Polisi walifanya kazi yao ipasavyo kwani wasajili laini wote mjini walikamatwa na kupelekwa polisi. Taarifa za baadae zinadai kuwa Vodacom walienda polisi na kuwaomba wawaachie watu hao na wao Vodacom watamfatilia mtu huyo aliesajili hiyo laini na atakabidhiwa polisi.