Arusha MP says 'Dirty' phots are fake

Arusha MP says 'Dirty' phots are fake

Arusha.
lema.jpg

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameomba Bunge kuingilia kati kuchunguza na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, watu waliotengeneza picha zinazomkashifu na kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya jamii.

Akizungumza mjini hapa jana, Lema alisema picha hizo zimeanza kusambazwa tangu mwezi uliopita kwenye Mtandao wa Fikra Huru.

“Tayari nimemwonyesha picha hizi Spika Anne Makinda na Katibu wa Bunge, wakanielekeza niandike barua uchunguzi uanze na nimeandika barua tangu Novemba 11,” alisema Lema na kuongeza:

“Binafsi nina watu wangu, tumefuatilia na kubaini wanaoendesha mchezo huu ni baadhi ya vijana wa Jumuiya ya Vijana CCM (UVCCM), akiwamo mwenyekiti wake, Sadifa Juma Hamis na kada wa chama hicho, Mtela Mwampamba.”

Hata hivyo, Mwampamba alimshangaa Lema kumhusisha na utengenezaji picha hizo na kumshauri kwenda mahakamani kama ana ushahidi.

“Namwambia aache woga, kila siku anapohubiri hakuna dhambi kubwa kama woga, sasa kwa nini anakuwa mwoga, Lema afanye siasa zenye tija mbona anajiita kamanda, kamanda gani anakuwa mwoga aende mahakamani,” alisema.

Naye Sadifa alikanusha kuhusika na utengezaji wa picha hizo na kwamba, hana sababu ya kufanya hivyo kwani hana tatizo lolote na Lema.

“Natokea Zanzibar, yeye anatoka Arusha sasa kwa nini nifanye hivyo wakati sina tatizo lolote na yeye, hili suala lenyewe ndiyo nalisikia leo,” alisema Sadifa na kuongeza:

Lema alidai mwenyekiti huyo alikuwa akisambaza picha hizo bungeni, akiwaonyesha wabunge mbalimbali hatua ambayo ilimsababisha kupeleka malalamiko kwa Katibu wa Bunge na Spika.

Alisema alitaka kumvamia Sadifa akiwa bungeni kumpokonya simu yake aliyokuwa akitumia kusambaza picha hizo, lakini alizuiwa na Spika na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Source: Lema amshtaki Sadifa kwa Spika akidai kumkashifu - Siasa - mwananchi.co.tz
 
lema si alibaka kule uingereza?? ile kesi yake imefikia wapi? ushahidi huu hapa alivyobaka
lema kubaka.jpg
 

Attachments

  • lema kubaka.jpg
    lema kubaka.jpg
    194.1 KB · Views: 194
LEMA abaka


BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo (pichani) anamtuhumu mbunge mmoja ‘mtata' wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda (jina tunalo) kuwa amembaka, Uwazi lina kisa cha aibu ya karne. Katika uchunguzi wake, hivi karibuni gazeti hili lilielezwa kuwa kuna habari ya kashfa nzito inayomtafuna mbunge huyo anayetokea Kanda ya Kaskazini lakini haikufafanua kwamba inahusu nini.
VYANZO


Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa mahakamani huko London nchini Uingereza.
Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu' hivyo gazeti hili likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London kikazi.


MAZITO
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
"Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).




MAZOEA YAANZA


Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: "Nikiwa kwenye mkutano….(jina la mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi waliohudhuria mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo ili ionekane mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza) wengi.
"Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka kunipa kadi ya chama chake nikakataa, ndipo akadai kwamba mimi nilitumwa kwenye mkutano huo na balozi na rais kwa ajili ya ushushushu.


KISA KUJISAIDIA HAJA NDOGO
"Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa naondoka kurudi nyumbani kwangu, mbunge huyo na wenzake nao walitoka. Tukiwa njiani wenzake walikwenda kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba akajisaide nyumbani kwangu, nilimkubalia. Alipofika ndani, bila kujua kila kitu kinaonekana kwenye kamera alinibadilikia kama vile adui vitani, ona sasa wema wangu ukawa umeniponza.


HADI KITANDANI
Alinirukia, akaniburuza hadi kitandani kwangu. Nilipokuwa mkali na kwa namna nilivyokuwa nimechanganyikiwa sishikiki ndipo akanivamia maungoni, akanichania nguo zangu akitaka nimwachie atimize lengo lake la kuniingilia kimwili kwa nguvu.
"Nilijitahidi ili asifanikiwe, nikamwambia amekwisha kwani lazima nimwanike ndipo akanipiga nusu aniue akisisitiza kuwa kama nitauanika uovu wake huo au kuchukua hatua zozote ataniua.
"Inaniuma sana, kunibaka anibake halafu atishie kuniua, unyama gani huu?"


AITA POLISI
Flora anaendelea kusema:"Katika purukushani hiyo, nilipopata mwanya kidogo tu, nikapiga namba ya polisi 999 kuomba msaada. Alipoona hivyo alitoka na kutokomea kusikojulikana. Polisi walipofika hawakufanikiwa kumkamata."


UBAKAJI/KUTISHIA KUUA
Flora alisema polisi walimchukua na kila kitu cha ushahidi zikiwemo nguo zake hadi kituoni, wakamhoji kwa kumrekodi sauti, wakampa namba ya jalada la kesi inayosomeka; 4621279/2012-UBAKAJI/KUTISHIA KUUA ambapo hadi leo mbunge huyo anasakwa na Polisi wa London, akikanyaga tu Uingereza lazima akamatwe akajibu tuhuma za ubakaji na kutishia kuua.
Flora akaongeza: "Ukweli ni kwamba hakufanikiwa kukamatwa kwa sababu alikuwa na passport za kidiplomasia ambazo nyingine hakutumia jina lake halisi.
"Kesho yake nilisikia alikimbilia Ujerumani, nikawaambia polisi lakini walikumbana na tatizo lile kwani majina niliyowapa siyo aliyotumia kuingia Ulaya.
"Januari mwaka huu nilipotaka kurudi nyumbani Kilimanjaro, mahakama ya hapa (Uingereza) ilinipa barua ambayo nilipofika niliipeleka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi nikafunguliwa faili Namba Mos/RB/17127/12 kwa ajili ya ulinzi chini ya R.C.O Ramadhan Ng'anza.


"Niliwaeleza kuwa mtu anayetaka kuniua ni mbunge huyo. Kweli waliahidi kunisaidia, nilipoondoka kurudi London niliwasiliana na polisi Kilimanjaro lakini niliona kama kuna kitu au mbunge huyo yupo juu ya sheria kwani walikana kunifahamu.




ASHINDA MAHAKAMANI
"Sitachoka kutafuta haki na kutetea wanawake wanaobakwa kila siku wanaona aibu kusema, naamini aibu haipo kwa mbakwaji bali kwa mbakaji, yule …. (anataka jina) ni mbakaji.
"Nimesharipoti mashirika mengi ya haki za binadamu ya Uingereza. Kuna siku nilishinda mahakamani, kule ni yeye tu anasubiriwa atiwe mbaroni akasimame kizimbani ndipo dunia itajua ninachokisema."


ASUBIRIWA KIZIMBANI
Flora allisema kama kweli mbunge huyo ni mwanaume aende tena jijini London kama hatasimamishwa kizimbani na kuozea jela."
Uwazi, kabla ya kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Kilimanjaro, RPC Robert Boaz, Jumamosi iliyopita lilimtafuta RCO Ng'anza ambaye alisikiliza mkasa mzima na kudai kuwa hamfahamu Flora lakini alipobanwa alidai yeye siyo msemaji wa jeshi hilo kisha akakata simu.


KAMANDA WA POLISI
Kwa upande wake RPC Boaz alisema kuwa kipindi kinachotajwa cha mwezi Januari yeye alikuwa likizo ndefu na hajawahi kusikia habari kama hiyo lakini akaahidi kuifuatilia kwa RCO Ng'anza na baadaye arudishe majibu kwa Uwazi.
Alipotafutwa tena Jumapili iliyopita kwa njia ya simu yake ya mkononi hakupatikana hewani.


SASA NI ZAMU YA MBUNGE
Kama ilivyo desturi ya Uwazi, Jumamosi hiyohiyo lilimtafuta mbunge anayetajwa katika aibu hiyo kubwa huku akiwakilisha wananchi wa jimbo lake ambapo alisomewa kisa kizima kisha akapewa nafasi kuzungumzia au kufafanua kashfa hiyo ya karne.


Huku akirekodiwa neno kwa neno, mheshimiwa huyo alisema: "Huyo mwanamke (akatajiwa jina la Flora Lyimo) simfahamu lakini usikubali kushiriki kwenye dhambi ya kunichafua kwa sababu ni uongo.


Uwazi: Kwa hiyo mheshimiwa hujawahi kusikia habari hiyo?
Mbunge: Niliisikia, ninaifahamu. Ina karibia miezi nane sasa kwani ameibuka sasa hivi?
Uwazi: Sasa kama hiyo habari ni ya uongo kwa nini usimshitaki?
Mbunge: Habari hiyo ipo mtandaoni, kama nikisema nishitaki mitandao nitashitaki mingapi? Mbona …(anautaja mtandao wa kijamii wa Tanzania) wameshanichafua sana. Nikianza kuhangaika na kesi najua miaka yote mitano nitakuwa mahakamani badala ya kuendesha harakati jimboni mwangu.
Uwazi: Kama anakusingizia kwa nini wewe?
Mbunge: Huyo ametumwa na …(jina la mwanasiasa mkubwa nchini) na …(jina la chama), huko ni kuchafuana kwa sababu kama ni kunikamata, nani asiyejua jimbo langu, ofisi yangu, nyumbani kwangu na umaarufu wangu? Mwambie aje sasa hivi anikamate.


TURUDI KWA MLALAMIKAJI
Baada ya kusikia majibu ya mbunge huyo, Uwazi lilirudi kwa mlalamikaji Flora na kumweleza alichokijibu mbunge huyo ambapo na yeye alisema:
"Nawatumia picha wakati akiingia na kutoka kwangu kwani huku kuna kamera za mtaani zinachukua kila tukio. Unajua lazima abishe kwa sababu ni aibu kubwa kwake na chama chake."


KUTOKA UWAZI
Sakati hili ndiyo tumeanza kulichimba, mambo mengi yataibuka kwa kuwa tunajiridhisha kwanza na muda wowote tutamwanika mheshimiwa huyo ili ajitokeze na kuthibitisha kuwa hakufanya kitendo hicho kwani mlalamikaji ameshasema yake




Kwa hisani ya - Flora Lyimo Blog
 
sasa yeye anahangaika na wanaosambaza badala ya kujihangaikia kwanza yeye aliyetenda
 
Huyu Sadifa si ndo yule bw.abwa toka zanzibar,hawezi vita na LEMA.
 
Ni jambo la kusikitisha kusikia Sadifa alishiriki mchezo wa kijinga kama huu Huyo mwehu mwingine aliyetajwa sishangai lakini of all the People Sadifa?

Kama TCRA hawatachukua hatua watakua wamebariki ufedhuli na sasa tutaona ni nani atakayebaki salama katika mchezo huu
 
Ni jambo la kusikitisha kusikia Sadifa alishiriki mchezo wa kijinga kama huu Huyo mwehu mwingine aliyetajwa sishangai lakini of all the People Sadifa?

Kama TCRA hawatachukua hatua watakua wamebariki ufedhuli na sasa tutaona ni nani atakayebaki salama katika mchezo huu
watakukoma, hawajui unatembea na sumu ee
 
Ni jambo la kusikitisha kusikia Sadifa alishiriki mchezo wa kijinga kama huu Huyo mwehu mwingine aliyetajwa sishangai lakini of all the People Sadifa?

Kama TCRA hawatachukua hatua watakua wamebariki ufedhuli na sasa tutaona ni nani atakayebaki salama katika mchezo huu

Hayo tena makubwa kiongozi wa muhimili mkubwa wa chama anaweza fanya hivyo
 
kiambatisho; Ushahidi wa mbunge Godbless Lema kumbaka flora lyimo wazidi kubainika


Taarifa za kweli kuhusu mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kumbaka mwanadada Flora Lyimo tarehe 8.8.2012 nchini Uingereza wakati wa ufunguzi wa tawi la chadema nchini humo umezidi kubainika.

Tarehe 2 -3, january 2013 akiwa tanzania, Flora aliwasilisha barua ya polisi wa uingereza kwa polisi kituo cha Moshi mkoani kilimanjaro na kufunguliwa jalada no.MOS/RB/17127/12.
Aidha tarehe 13/12/2012 Afisa upelelezi DC William Hughes wa kitengo cha uhalifu jeshi la polisi la uingereza kituo cha 4-6 shepherdess walk N17LF alifika ubalozi wa Tanzania nchini uingereza ili kujua pamoja na mambo mengine,
-Taarifa sahihi za GODBLESS LEMA
-Anuani yake
-Barua pepe
Ushauri kutoka mamlaka za Tanzania juu ya mikakati mizuri ya kushughulikia kesi hiyo ambayo inamuhusisha kiongozi wa chama kikubwa cha siasa na
-Wasifu wake.
Mbali na tukio hilo kuripotiwa ubalozini, vyanzo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na Gazeti la changamoto la tanzania toleo namba 348 la tarehe 18- 24 desemba 2012 lilichapisha taarifa ya tukio hilo kwenye ukurasa wake wa mbele.kwa kichwa cha habari "POLISI UINGEREZA WAMSAKA LEMA", Pia blog ya global publishers ya nchini tanzania katika report zake za tarehe 14 mei 2013 iliandika habari hiyo kwa kichwa cha habari "MREMBO;MBUNGE AMENIBAKA" Ambapo mrembo huyo (flora) alieleza alivyochaniwa na kufanyiwa kitendo hicho. alieleza kuwa lema alikuwa amemsindikiza mpaka nyumbani na walipofika LEMA aliomba aonyeshwe sehemu ya kujisaidia haja ndogo ndipo alipomvamia Flora na kumchania nguo na kutekeleza azma yake hiyo ovu.
Flora amekuwa akionekana katika shughuli mbalimbali za kijamii lakini ana wasiwasi kuwa anaweza kufanyiwa unyama na LEMA wakati akiwa Tanzania kwa sababu anasema anamfahamu lema pia kuwa ana asili ya ujambazi.
kiambatisho ni barua ya polisi wa kimataifa interpol kumweleza kuwa uchunguzi wa kesi yake unaendelea.
 
Lema ndio ajifunze sasa, kuwa siasa chafu sio nzuri, alidhani ni yeye tu anazijua sasa ajue SIASA CHAFU na wengine wanaziweza!
 
Inavyoelekea kila Disemba ikikaribia tutakuwa tunapitia vimbwanga vya hadithi za chadema nal hili litapita au litagota
 
Lema achana na hawa mabwabwa we fanya kazi ya kujenga chama.
 
Lema ndio ajifunze sasa, kuwa siasa chafu sio nzuri, alidhani ni yeye tu anazijua sasa ajue SIASA CHAFU na wengine wanaziweza!

katika hili unajisifia nini.
 
Back
Top Bottom