Arusha: Mawakili wameshaamua, bado kumchagua!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Nimeshafika Arusha. Kwenye Semina na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika almaarufu TLS. Kuna Semina na mada kadha wa kadha. Lakini kubwa ni uchaguzi wa Rais wa TLS kumrithi Wakili Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

Mawakili wa kutosha na kutisha wameshawasili Arusha. Wameshawachambua wagombea wa Urais wa TLS na kuamua. Wameamua kutoa chuma na kuweka chuma. Anatoka Lissu, anaingia anayefanana naye. Vijana wanajisemea 'weka, tuweke'.

Tunamtaka Rais wa TLS shupavu bila mabavu. Jasiri wa asili; mthubutu bila utukutu; shujaa asiye na mawaa na msemahoja bila vihoja. Tunamtaka Lissu mwingine. Akisema tumsikilize; akilia atulize; akitamka tuwe tunaamka. Tunamtaka wa kukoromea uonevu.

Mawakili wameshaamua kwenda na Wakili Fatma Amani Abeid Karume. Bado kumchagua tu. Wanampenda, wanamwamini, wanamjali na wako pamoja naye. TLS,imara wakati wote.

Nyaraka za TEC na KKKT zijibiwe badala ya kukejeliwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha kwenye mkutano wa TLS)
 
IMG-20180327-WA0002.jpeg
 
We kila pahala upo tu, we ni nani? Haya CAG yuko huku Dodoma anawasilisha taarifa yake leo vipi utakuja?
 
Back
Top Bottom