Arusha: Mahakama yatupilia mbali rufaa ya mawakili wa serikali kwenye kesi ya Lema

Haki haiombwi, inapiganiwa! Hongera Lema na timu yako. Soon Tanzania tutakuwa TLS inayojitambua na imara...! Mungu ibariki Tanzania na Watanzania...!
 
Ndio unavyojidanganya. Tayari mahakama imeona ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imemwonea Lema. Maana yake Lema akitoka atakuwa mara kumi ya alivyokuwa. Majaji wanashangaa jinsi serikali ilivyonajisi taalum ya sheria.
Kwa hukumu hii serikali haitapata tena fursa ya kumweka mtu ndani bila ya dhamana kwa kuonea.
Sipo CHADEMA, huenda sikubaliani na aliyosema

Kamanda kesi ya msingi haijamalizika...hapo ilikuwa ni rufaa tu
 
ukitoka utie adabu kipindi hiki sio cha jk, la sivyo utaozea jela. acha kuropoka
Akili zako sina uhakika kama zina akili. Badala ya kumlaumu huyo mwenye amri ya kutoka juu unamlaumu Lema.Do you think you are safe? Subiri hiyo amri kutoka juu itakavyokushughulikia wewe au mjomba wako ndipo utakapojua madhara ya kutumia vibaya mamlaka
 
Siku ya sheria nilimwona mkuu akiongea nikafikiri sana! Anapata wapi ujasiri wa kutoa maagizo kwa mahatma wakati serikali imeoza?????
 
Kwa nini akae jela miezi mitatu mbunge wa kuchaguliwa? Ni mini alichptaka kuwasaidia wapiga kura wake hasa? Kero zao walimtuma mojawapo ilikuwa ni kumtukana Rais? Haya, tayari keshamtukana Rais, je imemaliza njaa ya wapiga kura? Imejenga zahanati? Imeongeza chakula? Ningeshauri akitoka jela akae na wapiga kura wake awaombe msamaha, la sivyo hiyo miezo 4 jela kawaibia muda wao. Mbunge alitakiwa awe kazini akiwatumikia lakini yeye akachagua amtukane
Rais. WM

We zuzu alimtukana nini rais? Au hujui tusi ni kitu gani?
 
Sasa tunaanza kuiona nyota ya jaha kwa umbali, muda simrefu Lema utakuwa nasi tena kitaaa, nyota yako imeng'ara zaidi tangu uonevu huu ulipokupata, itakuwa shangwe bin raha siku ikifika, naikumbuka sana ile siku mwaka 1990 shujaa Nelson Mandela alipotembea mtaani akiwa huru baada ya miaka 27!
 
ukitoka utie adabu kipindi hiki sio cha jk, la sivyo utaozea jela. acha kuropoka
chunga mdomo unaongea kama vile unajua kwanini mh lema yupo ndani hadi leo ,nchi inaendeshwa kwa utawala wa sheria si kauli za ajabu ajabu waache majaji wafanye kazi zao.mwenzako akinyolewa na wewe tia maji.
 
Hawa mawakili wenu wana akili timamu?
Majaji wamesema wamesoma mapingamizi ya mawakili wa serikali bila kuona tija yeyote ya kisheria kwaiyo inatoa oda kwa Mahakama kuu kulishughulikia swala la Godbless Jonathan Lema haraka sana.

Kwa uamuzi huu wa mahakama wa waheshimiwa majaji Lema anarudi tena Kisongo ili aanze taratibu za mahakama za chini ili wampe dhamana.
 
ukitoka utie adabu kipindi hiki sio cha jk, la sivyo utaozea jela. acha kuropoka
Umesema vema Jk aliheshimu utawala wa sheria na kutoa nafasi mihimili mikuu kufanya kazi kwa uhuru
Sasa ma jaji hawa wamechoka na dhuluma ilokua inaendelea kwa lema
Mahakama imegoma kutumika
Full stop
Uweledi na u kilaza haviishi nyumba moja
 
Lema akitoka awe na heshima na adabu kwa Rais wa nchi hii Rais anamuwakilisha Mungu kwenye kutawala Dunia .
Kwa hiyo mlimweka mahabusu ili awe na heshima na adabu? Ngoja tuone kama mtaheshimiwa zaidi ya kuumbuliwa! Tayari ya Bashite yako hadharani, mtaumbuka mmoja mmoja hadi mzikimbie ofisi nyie wenyewe!
 
ukitoka utie adabu kipindi hiki sio cha jk, la sivyo utaozea jela. acha kuropoka
Wakili gani Bomu huyo kibatala, badala ya kupambana kisheria na mawakili wenzake anamwaga chozi kupata huruma ya majaji, kwani DPP hapo analaumiwa kwa lipi Wakati upande wa utetezi ni Bomu, wacha anyee debe tena kdg akirudi atachunga domo huyo criminal.
 
Tunakupenda LEMA ila kesho ukitoka acha matusi wewe nikiongozi mkubwa hata kama kunajambo linakukera , Leo watu wanasema watakukumbuka wakati miezi 3 wameanza kukusahau hii nibongo haina shukurani care your family bro
Tusi lipi alitukana? Charge sheet imeeleza tusi gani mkuu?
 
We zuzu alimtukana nini rais? Au hujui tusi ni kitu gani?
Angemtukana rais angekua keshafungwa.
Demokrasia ni ghalama sana uliwa kiongozi kubali kusemwa.kudhalilishwa hata kutukanwa hutaki acha
Obama Trump Bush si tu walitukanwa walirushiwa vinyesi na bado maisha yakaendele.
So hizi ndo ghalama za demokrasia
Kinyume cha hapo ni kukubali u DIKTETA
 
Back
Top Bottom