Arusha: Mahakama yatupilia mbali rufaa ya mawakili wa serikali kwenye kesi ya Lema

ukitoka utie adabu kipindi hiki sio cha jk, la sivyo utaozea jela. acha kuropoka
NELSON MANDELA aliozea jela?alifungwa gerezani miaka mingapi?baadae alikuwa nani?nitajie jina moja yu nchi hii la mtu unaeweza kumfananisha na TATA MADIBA tofauti na baba wa taifa alietangulia mbele za haki.acha uoga haki haiombwi kwenye bakuli kama anavyoomba matonya.
 
Hawa mawakili wa serikali bana wanatia aibu sana. Wanahangaika na mtu asie na hatia wanawaacha IPTL iendelee kulitafuna Tanesco
 
Lema akitoka awe na heshima na adabu kwa Rais wa nchi hiiRais anamuwakilisha Mungu kwenye kutawala Dunia.

Aisee wewe ni 'mpumbavu'kweli kweli hata ukitwangwa kwenye kinu 'upumbavu' wako hautoisha,jinga kabisa wew mam ....ae zak..
 
Hujui kitu nonsense! Kwenye vitabu vya sheria vipi? Upuuzi kama huo hauingii kwenye law reports!

Hata isipoingia au kukubalika kisheria ,haya yalio fanywa kinyume kwa kumkomoa Mtu kwa sababu una mamlaka pia yatakurudia wewe au jamaa yako..
 
nadhan kuna haja sasa ya kubadil kifungu cha kinga ya rais ktk katiba mbov h il jamaa huyu akinyofoka na yeye ashughulikiwe kwa ku2mia madaraka vbaya tena afungwe kifungo cha maisha na kaz ngumu!
 
Majaji watatu kesho 8:00 Asubuhi (27/2/2017) watasikiliza rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Let us see what will happen!

=======
Lema akiingia Mahakamani leo

View attachment 474935

Update kuhusu kesi ya Mhe Lema.

Mahakama ya Rufani ya Tanzania (Luanda, Kipenka, Mugasha, JJA) iliyokaa Arusha leo 27th February 2017 imetupa Rufaa zote mbili zilizofunguliwa na Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusiana na dhamana ya Lema. Serikali ilikubali yenyewe kwamba Rufaa zote mbili hazina mashiko kisheria; kama tulivyokuwa tunasema siku zote tangu wakate Rufaa hizo.

Files sasa zitapelekwa Mahakama Kuu ili kuendelea na mambo yanayohusiana na dhamana.

Mahakama pia imezungumzia kwa masikitiko makubwa namna ambavyo Serikali imekuwa ikitumia case hii kama mbinu ya kutesa na kusumbua watu na imeshangazwa namna ofisi ya DPP ilivyoji-conduct. Imeshangazwa namna wanasheria wanavyoweza tia najisi fani kwa mbinu za ajabu ajabu mahakamani.

Imemkaripia sana DPP; in open court, too.

Kwetu sisi ni vindication kwamba we were always right. Always.

Soon safari hii itaisha.

Motto; if U know U are right, persevere and let all temporary things pass. U will eventually be vindicated.

Na Peter Kibatala (Wakili)

======

Majaji waicharukia serikali kesi ya Lema
MONDAY , 27TH FEB , 2017
Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumyima haki.

Lema%20mahakama.jpg

Lema akirudishwa gerezani (Picha: Maktaba)

Akizungumza Mahakamani hapo leo mbele ya majaji wenzake Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa, Luanda amesema haipendezi na haingii akilini mtu (Lema) kushikiliwa kwa miezi mine bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki.

“Tunaomba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikai (DPP) muwe makini sana maana mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua Mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushitua sana,” alisema huku akishauriana na wenzake mara kwa mara kwa masikitiko.

Aliendelea kusema kuwa ofisi ya DPP inaitia najisi taaluma hiyo, kitu kipo wazi ila wanafanya vitu vya ajabu na havipendezi.

Alihoji jaji Luanda kuwa “Tumesoma faili lote tunashangaa hivi kweli ofisi ya mwanasheria mkuu ina wanasheria kweli na kama wapo kwa nini huyu mtu (Lema) awe ndani mpaka leo?”.

Alisema kwa kuwa mikono yao kisheria imefungwa hawawezi kufanya chochote kwa leo na kuwataka Mawakili upande wa Lema kurudi Mahakama Kuu, kuendelea na maamuzi ya dhamana.

Lema-Arusha_0.jpg


Godbless Lema

Hali hiyo ilitokana na Wakili wa serikali Faraja Nchimbi kusimama mahakamani hapo na kuomba kuiondoa rufaa hiyo kwa madai kuwa ipo nje ya uwezo wake.

“Waheshimiwa Majaji baada ya timu yetu ya wanasheria kupitia kwa kina rufaa hii kwa sababu zisizozuilika tumeona hatupo tayari kuendelea na rufaa hii, maana hatukupeleka kusudio (Notisi) kwa msajili muda ulipita, hivyo tunaomba kuiondoa na uamuzi wa kuiondoa rufaa hii tumeufikia Ijumaa muda uliisha kuja mahakamani,”. Alisema Nchimbi.

Baada ya kuwasilisha ombi hilo, Wakili wa Lema Peter Kibatala, alisimama na kusema upande wao hawana pingamizi ila waliomba hoja za awali za rufaa hiyo ziondolewe Mahakamani hapo bila kunakiliwa.

Baada ya ombi hilo Jaji Kipenka Mussa alipokea kwa niaba ya Majaji wenzake na kukubali ombi la kuiondoa rufaa hiyo namba 9/2017.

Kibatala.jpg


Wakili Peter Kibatala

Aidha Jaji Luanda alimkaribisha jaji Stella Mugasha pia kuongea kwa niaba yao ambapo alisema mahakama imekubali ombi la pili la kuiondoa rufaa namba 10/2017, baada ya Wakili Paul Kadushi kuomba kuiondoa pia.

Wakili wa Lema Peter Kibatala, alilazimika kusimama tena Mahakamani hapo kusema kuwa upande wao unasikitika kuona ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP wanatumia Mahakama kwa njia ya kumnyima haki mteja wao, hivyo aliomba mahakama hiyo iwatatulie tatizo la kisheria lililojitokeza hadi mteja wao awe ndani hadi sasa.

Kibatala aliongea hayo huku akishindwa kujizuia na kumwaga chozi la huzuni mahakamani hapo mbele ya Majaji hao.

Chanzo: EATV
mwanasiasa ambaye hajafungwa jela kwasababu ya siasa ni mwanasiasa uchwara. Hata Nyerere, Mandela, Mugabe, Nkruma, Lumumba,...... waliwahi....Lema wanampolish azidi kung'ara kwenye jamii. Sasa hivi hata akigombea ubunge jimbo la Ilala anachaguliwa pia kama ilivyokuwa kwa Lyatonga.
 
Lema akitoka awe na heshima na adabu kwa Rais wa nchi hii Rais anamuwakilisha Mungu kwenye kutawala Dunia .
Acha upumbavu tena ukome kumlinganisha Rais wa nchi hii na Mungu hata rais mwenyewe akiliona bandiko lako atakukemea,Mungu si mwanadam hata aringanishwe na wanadam,nani kati ya wanadam anayeweza hata kujioteshea unywele mmoja juu ya kichwa chake? .Narudia tena Acha UPUMBAVUUUU
 
Acha upumbavu tena ukome kumlinganisha Rais wa nchi hii na Mungu hata rais mwenyewe akiliona bandiko lako atakukemea,Mungu si mwanadam hata aringanishwe na wanadam,nani kati ya wanadam anayeweza hata kujioteshea unywele mmoja juu ya kichwa chake? .Narudia tena Acha UPUMBAVUUUU
Kweli mkuu yaan fisiem hawajielew
 
Back
Top Bottom