Arusha: Maduka yote ya kubadilishia fedha za kigeni(Forex) yasimamiwa na JWTZ, wananchi watakiwa kwenda Benki Kuu

Una uhakika? Mbona Godbless Lema anaukosoa utendaji wa serikali na kumwa-attack directly Magufuli, lakini bado yuko na hajashtakiwa kwa hayo? Unapata wapi uoga wa kudhani ukiikosoa serikali utashtakiwa?

Lakini pia unaweza kupata wasiwasi ukiona waandishi wa habari wanapotea, wanasiasa wanapigwa risasi n.k.
 
Umaskini mbaya sana. Na ndio maana ukiwa masikin lazma uwe mchawi au roho ya kichawi
Hatua nzuri ya kupambana na wanaouza sarafu yetu kienyeji enyeji na kuifanya ikose uwiano sahihi.
Wasomali wengi wanadola wanazibeba kwenye mabegi yao wanayotoka nayo huko kwenye uharamia wa melini.
Lakini pia kuna watalii wenye fedha za magendo hivyo nchi inakosa vyanzo vya dola zinazoingizwa takwimu sahihi.
Nchi za wezentu ukienda kubadili fedha wanaomba kitambulisho chako kwanza.sisi tunachukua tu.
 
MONEY LAUNDERS WENGI WAMEKUWA WAKITUMIA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA KUTAKATISHA PESA ZAO NA WABADILISHAJI FEDHA WENGI HAWAFATI SHERIA KWA MFANO KUSCAN PASSPORT KWA KIASI KIKUBWA CHA PESA KUBADILISHA NA KADHALIKA SO SISHANGAI TATIZO SHERIA ZIKISIMAMIWA WATU WANAKUJA JUU NCHI GANI INAYOENDA BILA SHERIA.
 
Mtu kuwa tajiri si dhambi. Naelewa (na natarajia serikali ifanye hivyo) wezi wote wanapodhibitiwa maana ndio njia sahihi. Lakini si kila tajiri ni mwizi na si kila maskini ni mtenda haki.
Ulichoagiza kifanyike wiki chache hizi zilizopita (kukiwemo suala la korosho na maduka ya fedha za kigeni -na umeta-target Arusha pekee) ni counter productive. Huwezi kuwatajirisha maskini kwa kuwafukarisha matajiri kwa kuwa poverty is essentially a symptom of mindset. Kuna aina ya watu ukiwalipa mshahara mkubwa na kazi wataacha kufanya hadi waishiwe pesa.

Nakuomba kwa unyenyekevu mkubwa; acha private sector ifanye kazi bila kuingiliwa. Omba watu wakusaidie kuweka policies sahihi na more importantly acha mahakama ziwe truly independent. Otherwise tuendako siko.

Igagwa lelo!
 
umetumwa na mabeberu weweeee,tulia Jpm apige kazi,piga kaziii baaaaa,kandamiiiza baaaaaba,umewabatiza na moto ,mabeberu na vibaraka wao wanaungua,safi sana baba kanyaga twendeeeeee
 
Kutorosha pesa nje ya nchi ni haramu. Hilo la kwanza
mkuu unajua hii maada ni ya kiuchumi Zaidi ila wana jamvi wana comment kisiasa Zaidi, sijaona sehemu ametajwa kiongozi Fulani wa serikalini au raisi kwani hahusiki moja kwa moja, inabidi tujue kwanza madhara yanayoweza kutokea kama uchumi wa nchi unayumbishwa ndipo a commenrt, hivyo kama mtu anakubishia kwa nadharia za kisiasa wewe wala usimueleweshe kwani hatokuelewa hata...
 
Una uhakika? Mbona Godbless Lema anaukosoa utendaji wa serikali na kumwa-attack directly Magufuli, lakini bado yuko na hajashtakiwa kwa hayo? Unapata wapi uoga wa kudhani ukiikosoa serikali utashtakiwa?
Wanamgwaya Lema wewe
 
Wanamgwaya Lema wewe
Hukosi kisingizio. Toka lini serikali ikamgwaya Lema? Huyo Lema mara ngapi amesha wekwa kizimbani? Toka enzi za Rais Kikwete alikiwa amesha pigwa pingu na kunyea debe.

Tafuta kisingizio kingine please?
 
Lakini pia unaweza kupata wasiwasi ukiona waandishi wa habari wanapotea, wanasiasa wanapigwa risasi n.k.
Lissu alistahili kuuawa aidha na serikali au wananchi. Lissu ni saliti mkubwa sana wa maisha ya watanzania.

Wewe fikiria mwenyewe mit ambaye ndugu zake wote kuanzia wazazi wake, kaka na dada zake na watoto na mke wake wapo nchini, lakini yeye anathubutu kushirikiana na makampuni ya kigeni kuishtaki nchi yake kana kwamba yeye hausiki na maendeleo ya nchi yake.

Zaidi ya hayo Lissu ana yashawishi mataifa ya kigeni yasiisaidie Serikali ya Magufuli kwa kuhofia kuwa ikaleta maendeleo ya wananchi wake. Yeye anataka watanzania waendelee kuwa masikini na watu tusio jiweza maadam yeye yuko madarakani. Hajui kuzuiwa kwa misaada sisi wanyonge ndiyo ambao tutaathirika na sio Magufuli.

Snowden yuko Russia amefichwa na Puttin. Hawezi kwenda Amerika. Akirudi huko kifungo cha maisha au kifo kina msubiri, sembuse Lissu?
 
Hukosi kisingizio. Toka lini serikali ikamgwaya Lema? Huyo Lema mara ngapi amesha wekwa kizimbani? Toka enzi za Rais Kikwete alikiwa amesha pigwa pingu na kunyea debe.

Tafuta kisingizio kingine please?
Utaishia kusema hayo. Kwani anafanyiwa hivyo kihalali? Ni serikali au utawala wa kijinga unaotumia mabavu kuwatisha raia wake ili waiogope badala ya kuheshimika. Ni dhahiri anaelazimisha watu wamtii kimabavu nimuoga hastahili heshima yoyote.
 
Lissu alistahili kuuawa aidha na serikali au wananchi. Lissu ni saliti mkubwa sana wa maisha ya watanzania.

Wewe fikiria mwenyewe mit ambaye ndugu zake wote kuanzia wazazi wake, kaka na dada zake na watoto na mke wake wapo nchini, lakini yeye anathubutu kushirikiana na makampuni ya kigeni kuishtaki nchi yake kana kwamba yeye hausiki na maendeleo ya nchi yake.

Zaidi ya hayo Lissu ana yashawishi mataifa ya kigeni yasiisaidie Serikali ya Magufuli kwa kuhofia kuwa ikaleta maendeleo ya wananchi wake. Yeye anataka watanzania waendelee kuwa masikini na watu tusio jiweza maadam yeye yuko madarakani. Hajui kuzuiwa kwa misaada sisi wanyonge ndiyo ambao tutaathirika na sio Magufuli.

Snowden yuko Russia amefichwa na Puttin. Hawezi kwenda Amerika. Akirudi huko kifungo cha maisha au kifo kina msubiri, sembuse Lissu?

Kama Tundu Lissu alivunja sheria basi angetakiwa ahukumiwe kwa kufuata sheria. Tofauti ni kwamba Edward Snowden anatakiwa Marekani na serikali ya Marekani imeweka bayana makosa yake. Serikali ya Tanzania iliweka wazi makosa ya Lissu?

Unajuwa tatizo kama rais anakuwa na nguvu ya kumuadhibu mtu kwa kutumia chombo cha usalama wa taifa ni hatari sana. Anaweza hata kutumia chombo hicho kwa kulipiza kisasi kwa mambo yake binafsi. Kama mtu kafanya kosa kwanini mambo yasiwekwe wazi na kuacha sheria kufuata mkondo wake.
 
halafu watamchagua
Arusha inaweza kuwa ni kitovu cha utakatishaji fedha chafu....kupitia wanaojiita wafadhili ,wafanyabiashara wakubwa n.k
Magufuli kaja kuwanyoosha.
Kura zake atazipata nyingi na syndicate za watakatishaji zitaangamizwa
 
uongo utakusaidia nini ? kauli duni kama hizi ndio zimesababisha Magufuli aangukie pua uchaguzi huu
 
Back
Top Bottom