ARUSHA: Lowassa kumtembelea Lema gerezani Kisongo

ARUSHA: Lowassa kumtembelea Lema gerezani Kisongo

TAARIFA-CHADEMA KANDA YA KASKAZINI

Waziri mkuu mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu Chadema Taifa, Edward Lowassa pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye wataongozana na Katibu wa kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa na Madiwani wa Jiji la Arusha wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro siku ya kesho watamtembelea Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema katika Gereza la Kisongo .
Yaani mpaka leo hajaenda!kweli Wana siasa wanapendana sana,kama wanavyotupenda sisi mashabiki wao.
 
TAARIFA-CHADEMA KANDA YA KASKAZINI

Waziri mkuu mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu Chadema Taifa, Edward Lowassa pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye wataongozana na Katibu wa kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa na Madiwani wa Jiji la Arusha wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro siku ya kesho watamtembelea Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema katika Gereza la Kisongo .
Lazima mzee amesikitika sana,yaani yeye na ufisadi wote haja wahi kukaa magereza, na lema yuko ndani kwa kuota,Tuna mwombea mungu akitoka aache kuota,aje afanye kazi wananchi waliomtuma.
 
Nyie wanasiasa mnafurahisha sana, hivi Lowasa asingekatwa akahamia CDM mngemtetea kama hivi mnavyomtetea sasa hivi kwa nguvu zote? au ndio mnafuata upepo tu.
Labda uulizwe wewe kuwa asingekatwa ungekuwa unanuandama hivi?
 
Chadema unafiki wao ni kiwango cha Uprofesa.......... Wanachokihubiri sicho wanachokitenda ......
Kuna mnafiki nchi hii kama boss wetu? Anasema atapambana na mafisadi lkn kumbe anapambana na maskini tu
 
Waarabu walipasua mimba za mama zenu na wakawahubiria injili ya dini mkaikubali.... Wazungu waliwapiga mijeledi...walipora rasilimali zenu na kuwaita nyani bado mliipokea injili yao ya Yesu.... Bado mnapata misaada yao na kuishi katika utamaduni wao...

Hata sauli baada ya kuua sana baadae alihubiri injili na walioteswa naye wakaipokea!!
Daaah hapa umepiga utosini kabisa mkuu
 
Nyie wanasiasa mnafurahisha sana, hivi Lowasa asingekatwa akahamia CDM mngemtetea kama hivi mnavyomtetea sasa hivi kwa nguvu zote? au ndio mnafuata upepo tu.
Jaribu kutumia ubongo kidogo . Hivi leo Messi akihama kutoka Barcelona na kuja Real Madrid akawa anafunga magoli tusimshangalie.?
 
Wote hao?? Au watafanya na mkutano wa kanda?
 
Labda watatafuta suluhu na kumaliza tofauti zao, yaani kati ya Lema na fisadi Lowasa!

'Ni heshma kubwa Mbele ya Mungu kumzomea Fisadi Lowassa.
Huyu Mzee ni Mnafiki sana.
Kuanzia Leo sio Waziri Mkuu Mstaafu ni Waziri Mkuu alieshinikizwa kujiuzulu kwa tuhuma za Rushwa...'- Kamanda Godbless Lema ( MB)

Kweli aijuae Future ( Ghaib) ni Allah pekee!
 
Labda uulizwe wewe kuwa asingekatwa ungekuwa unanuandama hivi?
Asingekatwa yeye nani? Eti hakuna mwenye ubavu wa kumkata!!Thubutu CCM inaongozwa na msingi! Hufai hufai tu hakuna kuonewa Huruma! Aachwe Makamu wa Rais na Waziri Mkuu aliyeko madarakani sembuse yeye!!!
 
Waarabu walipasua mimba za mama zenu na wakawahubiria injili ya dini mkaikubali.... Wazungu waliwapiga mijeledi...walipora rasilimali zenu na kuwaita nyani bado mliipokea injili yao ya Yesu.... Bado mnapata misaada yao na kuishi katika utamaduni wao...

Hata sauli baada ya kuua sana baadae alihubiri injili na walioteswa naye wakaipokea!!
Mkuu umefikilia mbali sana aiseee
 
Mimi sizungumzii jamaa yetu ama siyo yetu.
Nazungumzia UJANJA wa kisiasa . Kama ungekuwa unajua POLITICAL SCIENCE ungenielewa
Lakini kama wewe ni shabiki tu.
HUTANIELEWA!
Mkuu usiumize kichwa buku 7 hawawez kukuelewa
 
da nimefikiria mbali sana sikutegemea kama kuna siku lema , atakuja kukaa meza moja na lowasa
Hahahahaja ni aibu kwa Lema. Lakini hakuna jinsi, analinda mkate wake wa kila siku. Hii ndio siasa mzee.
 
Uzi umeshambuliwa na viwavi Wa kijani
Sio kijani pekeyake. Hata sisi wa nyeupee.ukweli ni ukweli tu usiuonee haya hata kidogo. Matamshi ya Lema yalitoka rohoni na ni ukweli. Na hajawahi kuyafuta kwa namna yoyote ile
 
Back
Top Bottom