Achana na mambo ambayo yako mahakamani. Huwezi kutabiri kitakachotokea. Anaweza kulambwa kifungo cha miezi 6 au zaidi na hivyo kumuondolea sifa ya kuwa mbunge kwa miaka 10. Tuache sheria ichukue mkondo wake. Tuache viherehere.Mbunge wa Arusha Mjini, aliyepo mahabusu, Godbless Jonathan Lema (CHADEMA), amewapa kilema wanaArusha. WanaArusha hawa si wale wa miaka ile. Hawa wanajadili mambo kwa uwazi, ujasiri, umakini, utulivu na umoja.
Nipo hapa Arusha karibu juma moja sasa. Nilikuja hapa kujiridhisha na kuthibitisha kuhusu nilichoripoti nikiwa Dar es Salaam kuhusu Lema kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Ubunge akiwa Mahabusu.Nilisema hivi:Arusha: Lema 'aendelea kuongoza' akiwa mahabusu
Nimejiridhisha vya kutisha na kutosha kuwa Lema anaiongoza Arusha na kuaminika,kukubalika na bado 'yupo' na wanaArusha wake. Anasifiwa zaidi ya kukandiwa; anasemwa vyema kuliko kukosolewa. Anaonwa kama 'Baba wa Nuru' ya kifikra Arusha.
Kwa mara nyingine, nimemtembelea Lema. Yuko 'gado' na mwenye ari kubwa. Anasubiri hatma yake tamu ya kisheria kuhusu yanayomkabili. Hajutii kuwa katika hali aliyopo kwa 'kukisimamia' anachokiamini.
Arusha yang'ara, Arusha yasonga mbele na Lema wake.
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
Mambo haya ndio alikataa Baba wa Taifa wakati ule Mh. Mrema alipokuwa analipuwa mabomu. Akamwambia Rais "Muacheni hata wakitaka kumbeba, kwani mkimkamata mtampa umaarufu wa kisiasa..."
Mzee yule alikuwa na hekima sana huenda kama za mfalme Suleiman. leo ni kweli yanatokea...... Mwl. Nyerere bila shaka anastahili kwa kanisa Katoliki kumtangaza mwenyeherina hata Mtakatifu. Alikuwa na maono sana kama manabii ambao walikuwa wanaongeana Mwenyezi mungu.
Mkuu Rejea tu tukio la Geita kulikuwa na sababu ipi ya kuwapiga raia waliokuwa wanamsalimia Lowassa. Nchi imekuwa ni ya vitisho. Viongozi ni wavivu wa kufikiri ni aibu tupu wanachofanya.
Huu ni ushahidi tosha wa uelewa wakoAngalia utaolewa huko kwa ujinga wako wakuwafuata mabwana za watu Arusha
Lema kama Mandela au kama Martin Luther King jr
kwa kutuma text kwa simu ya Wife wanafanana sana