VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Mbunge wa Arusha Mjini, aliyepo mahabusu, Godbless Jonathan Lema (CHADEMA), amewapa kilema wanaArusha. WanaArusha hawa si wale wa miaka ile. Hawa wanajadili mambo kwa uwazi, ujasiri, umakini, utulivu na umoja.
Nipo hapa Arusha karibu juma moja sasa. Nilikuja hapa kujiridhisha na kuthibitisha kuhusu nilichoripoti nikiwa Dar es Salaam kuhusu Lema kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Ubunge akiwa Mahabusu.Nilisema hivi:Arusha: Lema 'aendelea kuongoza' akiwa mahabusu
Nimejiridhisha vya kutisha na kutosha kuwa Lema anaiongoza Arusha na kuaminika,kukubalika na bado 'yupo' na wanaArusha wake. Anasifiwa zaidi ya kukandiwa; anasemwa vyema kuliko kukosolewa. Anaonwa kama 'Baba wa Nuru' ya kifikra Arusha.
Kwa mara nyingine, nimemtembelea Lema. Yuko 'gado' na mwenye ari kubwa. Anasubiri hatma yake tamu ya kisheria kuhusu yanayomkabili. Hajutii kuwa katika hali aliyopo kwa 'kukisimamia' anachokiamini.
Arusha yang'ara, Arusha yasonga mbele na Lema wake.
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)