GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
Utapeli hata huko nchi zilizo endelea upo ndugu yangu.We unasema Arusha. Nchi imekwisha hii, kila kona ukienda watua ni wakali kweli. Hali ni mbaya kweli kweli. Utapeli umezidi, yaani nashukuru tu kuna amani.
Sio watu hawana hela, sema wewe huna hela.Maisha ni magumu, watu hawana fedha. Ni tatizo la uchumi wa nchi. Nahisi wewe unataka kuunganisha Arusha na siasa za CDM. Mtwara kuna maisha mazuri? Kuna biashara nzuri toka asubuhi hadi usiku?
Watajuta kwanini walimchagua yule kichaa, sasa hawana hata wa kuwa wakilisha Bungeni
Acha ushamba mkuu si vyema kumwita mh. Mbunge G. Lema Kichaa. Je walikochagua wenye akili timamu hali za majimbo yao zikoje ukilinganisha na Arusha? Hivi huyu anayelalamika alitaka akipita mjini watu wamnunulie soda na chips ndo ajue hali ya Arusha ni nzuri? hli ya Arusha haina tofauti kiuchumi na mikoa mingine. Kigezo ambacho angekitumia ni kwenda TRA kuangalia kama mapato yameshuka kwa kiasi gani kutokana na watu kufunga biashara. Ujinga alioleta hapa hatujui unalengo gani kwani hata mikoa kama Mwanza, Morogororo na Dar hali sio nzuri je huko nako kuna Vichaa wabunge?
kuzorota kwa biashara ya Tanzanite kwa KIASI kikubwa imeathiri Hali ya uchumi katika jiji la Arusha, na hili limetokea baada ya mwekezaji..... Lakini pia utalii kwa Sasa sio kiviile na low season ndo hiyo inaishia na pia kukosekana kwa viwanda vingi IDADI Kubwa ya watu haina ajira.... Lingine pia ni Kuwa Sasa upatikanaji wa bidhaa umekua rahisi zaidi unamfikia Mtu hadi nyumbani so watu hawana time ya kwenda madukani mjini, tembelea katika viunga vya mji wa Arusha Kama kijenge zote Mwanama na ya juu, ngarenaro, sekei, ngulelo, kwa mrefu, sakina, kwa iddy, ilboru...... Kote huko Unakuta "Visuper Market" pamoja na vihardware, so tathimini yako ya kuangalia maduka ni irrelevant ingawa kiukweli uchumi wa Arusha umeshuka
Rekebisha kidogo hapo, ni Lema sio mheshimiwa mbunge. Halafu hivi wewe umeenda Mwanza hivi karibuni? Nakushauri uende ukaone biashara inavyo kwenda.
Nashukuru na nimeliona limeandikwa pia kwenye blog ya michuzi. Tuacheni utani na masihara mji wa Arusha kwa sasa una hali mbaya sana. Hali ya mji wa Arusha kiuchumi kwa sasa sio maridhawa kabisa. Nilijaribu kutembelea maeneo mengi ya kibiashara km sokoni ambapo kuna maduka mbali mbali . Ikifika saa 10 tu jioni wanaanza kufunga hakuna wateja, hata zile siku za kawaida za kazi. Biashara za taxi , ma-bus ndio usiseme, karibia 90% ni mbovu mbovu sana. Hali ya usafi wa mji ni mbaya sana. Kwa kweli , wana JF tuna haja yakuutizama upya mji huu, GENEVA OF AFRICA INAPOTEA KWENYE RAMANI