Arusha kumekucha

MODS

Hivi mtu akidanganya wazi kama NGONGO na MZEE2011 hawatakiwi kufungiwa?

Maana daladala zimegoma hapa Arusha, boda boda zinafanya kazi chache maeneo machache, Ni shida kweli ya usafiri hapa.

Hivi mkidanganya kuwa hawajagoma mnapata faida gani?

Duh! Nyani Ngabu alisemaga, MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!
 
Nawapa onyo hawa maaskari wanaopitapita wakiwa tayari kwa lolote,nawaambia ya kwmb NGUVU YA UMMA hawatazuilika hata kidogo mara itakapoanza. Wakaongeze silaha na mabomu nyingi.
 
Napata supu hapa naona daladal zinapita,tax na pikipiki kama kawaida wanapita! Chadema wangetoa fungu kwa kila daladala na tax ili jioni wapeleke hesabu kwa matajiri wao kama kawaida! Ni ngumu kufanyika afadhali wamiliki ndio wange sema wagome!
 
Uwezi kuwashikia watu wazima akili zao..

Wewe ukatae dhamana ambayo ni haki ya mshtakiwa halafu watu wagome.

Watu wamekopa benki, wamenunua daladala, pikipiki, waache kufanya kazi walipe mikopo yao eti wagome, hiyo mikopo watalipiwa na Lema?

Lema kaamua kwenda gerezani kwa mapenzi yake mwenyewe yoyote anampenda amfuate gerezani
 
Nipo maeneo ya ujenzi. Nimetokea mianzini hadi hapa. Hakuna vifodi vinavyofanya kazi na pale standi hakuna kifodi hata kimoja! Hadi nimefika hapa nimepishana na magari matatu ya ffu yakiwa na askari walio tayari kwa mapambano. Ninavyoona mm, hali si shwari na lolote linaweza kutokea!
 
usafiri ni wa kubahatsha chuga me mwenyewe nipo barabaran nasubiria usafiri nawaza kukodi tax
 
Katikati ya mji wa Arusha hakuna daladala hata mmoja! Mawe yanavurumishwa ile mbaya!
Kwa upande wa mbauda na majengo daladala zinaishia corner esso mjini hazifiki.
 
Huyu sijui vp!hapa nilipo napiyanga kwa miguu kwenda kazini coz hamna usafiri!we uko Arusha ipi!

Ukweli mgomo upo lakini kwa vile robo ya daladala ni za mapolisi, wao wanalazimisha magari yao yaendelee.
 

Uko mtaani wapi? hiyo thread ya jana kuhusu mgomo si uliianzisha wewe mwenyewe, sasa umeumbuka. Watanzania wanajua wanachokifanya. Hawawezi kupelekwa hovyo na wendawazimu. Hebu kamilisha ratiba manake posho yako uliopewa inaishia leo. Ukimaliza uibuke na lingine.

Hakuna mtanzania ndugu yangu wa kupoteza muda wake eti kushinikiza Lema atoke gerezani who is LEMA? si ameamua kutembelea vidume vya huko , ngoja aipate fresh, mtoto akililia wembe mpe.

Mpaka aombe mwenyewe kutoka si aliomba mwenyewe kwenda.
 

Thanks, pls endeleea kutapa taarifa zaidi!!
 
Unaweza ukawa karibu na ukweli lakini kusema hakuna daladala hata moja huo ni uzandiki.Naelewa kuna shinikizo la wapiga debe na wahuni wasiojua wenye daladala wengine wana mikopo bank,wanasomesha watoto vyuoni na nk kuwanyima fursa ya kufanyakazi kwasababu zisizo na mashiko tena za kisiasa ni kitanzi cha kujitakia.

Katikati ya mji wa Arusha hakuna daladala hata mmoja! Mawe yanavurumishwa ile mbaya!
Kwa upande wa mbauda na majengo daladala zinaishia corner esso mjini hazifiki.
 

Labda unazungumzia Arusha ya kufikirika ninakwambia daladala zinapiga mzigo kama kawaida.



Hii ndiyo hoja ya madereva wengi wa daladala.



Mkuu naona umeamua tu hivyo kwakuwa humkubali Lema from the begining!
Mimi nimetoka mianzini hadi ujenzi na miguu kwa kukosa usafiri. Hapo stand ya vifodi, hakuna haice hata moja. Au upo Nduruma!?
 
Mkuu FairPlayer.

Ebu niambie uko maeneo gani unawezakuta uko Kiding'aa mimi niko maeneo ya Golden Rose muda huu daladala zinapiga mzigo kama kawaida.

mkuu mgomo upo na hasa kwasasa ndiyo unazidi kupamba moto ila asubuhi walikuwa wamegawanyika..
 
Hali si shwari kabisa AR,joto la vurugu linazidi kupanda.. Maelfu ya vijana wanajipanga kulazimisha wawekwe mahabusu
 

Labda unazungumzia Arusha ya kufikirika ninakwambia daladala zinapiga mzigo kama kawaida.



Hii ndiyo hoja ya madereva wengi wa daladala.

Acha uwongo ww,mi niko apa stand ya vfod hamna gari inayopga kazi,labda uniambie aya mapra ya police
 
Wana JF huku Arusha hali ni tete baada ya madereva wa vifodi kugoma wakishinikiza mbunge wao aachiliwe huru na OCD Ars ahamishwe. Askari mmoja wa FFU kapigwa kajeruhiwa vibaya mno kwenye purukushani. Kituo cha vifodi kiko kitupu na barabarani hakuna kifodi hata kimoja, peoles are matching to and fro different areas.
NAWASILISHA
 
Wana jamvi sisi wengine hatupo Arusha lakini tumesikia through sms kwenye kipindi cha Power Breakfast kuna mdau mmoja kutoka Arusha alituma sms akitaarifu ya kwamba usafiri ni shida ndani ya Arusha coz kuna mgomo wa vifod na Hando akaelezea kwamba vifod ni daladala sasa hapo changanya na za kwako!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…