Huu hapa chini uthibitisho kutoka kwa Katibu Mkoa CCM Mary Chatanda
Kauli ya Chatanda
Akizungumzia madai hayo, Chatanda alikanusha akisema amekuwa akifuata taratibu zote katika utendaji wake na kuongeza kwamba amekodisha Kituo cha Mabasi cha CCM kwa kampuni ya Mtei baada ya aliyekuwa amepangisha, Kampuni ya Scandinavia kushindwa kulipa.
Chatanda pia alikanusha tuhuma za kumnyanyasa mwenyekiti huyo kwa kumnyima gari akisema kila wanapoitisha vikao amekuwa akimtumia gari nyumbani kwake Longido ili limlete Arusha Mjini na kumrejesha baada ya vikao.
Hata hivyo, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaCCM kwamba vituo vyote vya mabasi vinavyomilikiwa na CCM kukodishwa kampuni moja pekee ya Mtei katika mazingira yasiyo na uwazi.
CCM Arusha imekuwa katika mgogoro wa muda mrefu tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, ambao ulikifanya hadi kupoteza Jimbo la Arusha Mjini ambalo liliangukia mikononi mwa Chadema.
Mgogoro huo wa CCM, pia umekuwa ukitikisa UVCCM hatua ambayo hivi karibuni, ilimfanya mlezi wa chama hicho mkoa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya chama hicho Taifa, Stephen Wassira kufanya ziara mkoani humo kwa ajili ya usuluhishi.
Wakati huo huo, Kikao cha Halmashauri ya CCM Mkoa wa Arusha ambacho kilipangwa kufanyika leo, kimeahirishwa hadi Januari 11 mwakani ili kutoa nafasi kwa wajumbe wote kushiriki.Habari zilizothibitishwa na Katibu wa Mkoa wa Itikadi na Uenezi, Loota Sanare zimesema kuahirishwa kwa kikao hicho kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu, kunatokana na baadhi ya wajumbe kushindwa kuhudhuria.
Ni kweli kikao cha halmashauri kuu kimeahirishwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo hilo la baadhi ya wajumbe kutokuwapo na hivyo, tumeona ni vyema kusogeza mbele ili wote wafike, alisema Sanare.
Soma Mwananchi