Arusha: Kituo cha mabasi ni mali ya chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha: Kituo cha mabasi ni mali ya chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngoiva Lewanga, Dec 29, 2011.

 1. N

  Ngoiva Lewanga Senior Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika jiji la Arusha, kituo kikuu cha mabasi kinamilikiwa na chama cha mapinduzi(ccm) na wala sio chini ya jiji. Je wana wa Arusha hili mnalitambua?
  Katika hali ya kustaajabisha, kituo hicho hukarabatiwa kwa gharama za jiji la Arusha.
   
 2. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Leta source.
   
 3. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii ni mpya ndiyo maana ukiangalia hicho kituo cha mabasi ARS kimekaa kiccm ccm. Hakuna vyoo vya kuamini, kila mahali pananuka mikojo, hakuna mapipa ya kuwekea takataka, ccm kweli ni kirusi kisichopenda maendeleo. Mungu tunakuomba utuondolee hichi kirusi kinachoitwa ccm ili taifa letu lipone!!!
   
 4. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Niliisoma hii jana, sikuamini macho yangu.

  Nashangaa kwa nini mji wa Arusha haimiliki hiki kituo cha mabasi na vinginevyo kama vipo. Kama wamiliki wa haya mabasi wanalipa kodi, ina maana hii hela inaenda CCM? Je wafanyakazi wa manispaa wanalipwa na nani? CCM au Manispaa?
   
 5. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Ukitokea Shekh Amri Abeid Stadium kuna vyoo hapa Mahoo Hair Cutting Salon. Mbele yake kuna Michomoko ya kwenda Namanga.
  Hii taarifa ya kuwa kinamilikiwa na CCM sikuijua ngoja nifuatilie.
   
 6. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asije akachanganya kituo ch mabasi ya Mtei na stendi kuu.Naomba aweke habari ama hoja yake vizuri.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Huu hapa chini uthibitisho kutoka kwa Katibu Mkoa CCM Mary Chatanda

  Kauli ya Chatanda

  Akizungumzia madai hayo, Chatanda alikanusha akisema amekuwa akifuata taratibu zote katika utendaji wake na kuongeza kwamba amekodisha
  Kituo cha Mabasi cha CCM kwa kampuni ya Mtei baada ya aliyekuwa amepangisha, Kampuni ya Scandinavia kushindwa kulipa.

  Chatanda pia alikanusha tuhuma za kumnyanyasa mwenyekiti huyo kwa kumnyima gari akisema kila wanapoitisha vikao amekuwa akimtumia gari nyumbani kwake Longido ili limlete Arusha Mjini na kumrejesha baada ya vikao.

  Hata hivyo,
  kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaCCM kwamba vituo vyote vya mabasi vinavyomilikiwa na CCM kukodishwa kampuni moja pekee ya Mtei katika mazingira yasiyo na uwazi.

  CCM Arusha imekuwa katika mgogoro wa muda mrefu tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, ambao ulikifanya hadi kupoteza Jimbo la Arusha Mjini ambalo liliangukia mikononi mwa Chadema.

  Mgogoro huo wa CCM, pia umekuwa ukitikisa UVCCM hatua ambayo hivi karibuni, ilimfanya mlezi wa chama hicho mkoa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya chama hicho Taifa, Stephen Wassira kufanya ziara mkoani humo kwa ajili ya usuluhishi.

  Wakati huo huo, Kikao cha Halmashauri ya CCM Mkoa wa Arusha ambacho kilipangwa kufanyika leo, kimeahirishwa hadi Januari 11 mwakani ili kutoa nafasi kwa wajumbe wote kushiriki.Habari zilizothibitishwa na Katibu wa Mkoa wa Itikadi na Uenezi, Loota Sanare zimesema kuahirishwa kwa kikao hicho kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu, kunatokana na baadhi ya wajumbe kushindwa kuhudhuria.

  “Ni kweli kikao cha halmashauri kuu kimeahirishwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo hilo la baadhi ya wajumbe kutokuwapo na hivyo, tumeona ni vyema kusogeza mbele ili wote wafike,” alisema Sanare.

  Soma Mwananchi
   
 8. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  mnashangaa nini? kwani hiyo manispaa nayo si ccm tu,

  stand ya mabasi ya mikoani arusha ni ya ccm,
  wanja wa mpira wa arusha ni wa ccm,
  eneo lote kuanzia ccm mkoa mpaka mkombozi diary ni la ccm.
  eneo lote la soko la kaloleni na vibanda vyote vya maduka ni mali ya ccm.
  eneo lote la ccm wilaya mpaka soko la vijago ( karibu na fire brigade office) ni mali ya ccm.
  eneo katika ya petrol station ya mountmeru na TFA shopping center ( lilipo duka la brand house) ni mali ya ccm.

  bado sehemu nyingine nyingi tu.
   
 9. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sasa nimeelewa ni kwa nini wameng'ang'ania umeya kwa nguvu zote pamoja na kumwaga damu ya raia wasio na hatia
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndo maana hawataki kuachia umeya kwa garama yoyote either kwa hela ama kwakumwagika damu
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unataka kuniambia ccm ni kirusi hatari zaidi ya ukimwi, TB, Malaria, Kansa na vinginevyo vilivyo hatari? Ndani ya Tz?
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Itakuwa manispaa
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Lisemwalo lipo na kama halipo lajongea
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukisema vyote hivyo ni vya ccm unakosea unatakiwa kusema ccm wamejibinafsia
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli palipo na ccm hapaendelei hata njia yoyote, uchafu ni wao wizi ni wao uporaji wa rasilimali za uma ni wao,ukandamizaji ni wao na kila aina ya ubaya ni wao. Je kwa hali hii Tz tutafika?
   
 16. k

  kada1 Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mtajiju!!! Utawajua tu kazi kubeza kila kitu hata kama ni kizuri. Nyie mnaolipwa na Mbowe kuja kuiponda CCM hamna sera. Endeleeni na kazi yenu mwona kama inalipa!!!
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Si Arusha peke yake, CCM wamejimilikisha mali na rasilimali sehemu nyingi nchini... sehemu nyingi viwanja vingi vya michezo ni vya CCM na maeneo mengi ya wazi ni ya chama hicho
   
 18. B

  Baba Ipyana Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nafikiri ukisoma vizuri taarifa ya Chatanda ni kwamba wamekodisha kituo cha mabasi cha ccm kwa kampuni ya Mtei. Kituo hiki sio stendi kuu ya mabasi Arusha. ni kituo kinachojitegemea jirani na soko la kilombero. Kabla ya hapo kituo hiki kilitumika na mabasi ya scandinavia. naomba utoe maelezo sahihi usiwachanganye wana JF. Nadhani stendi kuu inaendelea kumilikiwa na Manispaa. Tafuta ukweli ujue kama sehemu yanapoegeshwa mabasi ya Mtei ni stendi kuu au la.
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tatizo ni kutokana na kuwa na chama kimoja ndio taaba yake hiyo mbona karibu viwanja vyote vya mpira ni mali yao..

  RIP TZ
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Siku nchi hii ikirudi mikononi mwa wenye nchi, hivyo vyote vitarudi serikalini kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote. Vitega uchumi vingi walivyopora ccm na kujimilikisha vilichangiwa nguvu na wananchi wote bila kujali kwamba ni wanachama wa ccm ama sio wanachama, sasa leo hii ccm wamejitwalia tu na kuvuna pesa wasizostahili, ingawa pia hawana uwezo wa kuvi maintain. Litawakumba kama ilivyotokea kwa KANU hapo nchi jirani Kenya, majengo na viwanja vyote walivyokuwa wamejitwalia vilirudishwa mikononi mwa wananchi hivyo kumilikiwa na serikali.

  Jambo la muhimu kwa sasa ni kufuatilia kama kweli kuna ushahidi wa fedha za halmashauri kutumika kukarabati miundombinu ya ccm, hapo lazima wananchi wa arusha msikubali hata kidogo kukosa huduma zenu za maendeleo, watendaji wa halmashauri wanapeleka fedha kuijenga ccm.

  Ni vizuri na mikoa mingine kufanyike uchunguzi wa kina, isijekuwa huo ndio utaratibu unaofanyika kila mahali ccm walipojitwalia viwanja vya michezo, stand pamoja na vitega uchumi mbalimbali.
   
Loading...