GE2025 Samia: Tutajenga SGR kuanzia Tanga - Arusha -Musoma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,714
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuunda serikali, ataweka kipaumbele katika ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kwenye ukanda wa kaskazini kuanzia Tanga, Arusha hadi Musoma.

Akihutubia wananchi jijini Arusha leo, Dkt. Samia amesema reli hiyo inalenga kurahisisha usafiri wa watu na usafirishaji wa bidhaa, jambo litakaloongeza ufanisi wa biashara na kuchochea maendeleo ya kanda hiyo.

Amebainisha kuwa kituo kikubwa cha reli hiyo kitapangwa kujengwa jijini Arusha, hatua ambayo itakuwa chachu ya ajira na fursa mpya kwa wafanyabiashara na vijana wa jiji hilo.

“Kuelekea mwaka 2030, ukanda huu wa kaskazini kuanzia Tanga, Arusha hadi Musoma tutajenga reli ya kisasa ya SGR, kwa sababu ya kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na watu. Lakini kwa sababu Arusha ni mji mkubwa, lazima kutakuwa na kituo kikubwa hapa, kituo ambacho kitaleta fursa zaidi za ajira kwa wafanyabiashara na vijana wetu,” amesema Dkt. Samia.

Kwa mujibu wake, mradi huo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha miundombinu ya nchi na kuongeza ushindani wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa
 
Pesa ya muhimbili hatuna kwasasa. Tatizo sio mipango au pesa ni ufisadi. Sasa mtoto wa best wake wa miaka 26 amewekewa bilioni 26 kwenye kwenye account yake moja Abdul na watoto wa Mama wameweka kiasi gani! IGP ana zaidi ya billion moja kwenye account yake kwa chini ya mwaka mmoja! hizo pesa zitatoka wapi.
 
Hiyo SGR tunajenga ss au wachina ?
Biashara Kwa vijana , uchuuzi na umachinga ?
Mungu nifundishe kunyamaza
 
Ni kurukaruka tu,kusaini mkataba kazi zinaanza kwa mbwembwe halafu hata 10% haifiki mkandarasi anapotea site pesa hamna!!

NB:Uvinza-Musongati iliyosainiwa juzi 300Km mkataba ni 72 months maana yake ataondoka madarakani na kuacha bado inajengwa,hakuna maana ya kuendelea kusaini ilhali lot 4,5,6 bado zinachechemea!
 
IMG-20251002-WA0029.jpg
 
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuunda serikali, ataweka kipaumbele katika ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kwenye ukanda wa kaskazini kuanzia Tanga, Arusha hadi Musoma.

Akihutubia wananchi jijini Arusha leo, Dkt. Samia amesema reli hiyo inalenga kurahisisha usafiri wa watu na usafirishaji wa bidhaa, jambo litakaloongeza ufanisi wa biashara na kuchochea maendeleo ya kanda hiyo.

Amebainisha kuwa kituo kikubwa cha reli hiyo kitapangwa kujengwa jijini Arusha, hatua ambayo itakuwa chachu ya ajira na fursa mpya kwa wafanyabiashara na vijana wa jiji hilo.

“Kuelekea mwaka 2030, ukanda huu wa kaskazini kuanzia Tanga, Arusha hadi Musoma tutajenga reli ya kisasa ya SGR, kwa sababu ya kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na watu. Lakini kwa sababu Arusha ni mji mkubwa, lazima kutakuwa na kituo kikubwa hapa, kituo ambacho kitaleta fursa zaidi za ajira kwa wafanyabiashara na vijana wetu,” amesema Dkt. Samia.

Kwa mujibu wake, mradi huo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha miundombinu ya nchi na kuongeza ushindani wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa
Muongo
 
Back
Top Bottom