Arusha imebadilika kabisa

Arusha imebadilika kabisa

Vijana wengi wa mjini kipato Chao Kinatokana na madini, wengine huchimba, wengine huuza na kununua nk. Nk
Ahahahaha! Arusha wameishaisha wachimba madini wamebaki wafanya shughuli zingine.
.
Nina uzoefu na uchimbaji wa dhahabu pamoja na uuzaji wake pesa ya madini kwa kijana huwa haionekani.
Hao vipato vyao vinapatikana kwa shughuli zingine wasikudanganye kupata hilo dini ni very very tough na misheria imezidi kuwa migumu.
 
rusha ni mji uliojaa wazungu kila Kona utafikiri tupo South Africa 🌍 na tushazoea kufanya biashara au mazungumzo ya hapa na pale na hawa wadoshi wakiwa hapa jijini.

Na wazungu wengi wao wamewekeza sana hapa. Asilimia kubwa sana ya wana Arusha pato Lao kubwa achia mbali madini la pili ni utalii.

Lakini kwa sasa hali ni tofauti kabisa urafikiri tupo singida au wap sijui hatuoni wazungu kabisa kabisa hata Ile migahawa wazungu hukaa hamna mtu mweupe hata kidogo.

Hotel, migahawa, na kule vinyagago na sehemu zote wazungu wanapopendelea kutembea au kukaa hamna kabisa watu weupe.

Makampuni mengi, migahawa, maduka na hata masoko wengi tunategemea utalii, sahiv kila mtu analia.
corona baba, tuwe wavumilivu hali ikitengemaa pesa za wazungu zitarudi kwa kishindo
 
Aisee ni kweli Chuga kumebalika sana! Saiv ata minadani hakuna pesa kabisa hasa kwa sisi wasaka tonge. Zaman tulizoea kuwauzia wanachuo lkn vyuo vyote vimefungwa!

Haya kuna watu walikuwa wanapanda milima kama Meru na Kilimanjaro wakirudi life linakuwa vzr lkn saiv hakuna hiyo kazi tena. Aisee asikwambie mtu cc tulikuja kusaka maisha hapa tunalia sana wakati mwingine ata pesa ya pango tunakoswa
Hata maofisini, hela ya chai imefutwa. Kunywa chai kwa mkeo!
 
Back
Top Bottom