DOKEZO Arusha: Hali halisi ya masoko yetu msimu wa mvua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Hapa ni soko kubwa la Kilombero lililopo jijini Arusha.

Miaka nenda rudi wafanyabiashara sokoni hapa hulipia ushuru kila siku, lakini ushuru huo hauwasaidii wafanyabiashara hao kwa kuwekewa miundombinu sahihi ya Soko wala mfumo mzuri wa Maji safi na taka.

Bali Mfanyabiashara ambae ni Mwananchi wa kawaida ameachwa ahangaike mwenyewe mahali hapo iwe mvua iwe jua ili mradi tu alipe ushuru.

Wafanyabiashara wa sokoni hapo wamesema kuwa msimu wa mvua kama hivi idadi ya wateja sokoni hupungua sana kutokana hali ya uchafu. Tope, na maji kutwama hivyo wateja hushindwa kuingia ndani ya Soko kupata mahitaji yao.

Ujenzi holela ndani ya Soko, wafanyabiashara wa sokoni hapo hujenga vibanda wenyewe kadiri ya uwezo wao,hivyo kutokuwa na mpangilio maalum wa soko.

IMG-20230421-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom