Arusha: Freeman Mbowe avishwa vazi rasmi la kimila la Wamasai na kusimikwa kuwa kiongozi wao

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,808
218,463
Kama tulivyoahidi kuwa nanyi bega kwa bega katika kipindi hiki ambacho Chadema imekuja na mkakati mpya wa OPERESHENI HAKI , basi leo tena Tunaendelea kuwapa uhondo na taarifa mbali mbali za yanayoendelea huko Arusha kwenye vikao vinavyoendelea.

Mpaka hivi ninavyoandika hapa tayari Mwamba Mbowe kishakabidhiwa uongozi wa Wamasai baada ya kuvishwa vazi rasmi la kimila na Wazee wa Arusha , Hii ni heshima kubwa kwake na kwa chama chake na ni pigo kwa mamluki wote waliotumika kummaliza bila mafanikio.

FB_IMG_1622025718056.jpg

FB_IMG_1622027752414.jpg
FB_IMG_1622027759778.jpg

Mungu ibariki Chadema .
 
Hii operation ikiendelea kwa muda wa miezi mitatu bila kusambaratika, basi mi nitatembea uchi nchi nzima. Hapa kuna mkakati wa mwenyekiti kupiga pesa bila kuwagawia wenzake kitu ambacho kitafanya wajumbe wengine ambao ni genge la mbeleji waisusie operation yenyewe. Time will tell
 
Umeishia darasa la ngapi ?
 
Hivi huu uongozi wa makabila, unakuwa je?
Maana hata akienda PM anavalishwa nae anakuwa kiongozi wao, lisu alivalishwa, mwenda zake alivalishwa.
Naomba ufafanuzi anaye fahamu
Mnyika yeye alivalishwa usukumani. Yaonekana wanapewa uongozi wa makabila watu wasiostahili kuwa wanasiasa. Hao hao kwenye boksi la kura wanalizwa!
 
Back
Top Bottom