Arusha bila Lema

Arusha bila Lema

Kwa hiyo mmemuweka JELA ili asigombee tena Ubunge
Mahakama ndiyo itaamua kama ana kosa au hana siwezi ongelea mambo yaliyoko mahakamani ushauri wangu kwa mbunge yeyote ni vizuri kujiepusha na mambo ya kuwafikisha mahakamani kwani huwezi jua mahakama itaamua nini
 
Mtu akifungwa au aliyewahi kufungwa sheria za Tanzania hazimruhusu kugombea hata ujumbe wa nyumba kumi hapo anakuwa kaaga vyeo vya kisiasa vyote.

Usichanganye na mambo ya siasa za Afrika ya Kusini ambapo Mandela alipotoka jela aliruhusiwa kugombea. Lema mwambieni kama anatafuta umandela kupitia jela imekula kwake. Sheria za Tanzania tofauti na za Afrika ya Kusini .Kama ana mshauri koko kampotosha mwanasiasa wa Tanzania kwenda jela ni kujiua kisiasa si kujijenga kisiasa. Tatizo CHADEMA hawana washauri wazuri wa siasa, wana wahuni wa kisiasa.
Nani kawaambia Lema kafungwa hukumu imetoka lini ya kifungo na kifungo ni cha nini ndoto au? Kifungo ni cha muda gani??
 
unafaidi nini binadamu mwenzio akifungwa?
Kwani wewe unafaidi nini Sisi tukikosa maji na dawa, nk.... Apambanie hayo hatukumtuma atangaze ndoto zake za kijinga
 
Mandela alifungwa miaka mingi lakini alitoka Lema ni Arusha na Arusha ni Lema
 
Mandela alifungwa miaka mingi lakini alitoka Lema ni Arusha na Arusha ni Lema
Lema hatukumtuma atangaze ndoto zake, hata Sisi huwa tunaota ndoto kama hizo pengine ila hatujawahi kutangaza hadharani, huwa tunahadithia watu wa karibu yetu kama mke nk... Huwezi kwenda kwenye media.
Hapa Lema anatafuta huruma ya kisiasa ( political sympathy)
 
Kama alishindwa kuwaletea maendeleo kipindi cha jk kama alivyofanya Joshua nasari zaidi ya vurugu tu basi awamu hii hataweza tena..
 
Kwani wewe unafaidi nini Sisi tukikosa maji na dawa, nk.... Apambanie hayo hatukumtuma atangaze ndoto zake za kijinga
kwahiyo akikaa mtaaani ndio anakukosesha maji na dawa na akifungwa ndio unavipata?
 
Mtu akifungwa au aliyewahi kufungwa sheria za Tanzania hazimruhusu kugombea hata ujumbe wa nyumba kumi hapo anakuwa kaaga vyeo vya kisiasa vyote.

Usichanganye na mambo ya siasa za Afrika ya Kusini ambapo Mandela alipotoka jela aliruhusiwa kugombea. Lema mwambieni kama anatafuta umandela kupitia jela imekula kwake. Sheria za Tanzania tofauti na za Afrika ya Kusini .Kama ana mshauri koko kampotosha mwanasiasa wa Tanzania kwenda jela ni kujiua kisiasa si kujijenga kisiasa. Tatizo CHADEMA hawana washauri wazuri wa siasa, wana wahuni wa kisiasa.
Lema kafungwa? Unajua maana ya mahabusu? Halafu ujue anahesabika hana kosa hadi mahakama impate na hatia. Pia mahabusu hafanyi kazi labda kufua nguo zake mwenyewe.
 
bridalmask
Watu wa Arusha wana akili sana. Walipochagua upinzani waliamini kutakuwa na mabadiliko fulani ila hadi sasa hakuna zaidi ya vurugu. Wakati huo Km. chache kutoka mjini kuna jimbo la Arumeru Mashariki linaloongozwa na mwanachadema na lina maendeleo na utulivu.

Ni ukweli usiopingika wana Arusha wanaona bora ya wakati wa Mrema wa CCM kuliko Lema wa CHADEMA. Ila muda utaamua, keep on waiting.
 
Yaani ndugu zangu wa mikoa mingine, labda niwaambie tu kuwa kwa sasa Arusha imetulia bila Lema. Watu wanachapa kazi, maisha yanasonga.

Tuko vizuri hata Bbla ya kuwa na mbunge, mbunge Lema alikuwa muhamasishaji wa vurugu kila kukicha. Kama kuna uwezekano naiomba mahakama iendelee kumshikilia na ikiwezekana afungwe tu.

Kiukweli wananchi wa Arusha tulimchagua Lema atupiganie ishu za maji, barabara madawa elimu n.k lakini anatuletea story za kuota ndoto. Huu ni upuuzi na ukosefu wa maarifa ya mbunge juu ya kutuletea maendeleo.

Kwa Sasa Arusha ilivyo nimeamini Lema ndio kikwazo cha maendeleo ya Arusha.
Mara ya mwisho alihamasisha vurugu lini?
 
Back
Top Bottom