Arusha: Askari watano mbaroni kwa tuhuma za rushwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Arusha. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha imewakamata askari watano akiwamo mmoja wa Uhamiaji kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi akizungumza na Mwananchi leo Februari 11, 2020 ofisini kwake amesema polisi hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti.

Amesema askari watatu ambao majina yao wanahifadhiwa mashauri yamefikishwa kwa mwajiri wao kabla ya kufikishwa mahakamani.

"Askari wawili mmoja wa uhamiaji Charles Mashita tayari wamefikishwa mahakamani" amesema

Amesema kuomba na kupokea rushwa ni kinyume cha kifungu cha15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na 11 ya mwaka 2007.

"Natoa wito watu waache kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kwani ni kosa lakini pia hata vitabu vyote vya mungu vinakataa kuomba na kupokea rushwa" amesema.

Mkuu wa Takukuru Arusha amesema Takukuru inawashukuru wananchi wa mkoa wa Arusha kwa ushirikiano wanaotoa kwa taasisi hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Hakuna atakayeshitakiwa. Ni kuzuga tu! Ni hela za kubrush viatu! alisema Mungu wa Tanzania! Persecution, selective prosecution on the move!
 
Sasa kama mtu analipwa 400000 bado anakaa kwenye nyumba ya serikal na hapo anakatwa hela na anasomesha na bado anadaiwa kwa mangi mpaka aje kusubiri mshahara mwisho wa mwezi kwa nini asipokee rushwa angalau imsogeze sogeze
 
Tena hiko kituo cha Sekei wapamulike kabisa.
Tunavuja jasho halafu mtu anabambika kesi ili kupata pesa.
Laana haitakaa iwaache Askari wa namna hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arusha. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha imewakamata askari watano akiwamo mmoja wa Uhamiaji kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi akizungumza na Mwananchi leo Februari 11, 2020 ofisini kwake amesema polisi hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti.

Amesema askari watatu ambao majina yao wanahifadhiwa mashauri yamefikishwa kwa mwajiri wao kabla ya kufikishwa mahakamani.

"Askari wawili mmoja wa uhamiaji Charles Mashita tayari wamefikishwa mahakamani" amesema

Amesema kuomba na kupokea rushwa ni kinyume cha kifungu cha15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na 11 ya mwaka 2007.

"Natoa wito watu waache kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kwani ni kosa lakini pia hata vitabu vyote vya mungu vinakataa kuomba na kupokea rushwa" amesema.

Mkuu wa Takukuru Arusha amesema Takukuru inawashukuru wananchi wa mkoa wa Arusha kwa ushirikiano wanaotoa kwa taasisi hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Askari analipwa 400,000 hapo hapo ana mkopo, huku familia inamtegemea na tulisikia siku hizi wameanzishiwa mpk kozi wanazojilipia wenyewe je tutegemee nini hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom