Arumeru - Watu watano wauwawa kinyama!

Arumeru - Watu watano wauwawa kinyama!

Marehemu mmoja kati ya wanne amekutwa na kitambulisho cha uanachama wa chama cha butcher na cha kupiga kura, anaitwa Richard Ombeni
 
Nime-update thread hakika vifo vya vijana hawa vina sikitisha na vina maswali mengi sana....
 
Nina mashaka na usalama wa taifa, kwani vijana waliouawa wanaonekana vijana wenye nguvu na wenye shughuli zao, pia nina mashaka kama haya mauaji hayahisiani na ile vurugu ya mashamba Arumeru
Mkuu hata mimi nina wasiwasi navijana wa IGP kuhusika na vifo hivi lazima waje na majibu ya kutulizisha maana hata panya ukikuta wameuwawa kwenye mazingira kama hayo razima utajiuliza na utatafuta chanzo....
 
Ama kweli raia watakwisha bila ya sababu!

ninaelekea mtaa huo na bila kama nitapa news ntawajuza wadau! Nitapita na nitaenda mpaka Mlangarini shambani ila kutokana na umuhimu wa Mi kuwa Jf ni lazima nidodose nini kilichojiri anga hizo!

Marehemu walale kwa AMANI YA BWANA!

Ntarudi baada ya!
Mkuu labda kama una ndugu zako maeneo hayo wananchi hawataki kabisa kuongelea swala hili hasa wasipo kufahamu watajua mpelelezi.....
 
ni matokeo ya nchi inayoendeshwa kihuni! hakuna usalama kwa raia
 
Mauaji.jpg
Mauaji1.jpg
 
Jamani, watu 5 wauwawe bila kujulikana chanzo hata tetesi!? Nnamashaka sana
Hakika ukiwaona inasikitisha polisi waje na majibu ya kueleweka vinginevyo mimi nitaendela kuamini kuwa wamehusika.....
 
Kuna maiti tano wameonekana maeneo ya Chekereni Tengeru Arumeru Mashariki karibu na mashamba makubwa ya wazungu asubuhi hii, inasemekana waliuawa kwa kunyongwa then wakaletwa kutupwa barabarani. Source Sunrise Radio-Arusha

Maendeleo ya CCM ndiyo hayo, Naomba sana Watanzania wa kawaida tunaowatumikia hawa walowezi tusikubali kila tunachoambiwa Kutekeleza.
 
Kuna tetesi ya kuwa mauwaji hayo yana weza kuhusishwa na vurugu za za juzi za kugombea mashamba.....
mkuu siganature yako imenigusa sana imegusa imani yangu heb niambie haya maneno alisema nani haya?
 
HUZUNI, HUZUNI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!MSIBA MZITO, LAAAAAAA VERY SAD. haiwezekani vifo vyao viende hivi, hapo lazima kuna jambo zito, nyuma ya vifo vyao
 
Sidhani kama ni sahihi kuweka picha za hao marehemu hapa. Mkuu crashwise nakuheshimu sana ila kwa hili hapana, si sawa
 
Sorry, off topic
Mungi hii signature yako imeniacha hoi!

"Rais wangu anavyopenda kuwazika wenzake! Yupo tayari awazike wananchi wote abaki yeye mwenyewe"
 
Sidhani kama ni sahihi kuweka picha za hao marehemu hapa. Mkuu crashwise nakuheshimu sana ila kwa hili hapana, si sawa

Mkuu hizi picha ni muhimu sana kwa ajili ya ndugu za marehemu kuwatambua ndugu zao..pengine walipotea na ndugu hawana Taarifa!
 
haiwezekani vifo vyao viende hivi, hapo lazima kuna jambo zito, nyuma ya vifo vyao
kweli mkuu.

Walioimba wimbo wa "nchi/kisiwa cha amani" hatimaye (nadhani) watafumbuka macho sasa na kujua waliosema 'wimbo' huo sio sahihi wako sawa au hapana!

 
Back
Top Bottom