Eng. Y. Bihagaze
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,488
- 908
TABIA MBAYA SANA
Kuna wanadam wana akili zilizochoka kweli kweli hawa wenye mashirika ya Tafiti pale wanapofanya tafiti za Kikampeni(sio kisiasa)..
Kwa mujibu wa maelezo niliyoyapata kutoka kwa wananchi mbalimbali hapa Arumeru mashariki, wakati ambapo mbio za kampeni zikiendelea, kuna watu wemevaa vaa vifulana na kujitambulisha kwa wananchi kama wakala kutoka mashirika ya Utafiti. Na wanatafiti nani atashinda kwenye kinyanganyiro cha Ubunge Jimboni humo. Mbona akili hizi zingine za kihayawani this way, Unatafiti nani ashinde!!.. UTAFITI.. au UBASHIRI?.. kwani utafiti si uchunguzi wa jambo ili kupata suluhu au tiba kwa jambo husika, sasa unapotafiti nani ashinde manake nini hasa.. mbali na maana hii ya Utafiti, watu hawa wamekuwa wakikiuka misingi ya haki-lindo ya mwananchi, ni TABIA MBAYA SANA
Kila mwananchi wanayekutana nae kwanza wao wanajitambulisha ni akina nani na lengo lao ni nini, kisha wanamnanga mwananchi ajielezee na yeye ni nani(wanaandika), anatokea wapi (wanaandika), kadi yake ya kupigia kura kama anayo ni namba ngapi(wanaandika) na ikiwezekana wanamuuliza hadi vitambulisho vyake vingne na wanaviorodhesha vyote, hatimae ndipo wanamnanga atoe maoni yake nani atashinda kwenye kinyanganyiro hicho. Hali hii huwatisha wananchi wengi na wengi huwa hawataji hasa mwelekeo wao kwa kuhofia madhara ambayo wanaweza wakayapata baada au kabla ya Uchaguzi.
Rai yangu mtindo huu wa tafiti (za Kikampeni hasa za kwetu TZ) zipigwe marufuku kabisa kwa sababu kuu tatu.
1. Ingawa mwananchi halazimishwi kutoa maoni yake ila kwa mlolongo wa utambulisho anaoutoa ni lazima awajibike kwenye tafiti husika.
2. Wananchi wananyanganywa uhuru wa kujieleza kwa sababu mifano miwili.. mama mmoja alipohojiwa alisema mimi ilibidi iseme itashinda CCM kwa sababu nikisema chama chochote cha upinzani sijui wangenifanya nini vijana wale, naskia unaweza kuchomewa hata nyumba yako kijana mwingine aliyevaa kilemba kinachoashiria yeye ni kutoka chama cha upinzani, alipohojiwa kwa hofu alijibu haraka haraka, itashinda CCM. Na baada ya watafiti hao kupita akawa anawasimulia wenzake kwamba hao ndio usalama wa taifa wanasaka CHADEMA wawamalize. Kuna watu wengi sana wameathirika na kadhia hii ya hawa wanaojiita watafiti ambao huwatumia vijana wadogowadogo ambao huonekana kama makachero flani kutoka kambi zetu...
3. Wananchi wanaopitiwa na watafiti hao, hujikuta wakilazimika kupigi kura chama kile walichokitamka mbele ya watafiti hao kwa sababu wasipokipigia kura hawajui nini kitatokea baada ya wasifu wao kuchukuliwa na Watafiti hao. Hii ni namna ya kunyonga uhuru wa mwananchi wa kupiga Kura.
Taifa letu lina uhaba mkuwa wa tafiti hasa za mazao ya chakula na biashara, tafiti za madawa hasa baada ya kugundua dawa nyingi zinaingizwa nchini kwetu kama majaribio mfano Chanjo wanazochanjwa wanafunzi wetu ni za kujaribishia ndio maana wengi hupata umauti na madhara makubwa kutokana na chanjo hizo labda ufanyike utafiti kuona ni watu wa group gani la damu wapate chanjo ipi na si kukurupuka tu kukimbilia kwenye tafiti za kikampeni ukiacha watu wakifa. vilevile kunai ile tafiti a sindano ya kinga kuhusu magonjwa ambukizi ikiwemo HIV kwamba ukishachomwa ile sindano mwanetu unapitiwa tu chochote na huambukizwi wala nini.. sijui imefikia wapi , kwa mara ya mwisho tulisikia wanajeshi kadhaa walichanjwa .. hatufaham zaidi. Nadhani kuna tafiti nyinginyingi zinazohitajika nchini, kwenye elimu ndio usiseme watutafitie kwanini mwaka juzi (2010) hakukuwa na A ya Kiswahili kwenye matokeo ya kidato cha nne(NECTA)wakati ambapo Kiswahili ndio lugha hii hii ya kwetu iweje iwe Ngumu kiasi kwamba taifa zima hakuna A ya somo hilo. Nadhani tafiti ni nyingi sana hasa nchini kwetu sasa kwanini kuwekeza kwenye tafiti za kisiasa zenye malengo ya kuwachanganya wananchi maskini ya mungu hawa ambao welewa wa kuchanganua mambo kwao si mkubwa sana, wakitishwa kidogo wananywea...nadhani nyie si-mbioni, rede-T na hizi za kikwetu..nadhani data mmeipata..
Kwamba CUF itashinda kwa asilimia kadhaa au CDM au CCM vinawahusu nini ninyi na UBASHIRI WENU, ambao mwisho wa huo UBASHIRI wa KIKAMPENI mnaacha uadui, utengano, chuki na kuwachanganya wananchi. Ni uhaini kumchanganya mtanzania kwenye matumizi halali ya haki yake. TAFADHALI fanyeni tafiti za KISIASA sio za KIKAMPENI.. ni TABIA MBAYA IPIGWE MARUFUKU.