Mkuu, kuna kiwango cha utajiri ambacho ukifika, then kazi unaifanya kwa hiari kama interest na wala si kwa kulazimishwa. Mfano. Bw. Reginald Mengi kama unafahamu huenda ofisini kwa nadra sana pale tu anapokuwa na vitu vya msingi lakini si kwa ulazima. Makampuni yake mengi sasa hivi yanaendeshwa na watendaji ambao ndiyo wanaowajibika kwa lazima kila siku.
Kama umepata kusoma vitabu vya Rich Dad, Poor Dad by Robert Kiyosanki, utagundua kuwa na yeye alistaafu kazi mapema sana katika shughuli zake binafsi. Utajiri wake unamruhusu kuendelea kuishi bila kufanya kazi. Hata hivyo amekuwa na interest binafsi ya kutumia uzoefu wake alioupata kuweza ku-inspire wengine wapate mafanikio.
Unapokuwa na utajiri wa kuweza kukupatia kipato katika maisha yako yaliyobaki, si lazima ufanye kazi (If you do not wish to work) kama nilivyoandika. Lakini kwa hulka yetu wanadamu si lazima iwe hivyo, kujishughulisha ni sehemu ya maisha hata kama wewe ni tajiri. Huyu jamaa Kiyosanki, alipostaafu akiwa ana miaka nadhani 45 au 47 alianza kwenda likizo na kustarehe sehemu mbalimbali hadi mwishowe akaona ni bora apate kitu cha kumshughulisha.
Kuhusu Think Think Think na abundant resources, hili lina mifano mingi. Kuna Taxi Driver namfahamu ambaye 1998 alikuwa anaendesha gari ya tajiri yake Carina, lakini alijitahidi kujenga marafiki wa kweli ambao walikuwa ni abiria anaowabeba ili kujenga biashara ya uhakika, na kila siku aliingia benki kuweka 50% ya mapato yake halali aliyoyapata kwa siku hiyo au iliyopita. Aliendelea kufanya hivyo hadi akanunua gari ya tajiri yake kwa kulipa nusu na kisha kumalizia miezi kadhaa baadaye. Aliendelea na mfumo wake wa kazi na kwa kuwa sasa ilikuwa ni gari yake hakubweteka bali aliongeza kiasi cha pesa alichokuwa anaweka benki.
Baada ya hapo aliuza ile gari na kununua nyingine, na liendelea na kazi huku karibu kila mwaka akiagiza gari mwenyewe kutoka nje ya nchi na kuzifanya private taxis. Sasa hivi anazo gari nne na 4WD ya kutembelea, kajenga nyumba ya kisasa na anaendesha maisha yake. Huyu aliweza kutambua resources zilizo karibu yake na kuzitumia vizuri.
Vivyo hivyo kuna vijana wanne Engineers ambao walianza shughuli zao kijiweni na wakapanda taratibu toka mwaka 1995 huku wakitumia resources kidogo walizonazo, leo hii ni vijana ambao wana mapato na biashara yenye heshima huku wakiwa Wakandarasi daraja la kwanza. Kuna mifano mingine mingi tu.
Angalia interest zako ni zipi, ujuzi wako ni upi, opportunities zilizopo karibu yako ni zipi na jaribu kufikiria ni namna gani utakuwa king'ang'anizi wa kujiletea mafanikio.