alvinroley
Member
- Sep 30, 2016
- 71
- 251
Rais na Mwanasheria nguli wa Malawi Arthur Peter Mutharika (79) kutoka chama cha DPP atajwa na The Sun kuwa ndiye Rais mwenye ulinzi mkali kupita Marais wote barani Africa awe ndani ya Malawi au nje ya Malawi. Wachambuzi wanadai hii labda imetokana na hali halisi ya Maisha ndani ya malawi hivyo jamaa anaamua kujilinda zaidi. Msafara wa Mutharika barabarani huwa ni kufuru na kwa huku kwetu hatujawahi kuuona labda kwa kuwa kwetu ni utulivu na amani ya kutosha. Msafara huu unajumuisha magari 8 ya kijeshi ikiwemo na vifaru kadhaa yakisheheni wanajeshi waliokamilika kwa silaha nzito. Pia huwa kuna magari yasiyopungua 10 ya jeshi la polisi la Malawi yenye askari wa field walio na silaha hatari na wanausalama wengi zaidi. Walioshuhudia video za msafara wake majuzi akitoka Blantyre kwenda Lilongwe kujiandaa na safari ya kwenda mazishini Zimbabwe ni mashahadi. Ulinzi huo haujaishia kwa Mutharika tu, bali pia kwa watoto wake Moyenda, Nikolplix na Charlotte ambao ulinzi wao pindi wawapo Malawi ni kufuru, watoto hawa wanapewa ulinzi wa hali ya juu nadhani nikupita ulinzi wa waziri yeyote pale. Imeelezwa kuwa ulinzi wa Peter Mutharika na jinsi anavyohangaika kujilinda hakuna ulinzi wa Rais yeyote hapa Africa unaweza kulinganisha..