Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mtangazaji kasema Arsenal inacheza kama mabingwa wanavyotakiwa kucheza.
Naaam sahihi kabisa.

Hii EPL kuna muda game inakupalia timu haitembei kabisa, Mpinzani kakukamata kila idara. Hapo ndio bingwa anatoa cheating code anabeba points 3 kwenye mazingira magumu.

Tungekuwa hivi mwaka jana tungebeba ubingwa.

Anayeona tumecheza vibaya, tumepaki basi ahamie Brighton anacheza mpira mzuri kila siku ila habebi chochote.
 
Mpira wa kuburudisha siyo lazima uwe effective ukuletee matokeo.

Iangalie City jana na Liverpool leo.

Walicheza mpira wa kasi, pasi na kuashiria wanapata goli soon. Matokeo yake Liverpool hata shot on target hawan.
Leo nilitegemea mshindi apatikane kwa tofauti ya magoli.

Ila nilikuwa na hofu arsenal hatutafunga mengi kuliko Liverpool

Approach yetu ya Leo ilinifanya niangalie game kwa kurelax nikijiamini goli atakalopata Leo liverpool kama si peneti hawatapata goli
Defence Leo wamefanya kazi iliyotukuka
 
Kai na gyokeres wote ni viazi
 
NImetizama game 2, kiungo cha bruno na rice bado kina changamoto, arteta kama ndio anataka iwe 1st 11 yake, basi hawa wawili ana kazi nzito ya kufanya.

Kai ana upeoo nyama huyu, lakini hamna mchezaji, tzolis bado simuelewi japo ndio afandali tulienae kwa LW, madueke ni KIAZI, ode nae kwangu ni wa kawaida kwa kweli, si mbovu kama madueke ila kiwmago chake hakiridhishi, arsenal ni kwa rice kurudi nyuma hawa watu ni πŸ”₯
 
Kuna misimu tulishindwa kubeba ubingwa kwa kutokua serious. Sasa hivi unaona mentality kuanzia kwa bench la ufundi adi wachezaji wanajiona kabsa wao ni timu ya kupambania ubingwa na sio top 4 ya kucheza UCL. COYG πŸ’ͺπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Huko online mashabiki wa Liverpool wanasema takwimu ni za uongo wana shot on target moja.

Shot yenyewe ni ile aliyopiga Mac Allister. Ukiangalia umbali wa aliyepiga unaona ile ni cross tu ambayo Mac Allister alikosea ikamfuata Raya.

It's nice unapoipiga timu inayojiona inatakiwa kushindania kombe ila sasa hivi inashindania kuonekana ina shot on target.
 
Maajabu ya dunia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…