Sasa hivi hauoni tena picha za tembo yupo juu ya mti.
Mechi mbili zilizopita tulikua nafasi ya pili.
Hakuna aliyekuja kufanya banter.
Arteta kuchukua hili kombe Pep akiwepo imekua ni bigger statement, wapinzani wanaacha play style yao na kuadopt mpya ili kutuzuia.
Makocha wanaopt kua defensive kwakua angalau hii inaweza kukupa point.
Mashabiki wanajua pia. Kwahiyo suluhisho wanadai Arsenal inapendelewa na VAR. Statistics zikaja, maamuzi dhidi yetu yamefanywa na VAR mara 15.
Kwa timu zilizokandamizwa na VAR sisi ni wa kwanza. Mechi dhidi ya Villa tumenyimwa penati na bodi ya marefa ikaongelea juu ya hilo.
Dhidi ya Sunderland, Calafiori alishikwa jezi na kudondoshwa refa hakuitisha penati. Konsa akavutwa jezi akaangukia juu ya mchezaji ikawa penati.
Ukiwa hauangalii mechi utaaminishwa vitu havipo.
Tukiwa tunacheza na City, Michael Oliver akatoa red kwa Trossard, next match akagoma kutoa red kwa Kovacic akidai anahofia kuinfluence mechi.
Tusipopambania matokeo na kutarajia marefa wawe fair we are doomed.