Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Eze mchezaji mzuri ila mvivu. Anacheza kama hataki/ Kibishoo.
 
Kuna nyie vilaza mkizidiwa mnasema mmesusia possesion, ila mkidominate wamepaki basi. Mna commedy sana nyie mazwazwa.

Mpk sasa mna 0 on and off target, dk.49. nawaona mnaset standard.
Arsenal kwenye transtion kwenda kwa mpinzani hawako na uharaka ndo maana timu nyingi zinawahi kukaba ndo inakuwa imeisha hivyo..wanabaki kupiga pass za nyuma na pembeni tu.Wakijakupata viungo wenye uharaka wa maamuzi basi timu itabadirika.
 
Halftime niliingia online nikakuta kila shabiki analalamika kwamba timu imecheza hovyo.

And yes, timu imecheza hovyo siyo kidogo.

Kama ungekua unaangalia mechi halafu upo na watoto wangekusikia ukiwa unatukana tu.

Ila mwendo ni ule ule mwizi anagewa energy ili aendelee kubondwa
 
Hii timu wanaojituma ni wachache wengi wao wanatembelea jitihada za wachache. Timu inawavivu kibao ,timu haina uharaka mpaka labda itokee shambulizi la kushtukiza la wazi sana. Timu imekuwa inaruhusu magoli malahisi mno..kwenye kukaba hawako compacted sana kama timu nyingine.Arsenal wakipigwa msako wa nguvu hawachelewi kufungwa sabab wengi wao wanakaba kwa macho tu.
 
Arsenal kwenye transtion kwenda kwa mpinzani hawako na uharaka ndo maana timu nyingi zinawahi kukaba ndo inakuwa imeisha hivyo..wanabaki kupiga pass za nyuma na pembeni tu.Wakijakupata viungo wenye uharaka wa maamuzi basi timu itabadirika.
Ndio ujinga unaikwamisha arsenal kupata matokeo haraka, ubingwa ule unapotea
 
Ndio ujinga unaikwamisha arsenal kupata matokeo haraka, ubingwa ule unapotea
Angalia hizi game Manchester city atakavyozucheza hadi anakuwa bingwa. Arsenal sahizi badala waamke wapambane sababu ligi ndo inaelekea mwishoni, timu ikidondosha points ndo basi hamna tena marudiano. Arsenal ndo kwanza anazidi kujirudisha nyuma. Anapiga hatua 5 mbele, anarudi hatua nyuma...hivyohivyo hadi ManCity atamkuta na kumuacha. Arsenal hapotezagi sana mechi kwa kufungwa ila yye anakosaga kombekwa sare nyingi😅😅😅
 
Msimu wa tatu makosa ni yale yale hii timu sijui imerogwa na nani.
 
Msimu wa tatu makosa ni yale yale hii timu sijui imerogwa na nani.
Haijarogwa mkuu ila haina mentality ya ubingwa/ kushindana we angalia tu Arsenal tunashinda hasa timu tunayocheza nayo ikikubali ila ikishindana game inakuwaga ngumu sababu ya aina ya wachezaji tulio nao na mfumo wa kocha wa Arteta amekaririka. Naona watu wanalaumu kwamba timu za EPL zinameambiwa zucheze Low block zikikutana na Arsenal.Sasa kama mbinu hiyo inawapa shida Arsenal kwann wasicheze sasa. Arteta akichezewa hivyo ni sare au anafungwa au tubahatishe goal zetu za mipira ya adhabu au kona hatuna mbinu nyingine sabab hatuna wachezaji wakufungua wapinzani zaidi ya wachezaji wakipiga pass tu.
 
Na hiyo ndio maana halisi ya competition, atafutwe tu kocha mwingine huyu atufikishi popote.
 
Na hiyo ndio maana halisi ya competition, atafutwe tu kocha mwingine huyu atufikishi popote.
Arteta akivumiliwa na mwaka huu tutashangaa ila shida pia makocha wazuri nao sokoni ni mtihani si unaona Man u na Chelsea wanavyohaha kufukuza na kuleta makocha wapya. Arteta ni anavumiliwa sababu ndo kwanza anaanza kuinoa timu ya kwanza akiwa kama kocha mkuu na anaonesha kitu kwamba huko mbeleni atakuwa tishio acha aendelee kujifunzia Arsenal ili baadae akikomaa Barca au Madrid wamchukue😄😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…