Ingawa tumeshinda bado matatizo yetu kudifendi yameonekana tena wazi, zaidi katika kipindi cha kwanza jamaa walipata kama nafasi 4 kutokana na maelezo, mawasiliano kwa beki zetu bado ni mabovu na kutojiamini kwa mabeki wetu bado ni tatizo kubwa.
Kwa vile wapenzi wengi wamelivalia njuga hili sualala difensi nadhani labda benchi la ufundi wataanza kufanya kazi ya ziada mazoezini kwa beki zetu. Tukiweza kusawazisha matatizo ya kizembe mfano man-marking, zonal-marking, communication na discipline vilevile wachezaji wetu kwenye flanks zaidi Walcoltt na Arshavin kurudi kusaidia difensi tunaposhambuliwa basi tunaweza kunusuru msimu wetu.