Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Huyu goigoi Havertz mmempa nini siku mbili tatu hizi ?
 
nas
Ukimuona Saint Anne inavyokua busy na matokeo yetu utafikiri ya kwake anayajua vile.

Yani anajitekenya halafu anacheka mwenyewe!
tunamsubiri kwa hamu tuone atacomment nini leo
 
Hawa jamaa wanaichukulia Poa Arsenal yetu.

Mdogo mdogo tunakusanya Points, wakija kutahamaki watakuta tuna alama 90 huko
Hiyo mijamaa tuwe nayo karibu sana, huenda tukaikosa baada ya kukabidhiwa ndoo ya EPL na/au UCL kwa chuki zao. Hawachelewi kufanya maamuzi magumu, kisa tu kuiona Gunners inafanya vizuri. Wamebaki kupika ramli tu sasa hivi.
 
Nilishawai andika humu humu
"namuona ozil kwenye miguu ya Kai"

Niliishia kutukanwa na kebei za hapa na pale
Watu walikuwa wanatoa maneno machafu sana hmu juu ya Kai ila wengine tukawa tunamtetea....inasikitisha kuona baadhi ya mashabiki wanabebwa na upepo wa kejeli za mashabiki wengine.... Mashabiki wa Chelkenge wanaomba sana jamaa afeli pale kwetu ila ndo hvyo Sasa pale amekutana na watu wanaocheza bolu kwlikwli...sio kama Chelsea kule wao wanachojua ni kukimbiakimbia tu....wakiipata wanambutuliaa mbele kwa Jackson mimbio au Mudryk 🤠🤠🤠...halafu wao ndo wajue nn cha kufanya kama kubutua nje au kuporwa....Inasikitisha sana
 
Hiyo mijamaa tuwe nayo karibu sana, huenda tukaikosa baada ya kukabidhiwa ndoo ya EPL na/au UCL kwa chuki zao. Hawachelewi kufanya maamuzi magumu, kisa tu kuiona Gunners inafanya vizuri. Wamebaki kupika ramli tu sasa hivi.
Hahahaha..........kuna mdau humu, alishauri Mashabiki wa Arsenal tuwe tunatembea kwa Makundi kuogopa kufanyiwa fujo na hawa Jamaa ikishindikana kuomba Ulinzi wa Polisi kwa IGP kabisa 😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…