Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kai Jana hadi anadribble, Kuna wengine wanamuona kama mchezaji ambaye hajui chochote kuhusu mpira
 
Lile goli la Kai ndiyo zile runs ambazo anazifanya mara kwa mara. Nafikiri angecheza na Pires angekua on fire kwakua Pires alikua mzuri wa one two.

A fit Partey anaweza onyesha strength ya runs za Kai kutokana na uwezo wa Partey kwenye long balls na thru balls za kuchana defense.
 
Jana Raya alizingua sana, Kai mdogomdogo anakujakuja.

Kuna mtu zile dakika za nyongeza alitaka aondoke, nikamwambia hii arsenal ya sasa subiri hadi filimbi ipigwe ndo useme mpira umeisha
Kai ameanza kunifurahisha. Inaanza kuonekana kama Arteta hakukosea kuendelea kumpa nafasi aimarike hata pale wengine tulipotaka ampumzishe.
 
Kai Haverts ameanza kupata confidence with & without the ball, anajua kujiposition and pia anatengeneza link nzuri na wenzake, mipira ya juu yote yake.

Na pia ameanza kutumia nafasi vizuri hivyo tutegemee mazuri zaidi kwake
 
 
Naona haters wanatudiss kushangilia vile, kwamba tunashangilia sana kuwafunga Luton,
nafkir hawajawai kupata msosi usiku wa manane na ilishakua ulale njaa, ata kama msosi ni ugali dagaa lazima mtu ufurahi, usifanye mzaa kuhesabu mabati
point tatu zilikua muhimu zile, alafu ilikua kidogo tu zituponyoke mara ghafla hz hapa achen tufurahi

Sent from my BKK-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Wale watoto jana waliweza kweli kutuzuia wakitumia advantage ya ufinyu wa kiwanja.

Kuanza kwa Kiwior kulisaidia kwenye kuzuia, at the same time yuko more physical lakini ilikua vigumu sana kwenda mbele ndo sababu muda mwingi Ødegaard alikua akishuka chini kuchukua mali kwa GK, jambo ambalo hatujazoea kuliona mara kwa mara.

Alipoingia Zinny, pale kati kukaanza kulainika. Akawa ana invert na hivyo kumpa breather Ødegaard ili aweze kusogea juu. At the end Øde akatoa assist!
 
Ule uwanja kuna mkubwa atadondosha point(s) pale. Liverpool katoa sare, sisi ndio tumepata ushindi kwa tabu. Hao Chelsea na Man Utd wamemfunga Luton wakiwa kwao.

Luton baada ya kupanda daraja wakaambiwa na bodi ya ligi waboreshe kiwanja chao kiwe kwenye hadhi ya PL. Pale ndio wamefanya maboresho.

Kama alivyosema Ambangile udogo wa kiwanja chao ndio unawapa advantage ya kucover spaces kirahisi, na kikosi chao kina watu walio physical, futi 6+, wako vizuri kwenye mipira ya juu.. no way tungeondoka na ushindi jana ila bahati ilikua kwetu.
 
Siku hizi wapinzani hawataki hata tutoe sare, tukitoa sare utawaona nyumbu na kenge zitakavyojazana humu..

Tunatakiwa tuendelee na ushindi ili kupunguza nzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…