Arsenal (The Gunners) | Special Thread

City wametuachia top spot. This time tuangalie tulikosea wapi turekebishe.

Yes, this is marathon, wala sina matarajio makubwa coz yeyote anaweza kuibuka kidedea, tukimaanisha.. Arsenal, City au Liverpool, hao wengine ambao sijawataja watakua ni wakimbiza upepo..
 
Brentford wana defend na watu 8 karibu karibu, wakikupiga goli umeisha

Uzuri Arsenal tuna watu kule nyuma wote futi 6+ kasoro Zinny tu

Hakuna kazi ngumu kufungua defence ya low block ya watu 8 waliokaa karibu
Leo wametukuta na hangover ya international break, ila hivyo hivyo tumeondoka na point 3 kibabe.

Saka walikua wanam-double, Martinelli hali kadhalika. Arteta akaona Martinelli leo yuko predictable sana, akamtoa. Trossard, mzee wa tight space akatanua uwanja, pira likaanza kumwagika.. Jiooni wazungu haoo!
 
Tumepata points 3, tupo on top ila baeo ugonjwa wa kushindwa kupress advantage haujatuacha.

Hua natamani inapotokea kwamba game inayohitaji tushinde basi mpaka first half tuna goli 2.

Ikatokea tuna game tunatakiwa kushinda goli nyingi basi timu icheze ikionyesha inajua hilo. Badala yake magoli mengi hua tunashinda mechi za kufunga msimu ambazo hazina maana.

Wapinzani wetu mechi za msingi utakuta mpaka dakika ya 60 anaongoza goli 3/ 4. Tukifikia uwezo wa kuona game muhimu na kudeliver kinachohitajika ni bahati mbaya tu ndiyo itatuzuia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…