Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mikel Arteta kuhusu goli dhidi ya Newcastle:

"Kilichotokea ni fedheha, hili bao ni la Ligi Kuu? Na Ligi hii tunasema ni bora zaidi duniani?"

"Nimekaa miaka 20 katika nchi hii na sasa nijisikia aibu. Ni fedheha kubwa sana . Tunafanya mambo ya ajabu kila wiki tena kwa kiwango cha juu.

"Tunapokuwa si wazuri vya kutosha uwanjani huwa nakubali, nainua mikono yangu juu na kuwajibika. Lakini kwa hili hapana, Haifai. Naona aibu kuwa sehemu ya hili."
 
Ila mashabiki tukifungwa tunatafuta kila namna ya kujiona wabovu.

Yaani Arsenal msimu uliopita iliyofukuzia ubingwa mpaka hatua za mwisho unasema Arteta mbovu?

Msimu huu tumezidiwa Points 3 tu na aliye kileleni.Unataka tuanze kucheza mpira wa kubutua butua tena?

Liva Jana Kadraw na Luton, unasemaje Liva mbovu?

Mkuu amini kuna mechi tutafungwa tu sababu ndio mpira.Newcastle wametufunga tukubali tactics zetu hazikufanya kazi.
 
Kwa hiyo leo mnalilia sare?
 
Mkuu umenena sana. Hatuwezi kuwapangia timu pinzani jinsi ya kucheza. Alivyotufunga Newcastle ni sawa na tulivyopigwa na Westwast. Master Arteta anatakiwa aumize kichwa kuona tunatoboa vipi na hizi timu zinazocheza mpira wa Newcastle.

Game kama ile na Newcastle ndo zinamfanya Guardiola atuache mbali kimbinu. Tufanye Newcastle hawakupata goli, je sisi tulikuwa na mpango wa maana wa kupata goli?
 
Washkaji mnaboa sana. Ushabiki wa mpira hautufanyi kuwa maadui na kutoleana matusi. Huu si uungwana kabisa na ni ushamba wa kiwango cha lami.
Huyo ana afya y akili mbona anajulikana, wengine tunakuja huku jf kuondoa stress nashangaa yy ndio anakuja kuchukua stress.
 
Ndugu yangu Execute umeongea ukweli mchungu ambao mashabiki wengi wa Arsenyo hawapendi kabisa kuusikia, humu watu wanapenda kusikia false hopes tu za kina Masingeli na Co-workers wake.
Najua watakubeza, watakukejeli na wengine watadiriki kukutukana kabisa na kukuita mamluki.
Naomba hii comment yako uihifadhi vizuri halafu baada ya kutolewa Uefa uje uwakumbushe tena.
Timu kubwa kama Chelsea, liverpool na Man Utd mashabiki wanapoona tatizo/mapungufu kwenye timu zao hua wana criticize na wanaungwa mkono ila kwa mid table team kama Arsenyau ukijaribu kucriticize unanaonekana ni mhaini
 
Ubaya wa kufungwa na Newcastle ni kuingia jukwaani na kukuta comments za labyrinth. Ila haya ya kutikanana humu siyo poa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…