Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kwa uwezo alioonyesha Raya leo imemfanya mpaka Arteta katoa ya moyoni..

Anasema katika mambo anayojutia kama kocha mchanga ni kushindwa kufanya uamuzi katika wakati uliostahili.

Inavyoonesha jamaa alitaka kufanya sub ya golikipa kwenye mechi tuliyosuluhu dhidi ya Fulham pungufu lakini alishindwa.

Anasema atalifanyia kazi siku za usoni.

Tutaona for the first time tukifanya sub ya makipa msimu huu.

Haya mambo utayapata Arsenal tu.

Hii Arsenal itaniua kwa kisukari jama!

Acha nilale mie! Nitaamka nikisikia mlio wa UEFA 😄
 
Ramsdale huwa ana wenge Sana halafu unakuta Ni muda wakutulia kulinda matokeo

Raya nimeona Ni mzuri kucheza Kross,long balls ,Hana papara kabisa
 
Mnapeana moyo🤠🤠🤠....jana ile penalty yenu kama ya magumashi hvi🤠🤠🤠....ww ambaye sio false hoper una hata kakikombe gani ka kuzugia mkuu🤠🤠🤠...na ule mpira wenu wa piga mbele tukimbizane
 
Kwli kabisa mwaka jana utoto ulitukost sana mkuu🤠🤠🤠...mwaka huu mpk mwezi wa 12 tutakuwa pale juu...baada ya hapo unganeni wte kutuombea mabaya tena maana safari hii lile jambo halitakaa kitokee tena
 


Nyie ndo mnapeana matumaini humu ndani ila sisi tunaongea ukweli . Nembu anza wewe kunionyesha kombe lenu lakuzugia tuone
.

Unanifurahisha sana kuendelea kufurahia kombe la mwaka 2003
yaani miaka 20 iliyopita , ivi miaka 20 unaichukuliaje mkuu?? yaani kombe umechukua kipindi hicho mkapa ndo raisi yaani mstaafu kikwete hana hata ndoto za uraisi leo unajisifu nalo mwaka 2023 .

Kombe unalojisifa wamechukua kina Edu, cygan, reyes ,viera , maya ,lehman na kina henry yaani humo watu wamekuwa makocha na wamefukuzwa wakapata kazi tena za ukocha wakafukuzwa fikiri ni muda mrefu kiasi gani , atleast hata wangekuwa hata kina koscienly au mchezaji yoyote anayecheza saivi tunaona kweli ni kombe
 
UTATOA, HUTOI ?

Sean Dyche alijua itakuwa kama msimu uliopita , kukaa sana nyuma na kufunga goli la kudondokea , muda mrefu wa mechi ilikuwa ULINZI Vs USHAMBULIAJI ( Everton walizuia zaidi na Arsenal kushambulia )

Kipindi cha kwanza kila mtu kuna mahali alikosea

1: Everton walizuia vizuri lakini wakipata mpira hawana sehemu ya kwenda

2: Arsenal wana mali muda mrefu lakini mipango ya kiufungua Everton ilikuwa ngumu sana .

Arsenal kwenye muundo wao wa 3-Box midfield -3 tatizo ilikuwa Everton walikuwa wanafunga sana space katikati ya mstari wao wa ulinzi na kiungo na pia wingers wa Everton waligoma kuruhusu fullbacks wao kuwa 1v1 dhidi ya wingers wa Arsenal .

Nini ambacho kilitakiwa na Arsenal walikibadilisha kipindi cha pili ?

1: Vuta subira

2: Tanua uwanja zaidi pembeni ya uwanja

3: Third Man Runner ( kama goli lilivyopatikana)

4: Uwezo wa kupiga mashuti ( Ball striking )

5: Dumisha muundo wako wa ulinzi pale ukiwa na mpira ili kukabiliana na counter attacks pamoja na kudumisha umiliki wa mpira mkiupata

Na goli la Arsenal lilipatikana katika orodhs hiyo

Subira ( walipoanzisha kona )
Third Man Runner ( Trossard )
Ball striking ( trossard tena )

NOTE

1: Pale ambapo unatakiwa kulinda uongozi wako unamuhitaji kipa wako aoneshe mamlaka kwenye mipira ya juu - Raya


2: Sean Dyche na boli lake daah ndio maana kumbe mpaka sasa hawajafunga goli uwanja wa nyumbani

3. Declan Rice , kila siku anacheza vizuri

4: Saliba na Gabriel walikabiliana vizuri tu na mipira ya juu

5: Hatimaye Arsenal wameshinda Goodison Park baada ya miaka takribani 6

6: WANAKUJA HUKO HUKO JUU , TEMBO ANATAKA KUKAA KWENYE TAWI LAKE

FT: Everton 0-1 Arsenal

#Ambagile

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 

Kombe unalojisifia atleast pawepo na mtu anayecheza mpaka now, ngoja nikupe somo kidogo usije aibika siku nyingine

Mfano man utd iliyochukua kombe la 2013 japo hawajisifu nalo kama wewe na kombe lako la 2004, kombe la 2013 la man utd lina mashiko zaidi kutokana na kuna wachezaji wapo mpaka sasa bado wanacheza mpira na si wastaafu kama wa 2004

Hawa wote wamechukua kombe la epl 2013 na man utd na wanacheza mpaka sasa

1. Welbeck- Brighton. 2. Smalling - As Roma 3. A. Young - Everton 4. Cleverly - Watford 5. De gea 6.J. Evans - man utd 7. Kagawa - Paok 8. Chicharito - LA galaxy.

Naomba nitajie wachezaji 2 tu waliochukua kombe la epl na arsenal ambao bado wanacheza team yoyote ile hata kama ni veteran au cha ndimu kama Kalou wa chelsea alivyokuja kucheza na kina bajana
pale chamazi

Ukitaja hata 1 tu kuanzia leo mpaka milele sisi tutaungana na nyie kwenye kusifu na kuabudu milele humu ndani na tupo tayarii kuchukuliwa utumwani na pastor mackenzie wa humu ndani ili tusifu na kuabudu chama lenu la Arsenal.

Tutajie mmoja tu ? Uone jinsi gani unaongelea kombe la zama za mawe
 
Mkuu Liverpool wanaposema wana makombe 19 ya ligi inajumuisha na ya nyuma...its called history....man utd 20 epl trophies...starts from way back....hvyohvyo kwa uefa...mm zikianza kupigwa story za uefa nakaa kimya....why...kwa sababu sina history yyte...bdo huko ni mdogo na huo ndo ukweli....ila if u talk of domestic cups...tutaongea vzuri...kwa sababu hyo inakufanya uonekane ni one of the best...Invisible wanachukua kombe mi naangalia mpira....sasa ww ambaye unakuja kubweka hmu una lipi la maana mkuu...una epl Titles ngapi...una fa cups ngapi...una carabao cups ngapi....una community shield ngapi....halafu uje uanze kujifananisha na sisi hmm....tunaposema nyny ni wadogo tunaongelea kwny aspects kama hzi....sasa nashangaa sana unajitutumua hmu ndani wkti ww ni bwana mdgo sana....leta history yako ya vikombe hapa ndo tuanze kuongea....vjnginevyo endelea kutuombea njaa tu mkuu siku tukifungwa uje kutupiga mabango
 
Hivi wazee sheria ya offside imekaaje maana jana mpira alipiga Gab ila ukamgonga mchezaji wa Everton ndo ukaenda kwa nketiah, hii imekaaje?
 
Kwli kabisa mwaka jana utoto ulitukost sana mkuu
...mwaka huu mpk mwezi wa 12 tutakuwa pale juu...baada ya hapo unganeni wte kutuombea mabaya tena maana safari hii lile jambo halitakaa kitokee tena
Mwaka huu pale juu hamtapanusa hata kwa dakika 5, Leicester City na wao baada ya kuchukua Epl 2015/2016 msimu uliofata walikua na hesabu kama hizo zenu za kukaa pale juu, nendeni mkawaulize vipi walifanikiwa tena kuwa top on the table?
Msituletee habari za Le Supercomputer.
 
Leicester Wana history gani pale EPL...unazungumzia watu waloshuka daraja mkuu🤠🤠🤠....timu Haina financial muscles yyte....no playing style...nilidhani tuta discuss kimpira kumbe unaongea kishabiki....ukitaka kufanya comparison ya matukio....wafananishe wale jamaa na nyny...wao walipata bahati ya kubeba ndoo wakashuka daraja....nyny mlipata bahati ya kuingia top 4 ila inavyoonekana mwaka huu kama mnaenda kupambana kutoshuka daraja 🤠🤠🤠...yaani mnashindana na Chelkenge kule chini kupokezana matatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…