USARA ZA GWIJI WA HIGHBURY
Arteta au Pep? je hawa Makocha wanafanana Approach vipi kuhusu Arteta kamuiga Pep kama inavyodaiwa tuone kwa kifupi tu
Pep Guadiora ni Muhumini mkubwa wa Possession football ( Mpira wa pass nyingi ) Pep mpira huu kautoa Barca pale ambapo Muhasisi mkuu Johan Cruffy Gwiji la soka Uholanzi
Pep alichokuja kufanya ni kumodify tu na kuongeza baadhi vitu ila hakuondoka kwenye msingi Falsafa hiyo mpaka leo anaongeza vitu ila msingi ule ule kumiliki mpira
Arteta Ulaliwahi kucheza Academy ya barca pia Antiguoko huko jiji Barcelona Spain Hivyo Arteta hizo falsafa alizipitia pia Licha kwamba Pep ndio amemu Influence Sana Arteta lakini swali je kwa sasa wanacheza kitu sawa
Binafsi niseme wanaweza kufanana baadhi ya vitu mfano falsafa ya kucheza na viungo wawili wenye asili ya namba 10 au 8 na kiungo mkabaji mmoja ,ila sio kila kitu Arteta ana path way ya kwake nisikilize
Arteta anacheza kitu kinaitwa Vertical Positional hybrid zaidi kuliko Kumiliki mpira tu
Kwa misingi hii Arteta anacheza na positioning Zaidi yupo Direct kiasi fulani Na mashambulizi ya haraka ( Quick attacking)
Kwanini Nasema Positional play sababu Uchezaji Arteta umejaa positional interchange na flexibility ( Unyumbulifu )
Arteta Licha kutumia baadhi patterns sawa na za Pep mfano 3-2-5 in build up akitaka kuoverload zaidi 2-2-6
Huku msimu huu akijaribu Zaidi kucheza 3-2-2-3 sababu ya uwepo Declan , Timber, Havertz,
Kwanini nasema Positional ndio msingi mkuu wa Arteta kuliko posession ni hivi Unamuona Kai Havertz licha kuwa anacheza Kama LCM on paper ila mara nyingi unamkuta katikati kama Second striker au unamkuta ndani ya box kama CF hii yote inaitwa positional interchange
Arteta na Pep wanaweza kuwa sawa ila wasifanane kila kitu
Amigo adios hermanos