Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kai Havertz deal situation
#AFC

◉ Arsenal opening bid rejected but it’s not over at all;

◉ Talks Arsenal-Chelsea will continue, same as for Rice deal;

◉ FC Bayern, informed/interested but no bid yet as Arsenal leading;

◉ Chelsea always expected 2/3 clubs in the race.

(Romano)
 
Toka saga la mudrick lile nmejifunza kitu kikubwa sana arsenal, kwanza amini ni mchezaji wa arsenal mpk ashike jezi na umwone arteta au edu wamesimama pembeni! Km hilo hujaliona usiamini lolote kutoka klabuni. Mashabiki wengi tulikua tunamtaka caicedo kuliko hata rice! Km uongo tuseme hapa! na ndo tulihisi atakua mbadala mzuri wa partey but final tunaaza kusikia mambo ya Kai sijui wap na wap? Huyu rice now tupo pekeetu lakin utakuja shangaa tunamkosa huyo Kai tupo pekeetu bdo bids zikaua rejected

Nadhani arsenal kuna shida kubwa sana ya viongozi na mifumo ya usajiri. Most of the time hatuleti wachezaji wa kuadf value kwenye kikosi moja kwa moja ila mara nyiny tunaleta wachezaji ambao inatakiwa tuwadevelop then ndo waadd value. Tutafika lin aise. Mara chache sana kuona arsenal tunaingia kwenye biding war na kufaulu kwa top player, nikumbusheni ni lin tulifaulu.

For sure kipindi kizur cha kuisema arsenal ni pale inapocheza kuliko kwenye dirisha la usajiri kwasababu ndo kipindi ambacho romours nyingiiii afu tunaenda kusajiri mchezaji ambae hata hakumtarajia. Ni lin nasisi tutasajiri top top player ni lin?? na sisi tutaingia kwenye bidding war na tukawin?? Ni lin na sisi tutaingia na first bidding na hapo hapo ikawa accepted when when?? Kiukwl mpk sasa sijaona msaada wa Edu sionii kiukwl naona arsenal ni ile ile tu inayostruggle kwenye usajiri toka kipindi cha mzee wangu Wenger

Haya tuliambiwa ipo £200mil ya usajiri ila check tunavyoyumba yumba kumbuka! Man city bdo hajaanza mambo yake ya usajiri bdo liver kama hajaanza kuingia sokoni, Man utd nae km anawaza sana ni lin watauza timu den ndo wangalie soko likoje. Ila sisi Arsenal tumekua wakwanza kuingia sokoni but bid zooote zimekua rejected. Ishu ya macallister kwenda liver imezungumziwa mara nne tu baada ya hapo dogo kashaavaa uzi tayari kumbuka katoka timu hyohyo ya caicedo wenzetu wamepata sisi tulikosa na wakati sisi ndo tulikua wa kwanza kutaka mchezaji.

Kuna shida sehem kwenye upande wa uongozi pale arsenal ###COYG#####
 
huu ndio ukweli ambao uko wazi kwa kila shabiki wa arsenal
 
Kai Bayern washamtia kwenye rada
 
Sema umeandika sana kaka, yapo mengi ya ukwel na yapo mengine ni nje na uwezo wa Arsenal kabisa wapo waliokataa tu kuja arsenal kwa sababu zao mfano Locatelli,Vlahovic hapo uwezi walaumu edu na timu yake,
Kuhusu Edu ni kwel yupo slow sana kwenye mambo ya usajili nahis sio pekeako ni timu yake nzima hadi wale wanaojadiliana kuhusu namna ya kulipa,awamu,aina gani ya ulipwaji na pia kwenye uongeaji nahis kuna pahala wanayumba sana kuna deal nyingi sana alifeli na nyingi alifaulu
 
Priorty zake asilimia 75 hua hazipati kabisa
 

We Share the same sentiments, well spoken; ndio maana namwwmbiaga hamis77 apunguze mzuka
 
Asenyo wachezaji wenu ni wale wa mafungu mafungu, rejected kwenye timu kubwa au wale wa kupewa kwa hisani.
Pep Guardiola amesema safari hii mpambane tu na hali yenu, hakuna mchezaji yoyote atakae wapea kwa hisani.
Ukiona mchezaji yoyote mwenye jina anaehusishwa na Arsenyau tambua hio ni janja tu ya Agent wa mchezaji husika kuongeza thamani ya bidhaa yake sokoni.
 
Kwa maana iyo tubakubaliana Arsenal ina thamani sana sokoni si ndio eeh.. Hadi kuitumia Arsenal kuongeza thamani ya mchezaji wake
 
Duh mnisaidie wakuu Harvetz atacheza namba ngapi pale kiasi awe wa muhimu mnoo kuliko kusajili right Back na sub ya Saliba?

Ni kheri tungesajili Rice na Caicedo kwa mpigo kuliko Harvetz wakati tatizo letu sio kufunga magoli Bali kikosi kidogo hasa eneo la ulinzi.
 
Mkuu usajili wa Kai hau make sense kabisa ilihali hatuja address matatizo sugu kwenye kikosi. Mfano kwenye defense hatuna natural RB Wala sub ya maana kwa Saliba na white kumbuka Tierney naye akiondoka Inatakiwa awe replaced. Mind you Tomi hachezi Tena mpaka January whilst Zinny ni injury-prone.

Ukija katikati tunahitaji replacement ya xhaka na sub yake, so akija Rice Bado atahitajika midfielder mmoja zaidi Ili ku cover left 8.

So ingeleta uhalisia kama Caicedo angesajiliwa maana anaweza toa cover ya CDM na CM pia RB. otherwise tutakua na forwards wengi ila hatuna ulinzi imara hapo kati na kwenye defence.

Kingine Saka Hana sub ya kueleweka, hatuwezi compete UCL na ligi kwa kumtegemea Nelson kama sub ya Saka.

Huyu Arteta mnamuamini sana ila tokea msimu uliopita nilisema tatizo ni depth hasa defense na asipo address tutaendelea kusindikiza tu, watu wakabisha na kejeli kibao leo hii Yako wapi baada ya kuumia Saliba?
 
Mi kiufupi arsenal timu yangu siielewi kabisa tumejitoaje kwenye dili la caicedo ambaye ni mutiple position player tunangangana na Kai

Just imagine mpka now tungekuwa na
Laporte
Caicedo
Rice
Cancelo
Afu tunamvizia gundogan/dani olmo/olise
Kikosi chetu kinashida sana kwenye ulinzi na mido so tuwekeze huko.
 

I was disturbed kumkosa Caicedo, better we miss Rice lakini sio hiki chuma
 
200M kwa mpira wa siku hizi siyo pesa ya kujisifu unapoenda nayo sokoni.

Katika 200M chelsea wanakuambia utoe 70M kwaajili ya Kai. Kwangu mimi Kai siyo mchezaji wa kutisha jamaa hajawahi kua na magoli zaidi ya 9 msimu mzima na kuna mashabiki wanaamini akija pale atakua moto.

Mtu mmoja Twitter anakuambia anakuja ili awe ndiye dominant shot taker pale mbele. Halafu ili kuprove hilo akaweka comp video ya kabla hajaja Chelsea, tatizo ni nini unajua? Hata chelsea walitumia comp vid hiyo hiyo kututhibitishia kua wamepata mchezaji mzuri.

Timu inayohusika na usajili ina ujinga mwingi. Same old Arsenal, inamtaka Buendia, Aouar, anakuja Lokonga na Vieira., Tushahitimisha tunahitaji kiungo ambaye yeye mwenyewe aliiaga mpaka timu yake kuna 90M ya Mudryk kwanini isitumike kwaajili ya Caicedo?

So Chelsea atakuuzia Kai kwa 70M kisha ataongeza 20M hivi anachukua mchezaji ambaye ni instant impact kwenye timu yao. Clever. Sisi tukichukua Kai itabidi tucheze 3 2 4 1 ili kumpa uwezekano wa yeye kupata namba kwakua wote tunajua Emile anaweza kufanya hiyo kazi ya shot taking pia hivyo hana wa kumuweka bench pale mbele.

Mi siamini Rice kama mchezaji ambaye inatakiwa kutumia zaidi ya 50M plus English tax tufanye 70M lakini West Ham wanataka 80M+ kichekesho City inamtaka Rice pia, hapo hapo ina Rodri na Kalvin ambaye anasugua benchi tangu afike.

Mashabiki tuliamini kwamba tunahitaji back up ya Saka, Caicedo na kiungo mwingine wa kudevelop pale, na ST ila sasa hivi unasikia ujinga wa Kai na bid ya Caicedo kua rejected

Upande mwingine ni kwamba PSG imeachana na Julian na imemgeukia Arteta, so leo au kesho tukisikia Arteta kaenda PSG itakua ni kwaajili ya ujinga wa bodi kutoelewa kocha akitaja targets zake basi hizo ndiyo anamaanisha anazitaka.
 
Trend siku hizi timu inakubaliana na mchezaji ikirudi kukubaliana na klabu ni bids kua rejected tu.

So saa hii United imemkosa Kim kaenda Bayern. Kwa Kane imekua ngumu, wakamuulizia Osimhen, Hojlund na Ramos wtimu zote zikataka 100M ili kuachia mchezaji.

Kwa kuhofia kupigwa wameenda kwa Watkins wa Villa. Jamaa kascore 15 goals msimu uliopita, msimu wake mbovu bado ni mzuri ukilinganisha na wa ST wao. Wamefika wamekuta Watkins anajadiliana kuongeza mkataba na Villa.

Na huyu Monchi aliyekuja hii inamaanisha Villa inaenda kua na ambitious na focused kuliko ilivyo sasa so na wao hawatotaka kumuachia Watkins na wakimuachia basi bei itakua ndefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…