Arsenal (The Gunners) | Special Thread

mkuu nimesema kuwa zamani tulikuwa tunashinda kirahisi kwa sababu zile game zilikuwa hazina umuhimu wowote tofauti na pride ya Team

Hakuna watu wanamjua vizuri pep kama Arteta, baada ya game ya leo ni wazi kuwa mbio za ubingwa ndio zimeanza rasmi, wakati pep anaanza mbio rasmi za ubingwa sisi team imejaa vijana ambao ata kumaliza nafasi ya 2 tu hawajawahi

Anyway, Sawa mkuu naheshimu mawazo yako
 
Acheni kukufuru nyie viumbe,
Umfunge Man Utd zaidi ya goli 3 kwa kikosi gani hasa mlichonacho?
Hilo goli la 3 lenyewe refa aliamua kuwapa tu ili mpunguze maneno maneno, maana kabla ya mechi mlikua mmeshaanza kumtuhumu kua atawabeba united.
 
Mechi ya kwanza ya ligi ya Arsenal Vs City iliahirishwa Kwa sababu ya msiba Wa Malkia Elizabeth II. Itachezwa mid February.
 
Acheni kukufuru nyie viumbe,
Umfunge Man Utd zaidi ya goli 3 kwa kikosi gani hasa mlichonacho?
Hilo goli la 3 lenyewe refa aliamua kuwapa tu ili mpunguze maneno maneno, maana kabla ya mechi mlikua mmeshaanza kumtuhumu kua atawabeba united.
Kiushabiki tutabishana saana, tukiongea kisoka utaona nilichosema.
 
Wewe jamaa una hoja na ndicho nilichokiona leo, nyakati Kama hizi, ndio mbio za Ubingwa zinaanza ,

Zinny na Jesus ningekuwekea video hapa uone wanavyoongea dressing room ,nashindwa kuweka video hapa
 
Kwa kweli gem ya leo Zinny amekuwa km mchezaji mkongwe wa miaka 30+. Utulivu wa hali ya juu na upambanaji wenye shauku ya ubingwa. Saka ni mashine ila kwa gem ya leo Zinny ametuheshimisha sana
 
Nikisema humu Namkubali Sana Zinny ,watu hawanielewi

Kwanza Ni Arsenal fan tangu mdogo

Hakati tamaa Hadi dk ya mwisho

Kyle Walker aliwahi kuulizwa hapo mancity Ni mchezaji gani Ni fundi(technical)

“In terms of technical ability - I’m nowhere near! - not in any order because I wouldn’t want to put them in order, my top three are Zinchenko, Mahrez and Silva,”
 
Wewe jamaa una hoja na ndicho nilichokiona leo, nyakati Kama hizi, ndio mbio za Ubingwa zinaanza ,

Zinny na Jesus ningekuwekea video hapa uone wanavyoongea dressing room ,nashindwa kuweka video hapa
Mkuu pep saizi anatusubiri tu kwenye game zetu maana anajua fika tutakuwa na pressure juu juu kama kuku kwenye joto kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…