Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Aisee hakuna Jersey Kali kama hii nyekundu, Kila mtu akivaa lazima imkubali


Tukibeba Kombe la EPL Mwaka huu lazima nitoe OFA kuwanunulia akina lembu Flano na wenzao wanaokesha kuiponda arsenal yetu humu
Arsenal naipenda sana tangu enzi za Arsene Wenga kwa sababu ya good football ila wanaoichafua Arsenal ni mashabiki ambao sio wastaharabu kabisa. Na ndio maana ningependa Arsenal ibebe EPL mwaka huu
Mkishindwa mtaendelea kulitamani kwenye picha tu. City ni wabovu, Liver ndio hovyo kabisa, Chalsea ndio hiyo kwanza ujenzi uko kwenye lenta, contenders mwaka huu ni Newwcastle. Bahati yenu hiyo msiachie iende bure
 
Kusema City ni wabovu hayo ni mawazo mgando , hujamjua vizuri Pep hakika.
 
Kusema City ni wabovu hayo ni mawazo mgando , hujamjua vizuri Pep hakika.
Kwa msimu huu city ni wabovu compare miaka miwili ya nyuma, wachezaji wako axausted akiwemo Kelvin De Bruyne na wenzake. Hii haitaji hata kuielezea sana, matokeo na uchezaji wao unaonekana. Na mwanzoni pia nilitahadharisha dependecy walioweka kwa mfungaji mmoja ambaye ni Haaland utakuwa na madhara sana kwa City kwa sababu
  1. asipokuwa kwenye form,
  2. akienda majeruhi au
  3. wenzake wakigoma kumpa ushirikiano,
timu imekufa. Ndicho kinachotokea taratibu sana
City ataendela kupoteza mechi moja moja na au kutoa sare kitu ambacho itaendelea kuwapa ninyi Arsenal advantage.
Mimi nabashiri hata Man u au Newcastle wanaweza kumpiku city kwenye second position, hadi tufike March, City atakuwa kwenye 3 au 4. Take my word IMO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…