Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Wewe una chuki binafsi na arteta au labda uliacha kuifatilia arsenal kwa muda

Hivi unaposema inacheza vibaya una refer kwa Wenger au mm ndio sielewi?

Hivi umesahau Arteta kaikuta arsenal kwenye hali ipi?

dully jr atanisaidia ,kipind cha emery ilifikia hii timu hata pass 10 Haiwez kupiga, ilifikia Arsenal mech Emirates tunazidiwa umiliki wa mpira , tunashinda kwa bahati , away games hata Watford tunapaki bas, Hivi unayakumbuka haya?

Tunabaki na mech 4 tunahitaji point 3-4 twende top 4 emery anashindwa na Europa fainal anadhalilishwa na mvuta sigara Sarri,

Arteta anaikuta timu haiwez tena kufanya buildup kuanzia kwa kipa, haiwez kuposses mpira ,anaisuka had anafikia hapa mech za Emirates ukija wapinzan wanaogopa ,

Uliona wolves hawa wagumu pale Emirates wanaomba po, huku had kocha wao anafanya uhuni wakupoteza muda kwa sub? Mpe credit huyu Arteta ,

Leo Arsenal anatoka nyuma kuanzia kwa kipa had anafunga goli , unasema haifurahishi ? Ulikuwepo kipind cha Unai emery kweli? Enzi Lucas toreira anacheza had no 10., Midfield ya xhaka guendouz?

Arteta ameanza ujenzi wa hii timu kwenye eneo la backline ambalo had Wenger anaondoka aliliacha ni bovu ,now amekuja kwenye midfield na attacking,

Nadhani Uliona shughul aliyooneshwa mancity pale Emirates bila refa kuingilia kati,

Hiyo ni advertise ya tuendako, now pale Emirates hiyo ndio itakuwa atmosphere,

Kama unataka ujue Alipoitoa hii timu Arteta , rejea arsenal ya emery ndan ya miez 18 aliyokaa , hata buildup ilikuwa mtihani ....
 
Naona kama alishindwa kumtumia Aubameyang vizuri. Mtu aliyezoea kuwa kinara wa magoli tangu aje, ila magoli yake yakapungua kwa Arteta.
Hivi si ndio nyinyi mashabik mlipiga kelele sana Arteta amdrop Auba?


Leo anafunga huko barca tayari inao ekana hamtumii vzr ,jaman tuache unafiki, huyu Auba sindio kachukua FA na Shield ndan ya Arteta? Tena alikuwa kipenz chake?

Mashabik mlipiga kelele sana Auba anakosa magoli dhid ya Newcastle yeye na wavu, dhidi ya man u anakosa magoli mawili , leo mnasema alishindwa kumtumia?

Mlipiga kelele sana ampige chini lkn Arteta akawa anampa second chance ,mkasema ampe nafas martinel ,mwisho Auba akawa nidhamu Zero , amefurumushwa mmerudi kumsimanga Arteta , lakin ndio sisi mashabik tuliomba am drop akaendelea kumpa second chance,leo anafunga huko barca anaonekana Arteta ndiye mwenye shida

Auba ni finisher mzuri sana , lkn muda wake arsenal uliisha ,

Arteta pale Arsenal ana total control ni Manager sio head coach, amemvumilia ikaonekana atawaharibu na watoto wengine as captain , ingeonekana ni Jambo la kawaida tu kujifanyia utakavyo ,, hii hali imeanza mwishon mwa arsene Wenger, ozil kuna mech alikuwa hachez anapoamua ,taarifa inatoka ana mafua ,
 
Mkuu unataka mpira gan chini ya Arteta ?

Unajua ili uupate huo mpira unahitaji wachezaji wenye profile husika?

Arsenal aliyoikuta Arteta chini ya emery kamwe isingewezekana kucheza mpira wa kuufurahia ,sisi ni mashahidi hapa , labda kwasababu tuna kawaida ya kusahau,

Mashabik pale UK walimwambia kwa mabango emery , NO TACTICS,NO STRUCTURE,

Emery kakaa arsenal miez 18 hakuwahi kuwa na 1st 11, hakuwa kuwa na structure ya uchezaji,

Arteta kapokea timu ya namna hiyo, hivo alihitaji Overhaul kubwa, akianza na backline yote kuanzia kipa had namba 6 , ndipo unapokuta sura mpya , had Leno anaondolewa maana mpira wa kufurahisha unaanzia kwa kipa ,

Na Tunaona Process , Arsenal ya emery mech za Away ilikuwa kiama, za Emirates tunabahatisha,

Mfano mech ya wolves kwa emery ile hatoki, lkn kwa Arteta limepigwa ball , had wanataka wakimbie mech ,

Unaposema Arsenal haichez mpira wa kufurahisha inabid utueleze Arsenal aliyoikuta Arteta ilikuwa inachezaje je ni ile ile ambayo hata kufanya buildup ilikuwa haiwez, mm nitakupa hata magoli 20 chin ya Arteta yanayoanzia kwa kipa had Goli,

Hapo Epl ni swala la muda mfupi utaelewa Arteta ni masterclass kwenye mbinu,

Kwasasa amempeleka xhaka kwenye new role ,

Makocha wengi hapo Epl wanapokutana na low block imekuwa ngumu kuzifungua , Arteta nimemshuhudia akizifungua vzr tu,

Timu inapokuwa pungufu amweza kuicheza low block ya hali ya juu , sio kwa kubahatisha ni tactics

Narudia ule moto aliowashiwa city pale Emirates ,refa akaingilia kati ,mimi nauchukulia Kama Onyo kwa wengine wanaokalili ,

Na nimeuona tena Dhidi ya Wolves ,hadi Bruno lage akataman aikimbie mechi

Ule moto Nauchukulia ni Onyo kwa siku za mbelen kwa wanaokalili Arsenal kwa timu kubwa atapigwa kirahisi tu,

Hii ni process na ni project inayopiga hatua vzr
 
Dah Hizi picha Zina zaidi ya Maneno Milioni moja Ya Kuelezea Jinsi Gan Martin Odergaard Anajituma na Kupambania Hii Team

Kupata kitu kama Hiki kwa Wachezaji Lazma Kocha Uwe na Uthubutu na Uwe na Mipango na Mbinu Zinazoeleweka..Kila Wakati Huwa Nataman Sana huyu Odergaard na Partey Wapokee Mpira nione Jinsi wanavyotoa pasi kwa usahihi na Kwa Kujiamini..

Smith Rowe ni Kiungo mshambuliaji na Huyu ni Playmaker/anachezesha team Halafu ana Work Rate kubwa mnoo..Tofauti Yao ni Kwamba Huyu dogo ni mtu wa mipango Sana ila Rowe ni mtu wa Kushambulia sana..Rowe anapenda Kushambulia ila Odergaard anapenda Kutengeneza sana.

.Bado ana Nafasi Kubwa mno ya Kufika Mbali zaidi ya Alipo..Huyu Mtoto ni Bonge la Mchezaji Aiseee. Yan Huyu Akikolea Pengo la Ozil linafutika Kabisa Huyu anakupa Assist Magoli na Anazunguka Kila mahali bila Kuchoka na anajua Sana Soka la Kuvutia..


 
ARTETA ANAPOIANDAA 4-3-3 TARATIBU

✍🏿 Nianze kusema mpira ni set up au tunaita plan vitu hivi vinatengenezwa ndani na nje ya uwanja nikimaanisha training session ,video analysis nk

✍🏿 lengo ni kutengeza kilicho bora wakiwa uwanjani ikihusisha ushambuliaji na kujilinda na ndio maana kiufundi kuna kitu tuna tactical and technical changes

✍🏿 hapa kwenye tactical (mbinu)ndio tunakuta mifumo.

✍🏿 Arteta alipokuja alipenda zaidi kutumia 3-4-3 mfumo ambao tulitumia zaidi counter attacks na maeneo ya pembeni kushambulia ila baadae ulishindwa tupa mahitaji

✍🏿 ndipo arteta akaja na 4-2-3-1 baada ya kumuintroduce rowe na kumleta odegaard lengo sasa kutumia eneo la katikati pia kushambulia kuwa na njia nyingi za kutengeneza nafasi

✍🏿 lakini sasa kadri siku zinaenda naona arteta anataka sasa kucheza mfumo wa mwalimu wake pep guadiora

✍🏿 mfumo 4-3-3 ambao kimsingi anahitaji kumiliki eneo la kiungo ili kuwepo fluidy na transition ya mpira kwa usahihi maana anaanzisha mashambulizi toka nyuma

✍🏿 ukifatilia kwa sasa licha mfumo mama kuwa 4-2-3-1 on paper ila display uwanjani tukiwa na mpira ni 4-3-3 odegaard hachezi tena kama tradional 10 bali deep lying playmaker au 8 ambayo ipo advanced kidogo hiki kitu kinafanya sasa kati kati tunakuwa na viungo watatu mmoja partey anaesimama kama pivot na huyu kazi yake ni kuchukua mipira kwa mabeki , na anatakiwa awe na uwezo mkubwa wa kupiga pass za mbele kwa usahihi mkubwa bila kupoteza ovyo, hii Role ilimshinda Lucas toreira ,pia Xhaka ilimletea matatizo ya kuchomesha sana, Partey ameimuda kwa asilimia kubwa , Areta aliwahi kusema anahitaji kiungo wa chini kariba ya Michael Laudrup, sikumuelewa kipindi hicho

✍🏿halafu ode na xhaka kama namba 8 wawili japo wana operate kwenye different zones ode uwa anapanda zaidi naweza kusema anacheza half 8 half 10,ndio maana tunamuona sana siku hizi upande wa Saka muda mwingi wakibadilishana space

✍🏿 hii kitu ipo man city kitambo tu tangu kina david silva wapo pale anacheza na de bruyne chini yao ni fernadinho

✍🏿 namuona arteta akitafuta rhythm kwa msimu ujao akiongeza kiungo mwingine CM nazani sasa ataucheza kwa uhakika

✍🏿 nimalize kusema 4-3-3 modern days sio lazima uwe na natural striker yani goal potcher tu bali uwe na striker anaweza kufanya link up na viungo kudrop chini kazi anafanya laca, Hii inaonesha Tayari Arteta kichwani mwake ana profile ya Striker gan anamuhitaji summer

✍🏿 tukisajili striker naamini ni kariba hii sio striker anae subiri tu mpira ndio maana ya team play kila mtu ahusike

 
Ødegaard anaanza kuwa one of my favourite Arsenal players, I love his energy in finding spaces and ability to play the right pass. Moves nyingi za magoli zinaanzia kwake, ana vitu vingi sana uwanjani lakini the footballing brain is his best attribute, the kid gat the brain.

MECHI NA WOLVES INAONESHA ALIKIMBIA TAKRIBANI KM 20.2 ,

I WISH NEXT WEEK ATARUDI NA ENERGY YA KUTOSHA

INASEMEKANA ATAKUWA CAPTAIN MPYA AU VICE CAPTAIN NYUMA YA KIERAN TIERNY NEXT SEASON


WAKATI EDU ANAMTAKA EMI BUENDIA , KWA £35M ,ARTETA AKILI YAKE NA FIRST CHOICE YAKE ILIKUWA ØDEGAARD KWA £30M
 
WAKATI WATU WANASEMA ARTETA AMELETA MPIRA ARSENAL USIOFURAHISHA ,

PEP GUARDIOLA ANAITAJA ARSENAL MOJA YA TIMU ZILIZOMFUNGULIA BUSTA


Pep (teams style of play) “Except Liverpool, Brighton, Arsenal, Villa, Leeds, the rest sit back. I’m not saying there's anything wrong with that. Every manager can do what they want.”

Zaidi soma hapa
 
Hapo chini ni video Arteta akimwambia Bruno Lage aendelee kupoteza muda tena

Narudia tena jaman kuna watu wamekariri Sana Pale Emirates kuna point za ubwete,

Ile BUSTA aliyofunguliwa Pep GUARDIOLA sikuile mpaka refa akaingilia kati ,kwangu niliichukulia Kama Onyo kwa wengine ,

Ndicho kilichomkuta Bruno lage,

Na Leo Pep GUARDIOLA amekiri Arsenal ni miongon mwa timu ZILIZOMFUNGULIA Busta

 
Mikel Arteta is a good tactician, Mambo ya mpira yanabadilika haraka sana, watu wasichoelewa ni kuwa Mikel Arteta anakosa baadhi ya complete profile, kuna replacement mbili zikifanikiwa basi Arsenal tunakuwa a tittle challenger, ndio maana target kuu ya Arsenal ni kupata a top CF & CM, anachohitaji Mikel Arteta ni upgrades kwa Granit Xhaka pamoja na Alex Lacezette, we gonna be untouchable Under Mikel Arteta.
 
Sina chuki bro. Nimesema bado sijamkubali kikamilifu. Kazi yake yeye ni kuendelea kuperform mpaka hapo nitakapoona amefikia kiwango ambacho kitanifanya nimkubali kikamilifu. Ni hayo tu.
 
Asante bro. Nitafurahi sana tukifika huko.
 
Itakuwa anarefer arsenal ya wenger
 
odegard vip hapo cjaelewa
 
Arsenal this EPL season:

With Auba: 14 games. 18 goals.
Since dropped: 9 games. 20 goals.

Arsenal have been better despite his scoring for Barcelona. These are the facts |
@Football_LDN
 
Nilisikia tunahusishwa na frank de jong

Na kuna habari nilizioana frank de jong anaweza kutua viunga vya gunners

That day, ntachinja mbuzi

Pia inabid tuongeze beki pale nyumba, saliba au aingie mwingine


Namba Tisa, yes inabidi aweze kucheza kitimu na sio kusubili mpira kama lukaku


For this to be done, we must secure top4 by peace or violence

#COYG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…