Wakuu kiaje habari za siku nyingi.
Naona nimepitwa na mengi hapa.
Usajili Arsenal wamemkatalia Maitland Niles kwenda Leicester kwa sababu Arsenal wanawachukulia Leicester kama mahasimu kwenye kugombania nafasi za juu kwenye ligi.
Hivyo Arsenal wanaona Niles akienda Leicester atawaongozea nguvu.
Hivyo kuna uwezekano mkubwa akaenda West Brom.
Niles amekataa kwenda Southampton kwa kuogopa kupangwa nafasi ya beki ilhali yeye ni mchezaji wa kiungo.
Ni kama ilivyokuwa kwa Real Madrid ambao walikataa Odegaard asiende Real Sociedad kwani klabu zote zinapigania nafasi za juu kwenye La Liga.
Mustafi amekubaliana na Arsenal kukatiza mkataba wake na sasa aelekea Ujerumani kuchezea Schalke.
Dogo Joe Willock anaenda Newcastle.
Arsenal next, ni kesho na Wolverhampton Wanderers.