Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Km sikukuelewa vibaya basi jana baada ya line up kutoka ulionekana kutokubaliana na Smith - Rowe kuanza lkn naona baada ya kuona alichofanya umemkubali
 
Nilipenda sana ile faulo ya Xhaka... Ila ile chop ya Saka nilipenda zaidi kwani ilifanya wajiamini zaidi
 
Km sikukuelewa vibaya basi jana baada ya line up kutoka ulionekana kutokubaliana na Smith - Rowe kuanza lkn naona baada ya kuona alichofanya umemkubali
Itakua hukuona next comment ambayo nilisema.

Sofascore ilionyesha tunacheza 3 4 3 na emile acheze kama rwf ila saa hii inaonyesha ni 4 2 3 1 huku emile akicheza namba natural kwake.
 
Mechi yetu ya Jana dhidi ya Chelsea imetuonesha Morale ya timu imeanza kupanda hasa baada ya kuwatumia wachezaji vijana akina Smith na akina Martinel.

Timu ilipambana hadi nikahisi huenda wachezaji experienced akina Auba, Willian and the likes wanamuhujumu kocha au ni Fatigue ya kucheza michezo mingi pasipo kupumzika.

All in all we are back, and hope our wins yesterday will going to elevate our momentum to the next fixtures.

Let's meet at the top 🥂🥂🥂
 
Mwizi inavyo onekana anatumia watu kunivuta shati.
Ila leo mwizi kakatiza WBA, kumbuka huo mtaa ni wawalala huo, hivyo miundo mbinu ya njia yao sio mzuri.
Njia ina matope na vidimbwi vya maji ya mvua, hivyo lazima mwizi aanguke.

Kuinuka na kujifuta matope tayari nitakua nishamkaribia.

Kwahiyo bado sijakata tamaa ya kumkimbiza mwizi.
Nina imani mpaka kufika mwishoni mwa mwezi wa pili nitakua nishamkamata na kumpukutisha kila kilicho changu.
Mzee wa kukimbiza kimya kimya, naona mlikaribia kumfikia mwizi mkaanza mayowe.

Mwizi kawaacha tena.
 
Ushindi huu lazima mtu kama Dully Jr arejee.
Ongereni kwa kutukamatia mtu shati
No ni sikukuu ndio imenirejesha mkuu,nilikuwa porini huko network shida ila sasa sikukuu imenogeshwa na sisi kuwabandua goli 3 the blauzi
 

Hahaha, mwizi amefuzu mafunzo ya kikomandoo, anapambana na hali zote.

Huo mwezi wa pili utakuwa unamuulizia kwa watu, tena nao watakuwa wanakwambia hatumwoni.
 
Top gani unaizungumzia mkuu. Nyie maeneo yenu ni hayo hayo mid table, pale top six kwa chini kidogo. Jana ni kwamba tuliwaombea mshinde kwa kuwa hatutaki kuona mnafukuza kocha maana ndiyo mtazidi kujivuruga.

Mambo ya top tuachieni sie na hao Looserpool. Wiki mbili hizi tumeinama kidogo kurekebisha baadhi ya sheria naona watu washaanza kujisahau. Wameanza kukichezea kiti!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…