*SIASA YA CHINA ILIYOZIMA NDOTO ZA MESUT OZIL KATIKA SOKA LA KIMATAIFA*
*Ukizungumzia* China Chini ya *Rais Xhi JINPING* Ni Moja Kati ya Taifa Lenye Idadi Kubwa ya *Watu na Taifa Lenye Uchumi Mkubwa Duniani* Moja ya *Doa la Taifa Hili la China* Ni Mauaji ya *Jamii ya Kiislamu ya Uyghurs* Moja ya Makabila Makubwa Sana Yenye *Idadi ya Watu Zaidi ya Milion 10 Nchini China Katika Jimbo la XIANJIN* Kabila linalopatikana Katika *Kaskazini Magharibi mwa Nchi ya China* Mpakani Kabisa Mwa Nchi za *Turjikistan*
*Tatizo la Mgogoro Huu Lilianza Kwa Post ya Mesut Ozil ya December 13 Mwaka 2019 Kupitia Katika Mitandao ya Kijamii ya Instagram,Twitter,Webo China na Facebook .....Kwa Kijana Huyu Mwenye Umri wa Miaka 32 Mzaliwa Gelsenkrchen,Ruhr Region Nchini German* Kuishutumu Nchi ya *China Kwa Mauaji Dhidi ya Jamii ya Uyghurs,Kufunga Misikiti,Kubambikiwa Kesi na Utesaji wa Mara kwa Mara wa Raia Hawa*
Baada ya Kauli Hii *Shirika la Utangazaji la China* Lilikatisha Matangazo ya Mechi Kati ya *Arsenal vs Manchester City* iliyofanyika Jumapili ya December 15 na Club ya Arsenal ikatoa Taarifa Rasmi Kuwa *Kauli ya Ozil Ni Kauli yake Binafsi na KLABU ya Arsenal Haiusiki na Matamshi ya Mesut Ozil* na Pia *Serikali ya China Kupitia Kwa Msemaji wa WIZARA ya Mambo ya Nje Bwana Jheng SHENG* alitoa Taarifa Kuwa Aliyotamka Mesut Ozil Ni Uzushi na Hakuna Kitu Kama Hicho Katika Serikali ya China na *Akamualika Ozil Afike Kaskazini Magharibi mwa China Kuona Maisha Halisi ya Jamij Hii ya Uyghurs* ....Baada ya Kauli Hii *Mashirika Kama Amnest international na Serikali ya Marekani* iliikashfu China Kwa Kukiuka Haki za Binadamu na Kwenda Mbali Zaidi *Shirika la Hali za Binadamu la Amnest International* likachapisha Jarida Dogo kwa Ajili ya Kuelimisha Jamii na Duniani Kuhusu Maisha ya Jamii ya Uygurs na Kusapoti Kauli ya Mesut Ozil
*Mechi ya Mwisho ya Mashindano Mesut ozil Kuichezea Arsenal ilikuwa Dhidi ya West Ham Katika Dimba la Ashburton Groove March 07 Mwaka 2020* na Mechi ya Mwisho ya Kirafiki ilikuwa Corona Season June 10 Mwaka 2020 .......
*Msumari wa Mwisho kwa Ozil Kwenda Kwa KLABU ya Arsenal Ni Mahojiano yake Kati ya Jarida la Michezo la Athletic Kuishutumu KLABU ya Arsenal Kuweka Kipaumbele Kampeni ya Black Lives Matter Badala ya Kampeni ya Muslim Lives Matter Ambayo Kimsingi anaamini China Kuna Ukandamizaji Mkubwa Sana wa Haki Dhidi ya Jamii Hiyo ya Kiislamu*
Kutokana na Kadhia Hii ya Mgogoro wa China na Faida inayopata Ligi Kuu ya Uingereza Mkakataba wenye Thamani ya £700,000,000 wa Haki za Matangazo Mpaka Mwaka 2022 Ni Sababu Tosha ya Mesut Ozil Kuwekwa Kwenye Blacklist ya Kuvaa Jezi za Washika bunduki hao wa *Ashburton Groove*
Mbali na Misukosuko ya Kutochezeshwa Katika Mechi za Mashindano za *Arsenal* Lakini Mesut Hakusita Kupiga Kelele *Kufukuzwa kwa Jerry Quay;Gunnersaurus* ...Moja Kati ya Washehereshaji(Katuni) inayofurahisha Mashabiki Katika Uwanja wa Ashburton Groove Lakini Vilevile Hakusita Kupiga Kelele Mauaji ya Raia wa Nigeria Dhidi ya Polisi wa Kikosi Maalum Cha Uhalifu Cha SARS
Lakini Vilevile Hakusita Kupiga Kelele Kubaguliwa na Wajerumani wakiongozwa na Rais wa *Deutscher Football Association (DFB) Bwana Reinhard Grindel* na Washirika wake na Kujiondoa Rasmi Katika *Timu ya Taifa Mnamo wa Julay 22 Mwaka 2018*
Mbali na Kutocheza Katika Mechi Yoyote ya *Arsenal FC* Mesut ozil Ni Mchezaji wa *Pili wa Arsenal Kulipwa Mshahara Mkubwa Kiasi Cha £350,000 kwa wiki Zaidi ya Tsh Billion 1 Kwa Wiki Akiwa Nyuma ya Pierre Emerick AUBAMEYANG Ambaye anamzidi Ozil kwa Bonus* Ingawa Mshahara wako Sawa na Pia Ni *Mchezaji wa 4 Anayelipwa Vzuri katika Ligi Kuu ya England Nyuma ya Gareth Bale £600,000 Kwa Wiki.....David De Gea anayelipwa £375,000 Kwa Wiki...Pierre Emerick AUBAMEYANG £350,000 kwa Wiki na Mesut Ozil £350,000 Kwa Wiki*
*Mesut Ozil* Amecheza *Mechi 600,Magoli 108, Assist 216,Red Card 3,Yellow Card 43 Katika Ngazi ya KLABU Akiwa na Vilabu vya Schalke 04,Werder Bremen,Real Madrid na Arsenal .....Huku Kwa Klabu ya Arsenal tu Akifunga Magoli 44,Assist 77 Katika Mechi 254 na Katika Level ya Timu ya Taifa ya Ujerumani Amecheza Mechi 92,Amefunga Magoli 23 na Assist 40*
*Good Bye Mesut...Ya OzilM10....Once a Gunner, always GUNNERS*
View attachment 1607662View attachment 1607668