Wapwa: Huyu ni Baba mzazi wa mashambuliaji wa Arsenal Pierre Aubamayang ambaye naye kitaaluma ni kocha na si Kocha tu ,kocha wa kiwango cha juu ,kuna muda alikuwa anafundisha timu ya Taifa ya Gabon
Hapa yuko na jezi mpya ya Arsenal yenye namba 14 ya mwanae kama sehemu ya kumsupport ,ni jambo linalotia faraja sana kwa Mzazi kukuunga mkono kwa kiwango hichi
Nachofahamu Mimi wapo wachezaji wachache wanaozaliwa na mashabiki wao mfano mchezaji anapozaliwa pacha hasa wa kike na wakiume ,moja kwa moja yule wa kike huwa anakuwa shabiki kindakindaki wa kaka yake kama ilivyo kwa Phill Neville yule aliyecheza UTD pamoja na Ighalo ambao wao wamezaliwa na pacha wa kike
Pia wapo mapacha wa kiume ambapo moja anacheza moja hachezi ,automatically yule asiyecheza huwa shabiki ,au hata ikitokea wote wanacheza huwa na element za kushabikiana
Nakumbuka kisa cha wachezaji mapacha wa Iran World Cup ya 2018 Russia Mehrdad Mohamed Keshmarzi na Milad Mohammadi Keshmarzi Hapa moja huwa anaitwa timu ya Taifa ambaye ni Milad lakini Mehrdad huwa haitwi pamoja na ukweli amewahi kuitwa
Lakini wakati wa World cup na maisha yote huwa anamsupport vilivyo nduguye ni jambo linalotia faraja sana
Nakumbuka hata nami wakati nacheza ndugu zangu wa familia na ukoo wetu kwa Baba na kwa Mama wote walikuwa wananisupport
Nakumbuka nilipozifunga timu hizi Simba na Yanga katika Career yangu zilileta natafaruku ndani ya familia
Kifupi nimefurahia sana kuona Mzee Aubamayang alivyomsupport wanae kwa kiwango hicho ,Kweli Damu nzito kuliko maji ,ila somo hapa ni Wazazi msupport watoto wenu katika mapenzi yao na mchezo husika
Kutoka kwa
tigana Lukinja