Wakuu updates basi ili tupate cha kuzungumza kwa manyumbu
Nani uyo alivimba juu ya uyu legendary wa arsenal?Aaron Arsenal njoo bana ufanye maupdates ingawa kuna jamaa alikubeza kwamba ' nayeye anaweza kuunogesha huu uzi kwa kuleta infos'...
Ila champions league kawaachaje pia?Huyo Ancelloti kakaa Msimu Mmoja na Nusu Kawaachaje Napoli? Wana hali mbaya kwenye Ligi Wakati Sarri aliiacha Napoli ya Moto
Everton na Arsenal matatizo yao ni tofauti,.
Huyu Emery kwa kweli utafikiri alitumwa kuja kutuvuluga!.. Huwa nakaa nawaza, hivi alifikiria nini kumuuza Ramsey halafu wakati huo huo anamuweka bench Ozil!. Toka aondoke Carzola angalau Ramsey alikuwa amefanikiwa kuziba pengo lake!!.. Kiukweli kuanguka kwa timu yetu kumesababishwa na yule mjinga kumuuza Ramsey!..Hii Bodi kwa kumdharau RAMSEY waliyumba kwa kweli, Yaani leo tunahusishwa na Rabiot wakati Mid wa aina yake tulikuwa naye kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Xhaka, torreira na Ozil kwisha habari, ikiwezekana na Martinelli ale ubavu wa huku kwa Nelson.Granit Xhaka, Dani Ceballos wamejumuika na wenzao katika mazoezi ya jana na leo.
Inategemewa kumuona Ceballos au Xhaka akishirikiana na Toreirra katikati ya dimba.
Nyumbu una timu ya hovyo fujo nyingi, ingekuwa unaongoza ligi tusingekuwa tunaingia humu.
Kimsingi mechi ya leo ni ngumu sana!.. Kitu kinachonipa matumaini ni kuwa kocha keshaanza kuibadili timu japo hatujaanza kupata ushindi!.. Hebu fikiria timu haina full backs (wote majeruhi), mabeki wa kati wanafungisha ovyo bila sababu, Chambers, holding majeruhi.. Yaani saka anacheza namba tatu!.. Mechi ya leo naamini tutapigana sana.. Lakini napenda kuwaasa ndugu zangu wana Arsenal kama tukifungwa leo tusikate tamaa na kuanza kumlaumu kocha!.. Wote ni mashahidi mechi iliyopita tulicheza vizuri na viwango vya wachezaji Ozil vimeanza kuboreka, sema kuna mapopoma siku ile walituharibia ushindi wetu na kitupa majonzi tele!.. Leo natumaini tutakipiga vizuri kabisa na kuna uwezekano mkubwa wa kushinda hii mechi kama tutadominate mpira, lakini pia tunaweza tushishinde kutokana na full backs wetu wote watatu kuwa majeruhi na centre backs wawili pia kuwa majeruhi.. Kea hiyo tukifungwa tusikate tamaa!.. Hebu fikiria kocha amepokea timu toka kwa yule popoma aliyemuuza Ramsey na kutultea balaa pale kati!.. Kiukweli kitendo cha kumuuza Ramsey na kumpeleja Miki kwa kumkopo kimesababisha timu isiwe na balance kabisa.. Mimi bado naamini Miki ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kutusaidia ukilinganisha na hawa waliopo.Leo ndo leo akikaa Kati MATTEO G tutakula tena mvua kama kawaida yetu sisi wazee wa sare na Vipigo tusijipe Matumaini mechi ya Leo hata juzi nilisema humu kwa sasa tupotupo tu hatujui tunachokitaka sisi mashabiki wa Arsenal huwa tunapenda sana KUJIPA MATUMAINI ila Leo naona wote tupo neutral hili ndilo linalotakiwa kwa sasa sababu hatuna timu ya Viwango ya kushindana na wakubwa zetu kwa sasa
Niwe mkweli sababu sitaki stress mechi ya leo Arsenal nampa 40 % Manchester 60 % kushinda ila lolote linaweza kutokea katika Mpira wa Miguu
MIMI NINA MIAKA 20 NAISHABIKIA ARSENAL YANGU ILA NKIONGEA UKWELI NAONEKANA SIO SHABIKI WA DAMU ILA UKWELI UNAKUWEKA HURU SANA NA NDO ITIKADI YANGU KATIKA MAISHA YANGU BINAFSI PIA HAITAKIWI KUFICHA UKWELI KAMWE
COYG !! HAPPY NEW YEAR TO YOU ALL
Sent using Jamii Forums mobile app