Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kwani malengo ya Arsenal ni yapi tofauti na kushiriki league tu ?
 
Wakuu wa Gunners naona maoni tofauti tofauti yanamiminika.

Jana mimi pia nilikuwa Leicester kushuhudia Arsenal ikiwadhibiti Leicester na kweli hadi mapumziko mambo yalikuwa 0-0.

Mambo yakaanza kuharibika kipindi cha pili ni makosa ya kiufundi.

Bodi ya Arsenal yote jana ilikuwepo uwanjani King Power kushuhudia kama ni kweli Arsenal imeshuka kiwango ambacho kinatarajiwa kutoka kwenye hii timu.

Baada ya kushuhudia Arsenal ikicheza vile kipindi cha kwanza na baadae kufungwa, bodi imeamua imuachie Unai Emery aendelee hadi mwisho wa msimu.

Bodi ya Arsenal imeridhika na viwango vya uchezaji wa timu yetu ingawa lolote laweza kubadilika khasa iikiwa baada ya Xmas tupo nafasi ya 7.
 
Board ya arsenal ni kichefu chefu kwakweli na kwa style hii sielewi kwanini walimtimua mzee Wenger, heri wangemuacha babu ila wangemuongezea wachezaji wa kazi tu.
 
Nikikutana na taarifa kama hizi za kumwamini Emery nazidi kuchukia soka.

Timu yangu ya Arsenal ina huruma sana na ndio imetufikisha hapa tulipo leo.
 
Mazeee good news toka London Emirates hazijatoka tu?kama Unai ataendelea kuwa kocha next match ntaliaga jukwaa rasmi na pia kama Mashabiki London wanaipenda Arsenal ni vyema uwanja uwe mtupu halafu tuone bodi na Mashabiki nani wana nguvu
 
Sio wa kuwajibu hao mkuu,unapoteza muda
 
Kwanza sisi mashabiki wa team nyingine tunampenda Unai hana tatizo kabisa ,watu walilialia Ozil acheze akamchezesha wakafungwa kabisa ,mashabiki wa arsenal wanampa wakati mgumu kocha bora kabisa Europa 3,ligue 1 kibao ....
Umeandika ujinga wa kufungia wiki....
 
Whaaaaaaaaaaaatttttt???????????!!!!!!!!!!

Ongeza sauti,sijakusikia mkuu
 
Baada ya mwezi huu Nikimwona huyu mzee wa kihindi tena katika bench tena.......nitafanya maamuzi magumu
 
Hao bodi wapumbavu sana hamuwezi mkawa mmefungwa halafu ukasema tumecheza vizuri na mnazidi kushuka nafasi kutoka ya 4 kuna ya 5 sasa hivi ya 6 next weekend ya 7 wenzenu wanapanda nyie mnashuka halafu bod iseme eti timu inacheza vizuri Chelsea ambao walikuwa chini kule tukawacheka na Lampard wao ndo wako nafasi ya tatu, Leicester ambao walikuwa chini kule ndo wako nafasi ya pili kweli halafu bodi waseme tuko vizuri akiendelea Huyu mhindi tutapona kushuka daraja tu msimu ujao hata uropa tutaiangalia kwa kideo tu tukiwashuhudia wenzetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…