Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Liverpool naweza kupanga kikosi leo kwa mechi inayofuata na nikawa sahihi kwa asilimia 85, timu inajulikana na wanapangwa wachezaji wazuri. Arsenal timu haieleweki.

Leo mara Willock, kesho Lt11 benchi mwaka wa pili huu kikosi chetu hakieleweki siku akipigiwa kelele anapanga kikosi kizuri. Haya majaribio sijui yataisha lini.

Hivi kwa kiwango cha Chambers na Frankfurt kuna aliyetegemea aanze benchi jana? Unampanga Maitland ambaye ni kiungo.

Ozil akose namba mbele ya Willock hivi ni vichekesho vinapatikana kwa Emery tu.
 
Halafu kuna watu wanakwambia UNAI ni kocha , sijui mpira wanauangalia wapi,?

Mimi Jana nilikuwa na mashabiki wa man u nikawaambia Ole mnamlaumu sana lkn mm nataman hata tungekuwa na ole ,

Nikawaambia man u kwasasa inajengwa na haina wachezaji wengi wazuri ,kwahiyo bado Ole anapakujitetea ,

Ole amejitanabaisha anacheza kwa press , lkn hana wachezaji wazuri, na ana Kikosi cha kwanza tayari ,

Nikawaambia Sisi tuna kocha mbovu kuliko ,msimu wa pili huu hawajui wachezaji wake awatumie vipi


Sasa hivi tulitakiwa tuwe nafas ya pili kabisa


Point dhid ya Watford kapoteza kwa tactic zake mbovu na sub mbovu

Mech na totenham pia tumekosa point 3 clear kabisa


Mech ya Liverpool wengi tulitaman sana apange kikosi cha kueleweka Tuone kipimo halisi cha timu YETU , akaja na watoto wa umiseta
 
72nd min: Arsenal losing 2-1 and take off Xhaka

84th min: Arsenal winning 3-2

Coincidence? I think not. Get Xhaka out of Arsenal FC.
 
LUCAS Toreira ni mwepes na anakaba sana tofaut na xhaka.

Xhaka anapocheza DM ndiye uchochoro wa njia ya mashambuliz mabeki ,pia toreira akicheza pembeni(BOX TO BOX MD) yaani kwa mfumo wa 4_3_3 anakuwa anapoteana sana.

Kama unai Emery anataka kuwatumia xhaka na toreira wacheze pamoja kwa mfumo wa 4_3_3 bas DM acheze toreira na pale anapo cheza toreira acheze Ceballos .

DM akicheza toreira kiukwel pale Kat huwa panatulia sana.

Jana goli la pili la Aston Vila xhaka kaanza kumsindikizaa jamaa kwa macho mpaka ndani ya box kitu ambacho alikuwa anauwezo wa kumalizana nae mapema kabla hajaingia eneo la hatar.

#UNAI OUT


72nd min: Arsenal losing 2-1 and take off Xhaka

84th min: Arsenal winning 3-2

Coincidence? I think not. Get Xhaka out of Arsenal FC.
 
Hahaha eti watoto wa UMISETA!
 
Aston villa ambao wapo chini kabisa wametusumbua itakuja kuwa man u OT. hiyo mechi hata draw hatupati
 
mimi mtu anayemtetea huyu gabachori huwaga simwelewi kwasababu moja tu.......BANIANI AMEONDOA ASILI YA SOKA LETU..........Highbury na Emirates ilikuwa ni kaburi la wagagagigikoko wote,kila mtu akijua anaenda pale wikend alikuwa anajiandaa kuutafuta mpira kwa tochi na hata away tulikuwa tuwachachafya iwe kwa matokeo chanya ,hasi au sare lakini leo hii Aston Villa,Watford wanatusumbua sisi?yaani ladha hakuna zimebaki kero tupu......leo hii GUE amekuwa mwokozi wa timu wakati una wachezaji kibao unawatumia out of position mpaka wanaonekena wabovu na kuwasababishia chuki kwa mashabiki kwa kushindwa kuperform katika nafasi wasizozimudu....hivi huyu Granit angecheza juu nani angemtukana leo hii?nani kamwambia urefu unakaba?ingekuwa hivyo NGOLLO asingecheza mpira,baniani aache ubishi amtumie LT11 DM huyo PEA anayemweka mjini siku akiflop kazi hana............maana mimi nna wasiwasi hata kama hao kina ROB,KT,HECTOR,DINO wapone na aletewe na wa nyongeza bado atapata tabu kupata matokea kwa ujuha wake

kwa moyo mkunjufu nasema hivi BANIANI EMERY OUT
 
72nd min: Arsenal losing 2-1 and take off Xhaka

84th min: Arsenal winning 3-2

Coincidence? I think not. Get Xhaka out of Arsenal FC.
hapana hapo sikubaliani na wewe,wakuondoka hapo ni kocha tu maana huyu xhaka unayemkataa leo akija kocha mwingine akamtumia ipasavyo anashine vizuri sana?shida ya UNAI ya kuamini urefu unakaba ndio inayofanya washabiki wamchukie GX,jamaa anachezeshwa nafasi asiyoimudu na mambo kama haya ndio yalisababisha tukampoteza AOC kwa kumtaka acheze wingback wakati yeye anaamini kabisa kuwa anaperform vizuri akicheza kiungo cha kati.....ukiangalia kwa kina utaona kuwa kuna mahali tunakwama maana wachezaji wengi walioondoka kimtindo huu tuliwatamani warudi.....upuuzi wa BANIANI hauna tofauti ule wa SARRI kumweka KANTE juu na kumshusha mwanawe kipenzi JOGINHO chini..........nakwambia hivi huyu XHAKA akienda pale liverpool tutaomba ardhi ipasuke tutumbukie ndani.....

BANIANI UNAI OUT
 
Wazee naomba ikumbukwe ni sisi ndiyo tulimkataa Wenger tukisema kachoka kaishiwa mbinu.

Unai kaja. Tukashangilia.

Leo hii hata hana muda mkubwa tunayumbishwa na mafanikio ya Man City na Liva. Liva alianza kuiunda hii timu 2015 tukumbuke magumu aliyopitia.

Cuty akaona isiwe kesi akaamua kuingia sokoni kununua mafanikio, same na Chelsea na Man U. These are big spenders than Arsenal.

So we headed to the final with a big spender. We got beat up tunanuna.
Emery kaamini vipaji, huku kuamini vipaji ndiyo kunafanya tusiienjoy timu.

Am saying f... this kama anaenda basi aende but bro is what we deserve.
 
mkuu kwa huyu UNAI hata apewe 1billion pound hana maajabu kumbuka kilichotokea pale PSG kila aina ya mchezaji aliletewa na kipi alichokifanya?

na kaa ukumbuke vizuri zile shangwe za mashabiki kama ulizifuatilia vizuri kisaikolojia washabiki walikuwa wanafurahia kuondoka kwa WENGER na sio kuja kwa UNAI amini hivyo,

kwa furaha iliyokuwepo muda ule hat kama angetangazwa ZAHERA ndio kocha wa timu hakuna ambaye angenuna kwani mioyo yao iliamini kuwa mchawi wa mafanikio ya timu ni ARSENE lakini walisahau kujiongeza kuwa anaondoka AW anakuja nani?

UNAI OUT
 
Ana kiburi sana huyu fala
 
Hahaha kweli watu wamemchoka.

Aisee hata akienda. Nina imani naye
na uzuri wake watu wanasema haya timu ikiwa haijapata matokeo mabovu.......

mechi tatu zilizopita

AWAY vs WATFORD DRAW
AWAY vs FRANKFURT WIN
AWAY vs ASTON VILLA WIN

maana tungekuwa tunafungwa then ndio tunayasema haya mngetuona sisi sio mashabiki wa kweli.


UNAI OUT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…