Tunakumbushana Kidogo
Kuelekea Mechi Dhidi ya BURNLEY EMIRATES.
Tumecheza nao mechi 107 mashindano yote
Tukishinda 53

Wakitufunga 33 na Tumetoka nao sare 21

Katika mechi 10 za mwisho kukutana nao Hawakuambulia ata Sare moja Tukiwafunga zote zikiwemo mechi za nyumbani tulizompiga vipigo vya 5-0,3-0,3-1,3-1 n.k.
Tunawakaribisha nyumbani tukiwa na faida ya kuwafunga mechi ya mwisho kukutana nao ambayo tulicheza uwanjan kwao Turf Moor na kuwafunga 3 - 1 mabao yakiwekwa na Aubameyang

️

️ na Nketiah

️ dakika za majeruhi

Kikosi kilichoanza Siku hiyo;Mfumo 4 2 3 1
Kipa:Leno Mabeki:Monreal,Mavropanos,Mustafi,Lichsteiner Viungo:Guendoez,Elneny,Willock,Iwobi,Mkhitaryan Fowadi: Aubameyang.

Nategemea Kuona mabadiliko makubwa ya kikosi kwa Chaguzi na maingizo ya wachezaji wapya tuliowasajiliwa msimu huu
Tukumbuke pia nao wanaingia uwanjani EMIRATES wakitoka katika Ushindi wa mechi yao ya kwanza na Southampton wakimfunga 3 - 0 uwanjani kwao Turf Moor.
Mara ya Mwisho kutufunga ilikuwa 02 Disemba 2008 walitufunga 2 - 0 kwao wakatutoa katka kombe la Ligi EFL Cup hatua ya robo fainali.
Ila wajiandae kubeba mzigo wa magoli

wasichezeee kabisa huu moto unaopamba bila moshi. Bunduki mpya, Risasi mpya, Arsenal Go Go Unai Go Go..