Arsenal wameweka vipaumbele katika usajili wa msimu ujao.
1. Kiasi cha fedha za usajili ni pauni milioni 40 pamoja na fedha yoyote itakayotokana na mauzo ya wachezaji kadhaa kati ya Mustafi, Carl Jenkinson, Mesut Ozil, Laurent Koscielny, Nacho Monreal na Saed Kolasinac.
Hao wachezaji hapo juu wanaleta kama pauni milioni 50 kama wakiuzwa.
2. Lacazette na Aubameyang hawataondoka Arsenal na mikataba yao itaboreshwa, ingawa kuna hoja ya Arsenal kufikiria dau kubwa kwa Aubameyang la kutoka China endapo litawekwa mezani.
3. Kulingana na bajeti iliyopo (milioni 40) na nyongeza kidogo Arsenal bila shaka watamsajili Yannick Carrasco kwa pauni kati ya milioni 20-25 ambae walijaribu kumsajili mwezi January mwaka huu.
Hivyo nafasi ya mshambulaji wa pembeni itakuwa imejazwa ingawa kama nilivyoema hapo awali kwamba Arsenal pia wanamfuatilia Ryan Fraser wa Bournemouth ambao wameweka ada ya usajili si chini ya pauni milioni 30.
4. Nafasi ya beki wa kati ndio anasajiliwa Joaquim Andersen ambae ni beki mzuri kwa kuumiliki mpira na utulivu akiwa kwenye nafasi yake na huyu ataziba nafasi ya Stephan Lichtsteiner na atasaidiana na Sokratis huku Laurent Koscielny akishuka bench au kuuzwa.
5. Denis Praet anakuja kujaza nafai ya Aaron Ramsey ingawa ripoti ya opta index yaonyesha Praet kutofikia kiwango cha uchezaji cha Ramsey lakini kocha Emery atatarajiwa kubadili mfumo wa uchezaji wa timu hiyo.
6. Kuna mshambuliaji mwingine wa pemneni ambae Arsenal wanataka aje kuziba nafasi ya Danny Wellbeck nae huyu aitwa Alexis Claude-Maurice, ambae klabu yake ya Orient ndio alikotoka Matteo Guendouzi.
7. Nafasi ingine ambayo Arsenal wanatarajia kuziba ni ya beki wa kushoto na beki mdogo wa Celtic aitwae Kieran Tierney anaonekana anafaa kuja kuziba nafasi ya Nacho Monreal na Saed Kolasinac
8. Denis Suarez anarudi Barcelona baada ya kufeli kuonyesha umahiri wake..
9. Arsenal haitasajili kipa na kipa namba mbili kwa Leno atakuwa ni Emilian Martinez ambae alipelekwa timu ya Reading kwa mkopo.
Hivyo basi tuanze kusikilizia kati ya jumatatu au jumanne kwa kuanzia na usajili wa kwanza kwa Arsenal wa mshambuliaji wa pembeni Yannick Carrasco.
Hivyo tutege masikio kusikilizia majina haya: beki wa kati Joaquim Andersen, beki wa kushoto Kieran Tierney, mshambuliaji kiungo (attacking midfielder) Denis Praet, Yannick Carrasco, na mshambuliaji Alexis Claude-Maurice.