Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hahahahahahahahah mkuu haya ni matusi makubwa hahahahahahahahah
 
we mkifungwa ndio unakuja na visababu vyako uchwara, ila kabla ya game wewe ni hodari wa kubinua mdomo kwamba mtashinda, mpira hauchezwi mdomoni, timu yenu ni mbovu mbovu sijapata kuona yani imeoza
Mkuu nimecheka sana eti Timu imeoza hahahahahahahahah
 
Vipi mkuu unawafahamu wachezaji hasa uwezo wao uwanjani!... Naombea dili ifanikiwe maana beki ya mwaka huu imetuumiza ile mbaya
 
Ni wazo zuri kumuuza wala kulikubali, mie naacha uamuzi wa mchezaji mwenyewe, japo napenda auba abaki,

Zaha sawa ni msumbufu, tena msumbufu kweli japo wakati mwingine anakuwaga kazi bure, lakini huyu labda wa achukue nafasi ya iwobi ila sio auba.

Ziyech Usimuwekee mategemeo makubwa saaana, nadhani anaweza asing'are EPL
 
Wakuu nasikia carasco anatua any time.......niulize tu watu wa data ni kweli?
 
Hii ndio habari mkuu ..mimi naamini kwenye Arsenal ya vijana wadogo, wenye talent ,wasio na majina na wenye njaa ya kufanikiwa kama kocha wetu Unai Emery, na kwa uongozi wa arsenal uliopo sasa hivi wana idea kama hiyo, naamini hiki kitu kitajatokea sio muda.
 
kitengo cha Richard hiko

Usajili News na Arsenal reshuffle (mabadiliko ya ndani)

Arsenal yaongeza dau kwa wachezaji wawili wa Samprodia kufikia pauni milioni 44


Mkuu umenipa kitengo kabisa.

🙂🙂

Carrasco anataka kuondoka China kurudi Ulaya na Arsenal wameweka offer mezani na wanasubiri kama ataikubali.



Halafu, wana Gunners mwamkumbuka huyu?

Atakuwa na Unai Emery kuanzia msimu ujao akichukua nafasi ya Steve Bould ambae amepelekwa kufundisha vijana wa umri wa chini ya miaka 23 akimsaidia mkuu wa Academy Per Mertesacker.

Steve Bould amekuwa "demoted" kutokana na Arsenal kucheza vibaya sana msimu ulopita.

Smaue Umtiti haji tena Arsenal kutokana na kushindwa kufuzu kucheza CL.

Ryan Fraser anaweza kuja Arsenal ingawa Bournemouth wamepania kuwasumbua Arsenal.

Tutaendelea kupeana Updates.
 
Arsenal na habari za Usajili:

Arsenal wameongeza dau la kutaka kuwasajili wachezaji wawili wa Samprodia
Dennis Praet na Joachim Andersen.


Joachim Andersen


Arsenal wameweka tena mezani Euro milioni 50 sawa na pauni milioni 44.

Joachim Andersen ni mchezaji wa kimataifa na pia ni beki mshahara wa Denmark na Arsenal wanataka Anderson achukue nafasi ya "boss" Laurent Koscielny.

Arsenal wameamua kufanya kweli baada ya kusikia Tottenham wakizongea kwenye viunga vya Serie A nchini Italy.

Denis Praet ni mchezaji wa kiungo wa timu ya taifa ya Belgium na aliwahi kuchezea Arsenal akifanyiwa majaribio akiwa na umri wa mika 16 kabla ya kwenda kwenye timu ya Anderletch.


Denis Praet

Samprodia ni timu ambayo imekwishfanya biashara na Arsenal ilipomruhusu Lucas Torreira asajiliwe na wakongwe hao wa kaskazini mwa jiji la London.
 
Wakuu nasikia carasco anatua any time.......niulize tu watu wa data ni kweli?
Carrasco ni mwendawazimu, ndio maana el cholo alimuachia easy, labda aje ajirekebishe arsenal..
Ni mchezaji msumbufu akiwa na mpira mguuni lakini hana madhara makubwa saana lango mwa mpinzani.
 
Atajirekebisha tu kama auba.....
Ila si anaweza walisha washambuliaji mipira mingi???
Carrasco ni mwendawazimu, ndio maana el cholo alimuachia easy, labda aje ajirekebishe arsenal..
Ni mchezaji msumbufu akiwa na mpira mguuni lakini hana madhara makubwa saana lango mwa mpinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…