MONCHI
Klabu ya arsenal imefikia makubaliano na monchi sporting director kutoka klabu ya as Roma kule italia.
Huyu jamaa ana miaka 50 halafu ni rafiki mkubwa wa kocha wa arsenal Emery unai .
Kwa muhujibu wa IL messaggero arsenal imepeleka ofa kwa mhispaniola huyo na kusema wapo tayari kulipa release clause yake yenye thamami ya £2 M.
Mtandao huo wa italia Umesema kuwa monchi amefikia makubaliano na arsenal na atajiunga nao kabla ya msimu huu kumalizika.
Ndiyo, arsenal wanamwitaji sporting director mwingine baada ya alikuepo Sven mislintat kuondoka mapema mwezi huu.
Monchi anataka kufanyia kazi uingereza lakini sevilla ambayo ni klabu yao ya zamani yeye pamoja Emery unai wanamwitaji kwa udi na uvumba.
Unaambiwa jamaa amejizolea sifa baada ya kuwaibua kisoka wachezaji Kama Sergio Ramos, Dani alves na Ivan rakitic.
Pia aliyekua winga wa zamani wa arsenal Marc overmars ni mtu mwingine anayewindwa kwenye nafasi hiyo lakini Taarifa zinasema hawezi kuiacha Ajax kwa sasa.
Mjerumani mislintat alijiunga na arsenal mwaka 2017 akitokea borussia Dortmund na ni yeye aliyehusika kwenye sajili zote nane kuanzia kipindi hicho hadi sasa.
Katika moja ya usemi iliyosemwa siku pale arsenal walisema kuwa mislintat alifanya kazi kubwa na nzuri sana pale Emirates.
Mislintat aliachana na arsenal February 8 kmwaka huu na kusema kuwa anaenda kutafuta changamoto mpya.
Pia huyu jamaa mislintat aliusika katika kumleta mshambuliaji Pierre aimeric Aubameyang klabuni hapo kwa kiasi cha £ 56 M January 2018.
Mislintat ni sporting director mwenye sifa nzuri ila hata huyu monchi kama atakubali kujiunga kama taarifa zinavyosema arsenal watakua wamepata mtu sahii kwenye swala zima la usajili.
Nakumbuka mwaka Jana Barcelona walikua wakimtolea macho kabla ya kumpa Eric abidal wadhifa huo.
Sent using
Jamii Forums mobile app